Jinsi ya kupika kunde mbichi za nazi

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
mahitaji

Kunde mbichi vikombe vinne

Tui la nazi vikombe viwili

Vitunguuu maji viwili

Vitunguu saumu kijiko kimoja cha chai kilichosagwa

Nyanya ya kopo nusu kijiko nusu cha chai

Pilipili mbichi mbili

Pilipili hoho (pilipili mboga) nyekundu nusu

Mafuta robo kikombe

Chumvi kiasi


Jinsi ya kupika kunde mbichi hatua kwa hatua

1. Osha vizuri kunde mbichi

2. Weka sufuria jikoni na chemsha maji kiasi

3. Mimina kunde katika sufuria ya maji yanayoendelea kuchemka. Acha mpaka kunde ziive; Zikishaiva ipua kunde kisha ziweke pembeni.

4. Mimina mafuta katika sufuria hadi yachemke kisha uweke vitunguu maji vilivyokatwakatwa kisha kaanga kiasi.

5. Tia vitunguu saumu huku ukiendelea kukaanga hadi mchanganyiko wako uwe kahawia.

6. Weka nyanya ya kopo katika mchanganyiko huo kisha ikaange kwa muda kiasi. Mimina kunde katika mchanganyiko huo na kisha weka tui la nazi na acha ichemke kwa dakika kadhaa.

7. Kisha tia chumvi kiasi na uache zichemke na kuchanganyika vizuri mpaka ibaki rojo rojo kiasi.

8. Pakua mboga yako ya kunde mbichi za nazi tayari kuliwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom