Jinsi ya kusamehe

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,348
559
Naomba msaada wenu wandugu
kuna mtu kanikosea, mtu mwenywe harekebishiki,
hasira zinanimaliza, hadi nasikia kizunguzungu, nahisi magonjwa yananinyemelea.

Naomba msaada jinsi ya kuweza kutoa hii sumu kwenye damu yangu niendelee na maisha.

mtu mwenyewe namuona kila siku. Ni jamaa wa karibu. Na tumejenga jirani. Hatuwezi kuhama.

sasa nimekuwa mgonjwa najua tiba ni kusamehe ila sijui nitumie utaratibu upi.
pleeease???
 
Naomba msaada wenu wandugu
kuna mtu kanikosea, mtu mwenywe harekebishiki,
hasira zinanimaliza, hadi nasikia kizunguzungu, nahisi magonjwa yananinyemelea.
Naomba msaada jinsi ya kuweza kutoa hii sumu kwenye damu yangu niendelee na maisha.
mtu mwenyewe namuona kila siku. Ni jamaa wa karibu. Na tumejenga jirani. Hatuwezi kuhama.
sasa nimekuwa mgonjwa najua tiba ni kusamehe ila sijui nitumie utaratibu upi.
pleeease???

Kama kosa hilo haliko likely kurudiwa na huyo mhasimu wako, umwombe Mungu kwa nguvu ili akusaidie kumsamehe. Uzuri ni kwamba unatambua wewe ndiye unayeumia zaidi kwa kuendelea na kinyongo.

Iwapo kosa dhidi yako litarudiwarudiwa, ni dhahiri unapaswa kuchukua hatua za kuliachisha kwanza (kisheria, kijirani, kidini, nk) ili hatimaye msamaha uwe na tija.
 
Piga magoti kwa Mungu ukimuomba akuepushe na hasira uliyonayo juu ya huyo mtu pia ukimuomba amsamehe kwa tendo alilotenda basi hata wewe utaongezewa thawabu kumbuka kusali kila siku na vile vile ukimuombea huyo mtu aliyekutenda vibaya kwa kusali hata ile hasira uliyonayo na mambo mengine uliyokuwa unamuwazia yeye basi yote yataondoka mtangulize Mungu mbele yako katika hili jambo kwa kuwa hakuna tiba zaidi ya kwenda mbele kwa mwenyezi Mungu na kuomba msaada wake kwa mema na sio mabaya
 
Dawa ya wewe kuondoa yote haya ni kupatana na e na kuweka tofauti zenu pembeni utaishi kwa amani na hayo magonjwa yataondoka ..jifanye mjinga pole Haika
 
Naomba msaada wenu wandugu
kuna mtu kanikosea, mtu mwenywe harekebishiki,
hasira zinanimaliza, hadi nasikia kizunguzungu, nahisi magonjwa yananinyemelea.
Naomba msaada jinsi ya kuweza kutoa hii sumu kwenye damu yangu niendelee na maisha.
mtu mwenyewe namuona kila siku. Ni jamaa wa karibu. Na tumejenga jirani. Hatuwezi kuhama.
sasa nimekuwa mgonjwa najua tiba ni kusamehe ila sijui nitumie utaratibu upi.
pleeease???


Pole sana Haika.
Nakuelewa hali unayopitia. Mimi pia nimeshawahi kuumizwa sana. Sikujua hata nianze wapi kusamehe.
Kwa taarifa yako, aliyekuumiza either hajui umeumia kihivyo, au atapenda kukuona unaendelea kuumia. Cha muhimu kujua ni kwamba - afya ni yako, maisha ni yako, na future ni yako. Usife kwa kihoro, kataa hali hiyo. Kuna ushauri umetolewa hapo juu - just ignore the chap, basi. Tena ukikutana nae toa tabasamu, msalimie kisha upite. tafuta mtu wako wa karibu sana unayeweza kumuelezea swala hili, na kila unapposikia kama unataka kupasuka, mwambie na atakushauri na kukusikiliza.
The best weapon - INGORE HIM/HER.
Ila pia, amua kumsamehe na kutokuweka mazingira tena ya wewe kuumizwa na yeye.
Pole sana na Mungu akusaidie.
 
Kama unampenda Mungu na especialy Yesu fahamu yafuatayo:-
1.Hasira ni dhambi
2.Achilia upate kuachiliwa ( Usipomsamehe huyo mtu hata wewe kwa dhambi ya hasira hutasamehewa).
3.Mungu ametwambia ktk neno lake hatutajaribiwa zaidi ya tuwezavyo kusitahimili.
4.Unashughulika na pale ulipoangukia na kukiacha kisiki kilichokukwaza salama salimini ( Tumepewa AMRI na MAMLAKA ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za adui kwa jina la Yesu ) maana yote maudhi,ugomvi,hasira nk nk vyatoka kwake.kusudi jina la Bwana litukanwe kwa kukuona wewe mwana wa Mungu unajimaliza kwa uchungu kama MPUMBAVU.
 
Kwanza tuambie amekukosea nini? Au amekutafunia wife maana msamaha wa hapa unahitaji moyo kwakweli. By the way pole sana
 
Pole sana. Lakini hamna nji rahisi kama wewe kumuomba msamha kuliko kutegemea kupata msamaha kutoka kwake.
Au kusameheana. Na hilo kwa kawaida ukilifanya yy hujiona mshindi na wewe unabaki ukiwa na amani rohoni.
Mimi kuna mpangaji mwenzangu alikula mke wa mwenzake na jamaa akawakuta. Unaweza kukubali aliyeliwa aliomba msamaha na mpaka leo mwaka wa 3 wako wote nyumba 1?
 
Dawa ya wewe kuondoa yote haya ni kupatana na e na kuweka tofauti zenu pembeni utaishi kwa amani na hayo magonjwa yataondoka ..jifanye mjinga pole Haika
ogopa hii kitu sana maana utakuwa unabaki na kihoro
 
Nakushauri usome maneno haya hapa chini, kuna maelekezo ya msingi kabisa katika Biblia
Warumi 12:17-21 Msimlipe mtu uovu kwa uovu. Jitahidini kutenda yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama ikiwezekana, kaeni kwa amani na watu wote. Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:``Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana. Badala yake, adui yakoakiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kitu anywe. Maana ukifanya hivyo, utampalia mkaa wa moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

katika experience ya maisha yangu nimeona hili likiwa suluhisho kubwa sana la wanaonikosea.
(1)Ninaanza kwa kumwomba Mungu msamaha pale yumkini kwa kujua au kutojua nimekuwa chanzo cha simtofahamu hiyo.
(2) Ninamwombea aliyenikosea msamaha kwa Mungu.
(3) Ninapingana na roho ya chuki kwa jina la Yesu kwenye maombi.
(4) Ninamwomba Mungu amfungue ufahamu ili ajue kuwa amenikosea.
(5) Naomba Mungu anioneshe ni wema gani ninaoweza kumfanyia ili kuushinda huu ubaya.
(6) Nachukua hatua ya kumfanyia wema(even if is costful),
(7) Nikipata neema naweza kuzungunza nae. Isiwe na mara tu mlipokosana, bali iwe baada ya muda fulani hivi ili kama kulikuwa na hasira zipoe kabisa.

UKWELI NI HUU: HUWEZI KUUSHINDA UBAYA KWA UBAYA AU KWA KUKIMBIA, USHINDE UBAYA KWA WEMA. HAKUNA UBAYA WOWOTE UNAOWEZA KUSTAHILI MBELE YA WEMA.
 
just ignore him/her...so simple!

Mara nyingi tuwapendao ndio wanaotuumiza. It seems huyu jamaa anampenda huyo jamaa yake sana kwa hiyo hawezi kum-ignore. Cha kufanya awaambie ndugu au jamaa wa huyo bwana/bibi halafu wawapatanishe.
 
kusamehe si kazi rahisi ila ni jambo ambalo tunatakiwa kulifanya samehe wote walokuuzi na ukishasamehe sahau kabisa usiweke uchungu moyoni magonjwa ni mengi
 
Pole sana Haika,muombe Mungu uachilie hayo yaliyoko moyoni,
Muombe Mungu akupe hekima ya kusema nae ana kwa ana muweke tofauti zenu pembeni,na umuombe msamaha pale ulipomkosea wewe obvious na yeye atakuomba msamaha.Lakini kikubwa Muombe Mungu na kuzingatia kusoma verses ulizopewa na wachangiaji hapo juu Mungu atafanya kitu juu yako.Nakutakia amani ya Kristo
 
Pole sna muombe Mungu na siku zinavyoenda utazoea na kurudia hali ya kawaida ila kumbuka mwanzo huwa ni mgumu.
 
vema ukahama....Pangisha nyumba yako au Uza, Kajenge sehem ingine...!!! kama mmezaa watoto wataenda kucheza pamoja, kama chuki bado ipo, mmoja wenu anaweza fikia pabaya zaid kuhamisha hasira au chuki kwa watoto...!!! Kuhama ni moja ya solution.

Kusamehe ni njia nzuri ila inategemea na Mioyo yetu, kila mmoja ana moyo wake...Kwa kuwa hujasema umekosewa nini na aina how many times umejaribu kusuluhisha ikashindikana, kukosana Binadam ni jambo la kawaida..angalia the way unavyoweza ku-escallate tatizo kwa watu wengine kusaidia kusolve hilo tatizo...otherwise uchune...na Igore him....!!!
 
ni ngumu kusamehe ila ni muhim sana so jaribu kusamehe ili maisha yasonge mbele tena kwa amani ya bwana Yesu!ubarikiwe mpendwa!!!
 
Back
Top Bottom