Jinsi ya kupika Ugali

hahahah
yaani mmenikumbusha ugali oops
pale kwa mamaangu mzazi -- tunakula ugali na mlenda( nsoga) aaah unashuka kama nini unashushia na Togwa jamani

kule tabora -Ugali na Mswalu akina nyie mpo

Ugali na Kisamvu ,matembele ,kimanshia sijui nimepatia spelling
DSCN0634.JPG
Mke wa raisi,huu unaonekana ni wa AZAM,mbaya hata haunogi kabisaaaa.Ugali ni dona bwana!
 
Mke wa raisi,huu unaonekana ni wa AZAM,mbaya hata haunogi kabisaaaa.Ugali ni dona bwana!


ugali wa muhogo mamy ila dona nayo isagwe ilainike kuna ile unakula kama makapi aah nikija kwako nipikie ugali wa muhogo na kisamvu sawa Ziondaughter
 
ugali wa muhogo mamy ila dona nayo isagwe ilainike kuna ile unakula kama makapi aah nikija kwako nipikie ugali wa muhogo na kisamvu sawa Ziondaughter

Karibu sana.Ila ugali wa muhogo mhhh? sijui kupika una masharti sana,mpaka moto uupatie sana.Nitakupikia wa ngano na vibua , nadhani utaufurahia mamii.
 
No one really cooks in pots this big, but this is at the school Vermonter worked at and he's cooking for tons of children.
 
[h=1]Ugali Kwa Mchuzi Wa Nazi Wa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia, Mboga Ya Matembele Na Samaki Wa Kukaanga[/h]
ugalimchuzi%20nyanyachungu%20bamia%20nazi%20matembele%20samaki%20kukaanga.JPG


Vipimo Vya Ugali

Unga wa mahindi 4
Maji 6 kiasi kutegemea na aina ya unga

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Weka maji katika moto.
2. Tia unga kidogo katika kibakuli, koroga ufanye uji.
3. Maji yakichemka tia kwenye maji uwe uji.
4. Ujii ikiiva punguza kidogo tia unga kidogokidogo na usonge ugali. Ikiwa unga ni mgumu utaongeza maji ya ule uji ulopunguza usonge hadi uive ukiwa tayari.

Vipimo Vya Mchuzi Wa Nazi Kwa Nyanya Chungu/Mshumaa/Ngogwe Na Bamia

Nyanya chungu/mshumaa/Ngogwe 7
Bamia 10
Kitunguu maji 2
Nyanya/tungule 2
Tui la nazi jepesi 2 viwili
Tui la nazi zito 2
Chumvi kiasi
Ndimu 2 mbili kamua
Bizari manjano/haldi/turmeric ½ kijiko cha chai
Pilipili mbuzi 3

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Katakata kitunguu maji na nyanya vipande vidogodogo sana kisha weka katika sufuria.
2. Iache ichemke kwa maji yake ya nyanya, ikishachemka tia maji kidogo kama robo kikombe.
3. Tia nyanya chungu, bamia na koleza ndimu, chumvi.
4. Iache ichemke. Inapokuwa tayari imeiva tia tui jepesi endelea kuacha katika moto huku unakoroga kidogo kidogo.
5. Tui jepesi likipungua kiasi chake, tia tui zito, kisha usiachie mkono koroga ikichemka kidog kiasi cha kuiva tui mchuzi tayari.

Vipimo Vya Mboga Ya Matembele

Matembele 5 mafungu
Mafuta ¼ kikombe
Kitunguu maji kilokatwakatwa 1
Nyanya/tungule 4
Chumvi 1

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Punguza miche ya matembele kwa kuikata ncha kisha osha majani yake. Acha yachuje maji .
2. Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji na nyanya hadi viivie.
3. Tia mboga, Iache ichemke kwa maji yake hadi iive. Ukiona bado haikuiva tia maji kidogo tu.
4. Ukipenda unatia ndimu kiasi cha kipande kimoja ukamue .


Samaki Wa Nguru Wa Kukaanga

Samaki Wa Nguru 4 vipande
Kitunguu thomu na tangawizi ilosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi 4
Ndimu 2 kamua
Bizari ya samaki 1 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Mwoshe samaki kisha mtie kitunguu thomu, tangawizi ilosagwa, chumvi, pilipilimbichi ilosagwa, ndimu na bizari ya samaki.
2. Mwache akolee viungo kwa muda kidogo.
3. Makaange katika mafuta hadi aive akiwa tayari.





Kidokezo:
1- Mboga matembele unaweza kuipika kwa nazi ukipenda.
2- Kuona picha za nyanya chungu au nyanya mshumaa au ngogwe kama zinavyoitwa na watu mbali, bonyeza upishi ufuatao:



 
sikujua ugali unatiwa chumvi... na kuna ugali wa muhogo (muhogo is not a cereal, it is a root)
 
Ugali wa muhogo aka (kivunde) kwa dagaa wa kigoma, pembeni una bilauli ina maji bardi kabsa game nzima mnaipiga chini ya mti, acheni masihara jamani
 
Andika kiswahili bwana aaagh mie sjaelewa, kwanza wenye kizungu hawana mpango na ugali wanaita 'very basic food' ni vyema ungeandika kiswahili
 
Back
Top Bottom