Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

1. Kwanza chagua jina halafu nenda Brela kasajili jina. It's a one day process.

2. Baada ya kupata 'OK' ya jina. Nenda kwa mwanasheria akuandalie documents mbili muhimu. Hii ni The Memorandum of the Company na Articles of Association copy nne nne. This is a Two days Job.

3. Unarudi Brella na kujaza forms na ku-submit na hizo documents na unalipia - applicable fees. This is another two days job.

In total 5 working days zinatosha kusajili kampuni. Ukianza Jumatatu, unamaliza Ijumaa. Kama una mkono mrefu, unaweza kufanyiwa kwa Fast Track na ukamaliza mambo yote in a day or two.
kwa wazoefu, mtusaidie, hivi ni leseni ngapi mtu unatakiwa kuwa nazo ukianza biashara au ukifungua kampuni, aina ngapi za leseni kabla ya kuanza biashara? pamoja na zile za manispaaa, sijui jiji/miji etc.
 
Kama ni Limited Co. Andaa kama 300,000/=
what do you mean? take this example, mfano kampuni yangu nimeweka jina la kingkonglll co.ltd, na nyingine nikaweka kingkonglll investments, zote nimepeleka memo na articles, what is the difference, na kwanini ada ziwe tofauti, ipi ina ada kubwa na ipi ada ndogo, ipi inadili na nini na ipi inadili na kiwango minimum kipi...thanks.
 
kwa wazoefu, mtusaidie, hivi ni leseni ngapi mtu unatakiwa kuwa nazo ukianza biashara au ukifungua kampuni, aina ngapi za leseni kabla ya kuanza biashara? pamoja na zile za manispaaa, sijui jiji/miji etc.
It depend ni biashara gain unafanya, kama ni biashara ya kawaida leseni ni moja tuu kwa specialized business then unaomba specific license on top of general business license, lets say usafirishaji Sumatra, communications, TCRA, air transport TCCAI!

Kama utamake more than M. 20 kwa mwaka, unapaswa kujisajili TRA na kupata VAT certificate, then unalipia fiscal devices zinazotumia GPRS hivyo TRA wana monitor every transaction iliyo katiwa risiti.
Pasco
 
chash... at all; naomba kujua kuna tofauti gani katika kusajili kampuni kama sole proprietership au partnership??

Hasa katika viambatanisho wanavyotaka ili upate usajili

pia interms of gharama za usajili.
 
Last edited by a moderator:
naomba kujua kuna tofauti gani katika kusajili kampuni kama sole proprietership au partnership??

Hasa katika viambatanisho wanavyotaka ili upate usajili

pia interms of gharama za usajili .. sole proprietership inaweza kugharimu tsh ngapi na partnership pia!
 
Nilisoma hapa nikadhani rahisi, nikaanza kuhangaika kusajili, nimepiga kwata jengo la ushirika hilo hadi mwisho aw siku nikakubali hii nchi rushwa haitakwisha kamwe!! Nilifanikiwa kusajili Kampuni yangu, mwezi December mwaka jana!! Sio Siri ni baada ya kutoa tshs laki sita!!
 
Kumbuka, baada ya kusajili kampuni (Incorporation) na kabla ya kuanza biashara utatakiawa kupata leseni ya biashara (business licence) na pia kujisajili kama mlipa kodi (TIN certificate).

Nakutakia mafanikio.


Hapa wengi tunahitaji msaada jamani....nawapongeza TRA system ya kupata TIN kwa sasa ni bure na ni one day process....issue imebaki halmashauri katika kutoa lesen.....hivi hizo kodi zitapatikanaje jamani????kama mnaohusika mnapita pande hizi naomba hili wazo mzingatie(Mfano Arumeru-Arusha)....yani nafuatilia leseni toka January,nilipoenda mara ya kwanza nikaambiwa natakiwa kuwa na 42elfu,kwa biashara mpya ni kazi sana kutoa hiyo pesa na nikawaeleza watendaji lakini ilikuwa kama nawaomba chakula.....leo nimerudi naambiwa 150,000/= ili niweze pata leseni.....swali la msingi??watu wangapi watakuwa radhi kutoa hicho kiasi vijijini?kwanini tusipewe muda wa matazamio ya biashara?ili walau after a year waje kukagua wajue maendeleo ya wananchi wao?....nahisi kodi yangu inaliwa bure.....
 
Kampuni yetu ina deal pia na mambo ya company registration process (documents & forwarding the same to BRELA). Aidha tuwasiliane tukuhudumie: Our company name: PLUS BUSINESS & RESEARCH CONSULT, P. O. Box 75779 Dar, located at Magomeni- Morocco Hotel just after DD Phamacy - at new storey building. +255 (0) 657 700 315 or e-mail: plusbusinessconsult@gamil.com
 
Natafuta kwa nini forms zao za kusajili kampuni wasiziweke kwene mtandao ili watu kama sisi tunaotazitafuta tuweze kuzipata kwa urahisi?

kila form zipo kwenye website yao hata search ya jina na jinsi jina lako linavyoweza kukataliwa ama kukubaliwa vipo,pia vitu vya kuepuka kuweka kwenye majina navyo wameelezea.
mie wakati nafungua nilianzia kwenye web yao na hata nilipopeleka jina lilipita bila masahihisho.
soma kwanza kwa uelewa zaidi tu
 
Niambieni jina lake huyo binti mwenye nyodo ili nimpe taarifa Mzee Mahingila the CEO wa BRELA. Hana mchezo yule mzee


una uhakika gani kama huyo binti ana nyodo?
ulishawahi kumuona?
au tu unataka tujue unajuana na ceo wa brela?

je kama mtoa post ya huyo binti ana kisasi chake personal wewe unaingilia tu bila tu kuhoji
unajiita GT mkuu kwa hili?
 
naomba kujua kuna tofauti gani katika kusajili kampuni kama sole proprietership au partnership??

Hasa katika viambatanisho wanavyotaka ili upate usajili

pia interms of gharama za usajili .. sole proprietership inaweza kugharimu tsh ngapi na partnership pia!
business name registration(wanaiita kampuni ndogo) ndio huweza kusajiliwa kama sole propriator au patnership.gharama za usajili kwa aina yote mbili ni moja yaani sole propriator na patnership ni moja SH 6000 bila msaada wa wadau wa takrima,ila na takrima ikihusika kuna watu wanacharge mpka laki 1 .huhitaji document zozote kuambatanisha zaidi ya kujaza form ambayo inajieleza

With Company Limited ,no way kwamba inaweza ikawa sole business kwa mujibu wa Companies act 2002(kama sijakosea mwaka)ni lazima share holders waanzie wawili na maximum ni hamsini.bei ya usajili ni kubwa na maximum ni 345,000(kama haijaongezeka zaidi) na hii huitaji uandae memorundum of associations (hivi ni vitabu vinavyo ainisha objects za company na articles za company ambazo mara nyingi huandaliwa na wanasheria ,japo maisha yamewafanya hata si tusio wanasheria kuweza ziandaa kwa ubora uleule).
naamini nimeeleweka
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom