Mada: Fahamu mbinu mbalimbali zinazoweza kukuwezesha kupata mtoto wa kiume

Christa

Member
Dec 15, 2012
37
4
1590562970513.png


BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU MADA
Naomba msaada wenu,nimeolewa na nina watoto 2 wa kike.nifanyeje ili nipate mtoto wa kiume mana mme wangu anapenda sana watoto wa kiume hivyo ananikosesha raha.
---
Wadau naombeni kwa mwenye ufahamu ni siku gani ukilala na mwanamke utaweza kumpata mtoto wa kike/kiume? Anifafanulie please.

Sent using Jamii Forums mobile app
===
UFAFANUZI WA JUMLA WA JAMBO HILI
Njia kupata mtoto wa kiume hizi hapa

Ni kwamba, kuna njia kadhaa za kitaalamu zinazoweza kutumiwa na wazazi ili kujipatia watoto wanaoweza kujiamulia kuwa wawe wa kiume au wa kike.

Uchunguzi wa Nipashe uliohusisha mahojiano na madaktari kadhaa wakiwamo mabingwa wa masuala ya uzazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, umebaini kuwa sasa wazazi wanaweza kufanikisha ndoto ya kupata watoto wa kiume au wa kike kadri watakavyo kwa njia rahisi inayotoa matokeo chanya kwa asilimia 80 au nyingine ya kitaalamu zaidi inayopatikana pia nchini na ambayo matokeo yake huwa na uhakika wa takribani asilimia 100.

Kupitia mahojiano hayo na wataalamu, Nipashe imebaini kuwa karibu wote humtanguliza Mwenyezi Mungu katika kufanikisha jambo hilo.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum yaliyofanyika Alhamisi, Daktari Bingwa wa Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Living Colman, alisema jambo hilo linawezekana lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla wazazi kupata mtoto wa jinsia waitakayo.

Alisema wahusika ni lazima wawe na afya njema na pia mbegu kutoka kwa mwanaume lazima ziwe na ubora unaotakiwa katika kufanikisha utungaji wa mimba.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Tanzania ina watu milioni 45, huku wanawake wakiwa milioni 23, sawa na asilimia 51.

Njia ya kupata mtoto wa kiume au kike
Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya madaktari waliitaja njia ya upandikizaji wa mbegu kuwa ndiyo kubwa na ya uhakika zaidi kufanikisha utungaji wa mimba ya mtoto wa jinsia waitakayo wazazi.

Hata hivyo, Dk. Colman aliiambia gazeti hili kuwa mbali na njia hiyo inayohusisha matumizi ya maabara, ipo njia nyingine rahisi inayotokana na ufuatiliaji makini wa kalenda ya mzunguko wa hedhi wa mama.

“Hii ni rahisi zaidi na haihusishi upandikizaji wa mbegu kwenye maabara… hata hivyo, njia hii inahitaji wahusika kuwa makini zaidi katika kufuatilia mzunguko wa hedhi wa mama kwa sababu kinyume chake matokeo huwa hafifu,” alisema Dk. Colman.

Akieleza zaidi, Dk. Colman alisema wengi hujaribu kufuata njia hiyo ya kalenda na kupata matokeo hasi kwa sababu ya kutozingatia maelekezo, lakini ukweli ni kwamba yenyewe hutoa matokeo ya uhakika kwa asilimia 80.

“Kati ya watu 10 wanaokuja kwangu na kuomba ushauri wa namna ya kupata watoto wa jinsi waitakayo, nane wamefanikiwa… kwa hiyo hii inawezekana kabisa,” alisema Dk. Colman.

Ufafanuzi wa njia ya Kalenda
Wakati baadhi ya madaktari wakitilia shaka njia ya kalenda, Dk. Colman anasisitiza kuwa huleta mafanikio chanya kwa kiasi kikubwa na kwamba, lililo muhimu ni kwa wazazi kuwa na utimamu wa kiafya na kubwa zaidi ni kuzingatia muda sahihi wa kushiriki tendo la ndoa kwa nia ya kupata mtoto.

Akifafanua, Dk. Colman alisema daima, mwanamke huzalisha mbegu aina moja zinazotambulika kama ‘XX’ na hizo huendeleza ukike. Kwa wanaume, mbegu zinazozalishwa huwa ni za aina mbili ambazo ni ‘X’ (kike) na ‘Y’ (kiume).

Alisema kuwa mbegu yoyote ya mwanamke (X) ikichavushwa na mbegu ‘X’ ya mwanaume hutengeneza muunganiko wa ‘XX’ ambao mwishowe huwa ni kutungwa kwa mimba ya mtoto wa kike. Hata hivyo, inapotokea mbegu ya mwanamke ikakutana na mbegu ‘Y’ hutokea muunganiko wa ‘XY’ ambao mwishowe huwa ni mimba ya mtoto wa kiume.

Akieleza zaidi, Dk. Colman alisema kuwa sifa ya mbegu ‘X’ huwa ni uimara wake kulinganisha na mbegu ‘Y’, lakini pia huwa na mwendokasi mdogo kulinganisha na mbegu ‘Y’ ambazo zenyewe huwa hazidumu muda mrefu kabla ya kuharibika kwa vile siyo imara kulinganisha na ‘X’, na zina mwendokasi mkubwa zaidi.

“Mbegu X ipo imara lakini inapotoka huenda taratibu wakati mbegu Y ni dhaifu, lakini mwendo wake huwa ni wa kasi zaidi,” alisema.

Kwa sababu hiyo, Dk. Colman alisema wazazi wanapaswa kuzingatia kalenda ya mzunguko wa hedhi ili kufanikisha mimba ya mtoto wa kiume au wa kike kulinga na na vile watakavyo.

“Ni lazima ujue mzunguko wa mwanamke husika ni wa aina gani… kwa maana kuna mizunguko ya wastani wa siku 28 ambayo hii yai lake hutoka siku ya 14, kuna mzunguko mfupi wa siku 21 na yai hutoka siku ya 10 na pia wale wa mzunguko mrefu wa siku 36 ambao yai hutoka katika siku ya 18,” alisema.

"Kwa kawaida, yai hutoka katikati ya mzunguko wa mwanamke kulingana na mzunguko wake. Hivyo, mbali ya kujua hilo la mzunguko, ni lazima wazazi watambue tabia za mbegu X inayosafiri taratibu na Y inayosafiri haraka… hilo ni muhimu kwa sababu ndilo husaidia katika kufanikisha ndoto ya kuchagua jinsia ya mtoto," alisema.

Aliongeza kuwa wahusika wakishiriki tendo la ndoa siku mbili au tatu karibu na yai la mama kutoka, maana yake kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kutungwa kwa mimba ya mtoto wa kiume kwa vile kutokana na tabia ya mbegu Y ya kusafiri kwa kasi, maana yake ndiyo itakayotangulia na hivyo kukutwa na mbegu ya mama wakati nyingine ya X ikiwa imeachwa kwa vile kasi yake ni ndogo.

Alisema kwa sababu hiyo, wazazi wanaoota kupata mtoto wa wa kiume watalazimika kushiriki tendo la ndoa wakati zikiwa zimebaki siku mbili au tatu kabla ya yai la mama kutoka.

Aidha, Dk. Colman alisema ikiwa wazazi watakuwa na ndoto ya kupata mtoto wa kike, watalazimika kushiriki tendo la ndoa siku nyingi, kati ya 9, 10 au 11 kabla ya siku inayotarajiwa kuwapo kwa yai la mama katika mzunguko wake.

Alisema hilo ni muhimu kuzingatiwa kwa sababu kutokana na tabia ya mbegu X (kike), maana yake mwendo wake utakuwa wa taratibu na itadumu kwa siku hizo nyingi kabla ya kukutwa na kukutana na mbegu itokayo kwa mama huku mbegu Y ikiwa tayari imeshaharibika kutokana na kutangulia kwake mbele haraka na kukosa uimara wa kusubiria siku zote hizo.

“Mkishiriki tendo la ndoa mapema kidogo, kama siku mbili au moja hivi karibu na yai kutoka, mtapata mtoto wa kiume. Lakini ikiwa ni siku nyingi kabla ya hapo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kike,” alisema Dk. Colman kabla ya kutahadharisha kwa kuongeza:

“Ila hizi zote siyo kanuni za kudumu maana mwili wa binadamu hubadilika… lazima hili lifanyike kwa kuzingatia mzunguko wa mwanamke na hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya tafiti.”

Aidha, Dk. Colman alisisitiza kuwa msingi wa mafanikio ya mpango huo wa kuchagua jinsia ya mtoto kwa kuratibu mzunguko wa hedhi ya mama ni kujua kwa usahihi siku za mzunguko huo.

“Kikubwa ni mwanaume na mwanamke kujua yai linatoka lini ili mbegu X au Y zikutane na yai la mwanamke na kufanikisha utungwaji wa mimba ,” alisema Dk. Colman.

Aliongeza kuwa, endapo kuna wazazi wanapenda kuwa na watoto wa jinsia tofauti, ni vyema wakazingatia njia hiyo isiyogharimu chochote ya kuzingatia vyema mzunguko wa hedhi wa mwanamke kama ni wa kawaida, mrefu au mfupi.

Alisema eneo hilo ndilo huwashinda wengi na kupata matokeo tofauti na yale wanayoyatarajia.

“Hapa wengi huchanganya sana. Unakuta mwanamke mzunguko wake ni wa siku 28 na hivyo yai hutoka siku ya 14, lakini wawili hao wanatumia kanuni nyingine ya mzunguko mfupi wa siku 21 ambayo yai hutoka siku ya 10.

Ni lazima pia kuzingatia muda wa kushiriki tendo la ndoa kulingana na tabia nilizozitaja za X na Y,” alisema Dk. Colman.

“Hadi sasa, katika watu 10 walionifuata na kuniomba ushauri wa kupata watoto wa jinsia waitakayo, nane wamefanikiwa (asilimia 80). Kwa hiyo utaona kwamba jambo hilo linawezekana, ila muhimu ni kuzingatia masuala hayo ya mzunguko wa mama na siku ya kushiriki tendo la ndoa,” alisema.

Njia ya Upandikizaji
Mbali na njia ya kuzingatia mzunguko wa mama kabla ya kushiriki tendo la ndoa ambayo haileti mafanikio kwa asilimia 100, Dk. Colman aliitaja njia nyingine inayotoa fursa kwa wazazi kuchagua jinsia ya mtoto kuwa ni ile ya upandikizaji mbegu kwa mama kuwa ndiyo ya uhakika zaidi katika kuchagua jinsia ya mtoto.

Hata hivyo, Dk. Colman alisema teknolojia hiyo ya upandikizaji ni ghali na kwa hapa Tanzania bado ni ngeni na haipo katika hospitali za Serikali.

“Upandikizaji mbegu unaanzia kwa kutolewa mbegu mwanaume na baadaye kupelekwa maabara. Huko hupimwa magonjwa yote ili kujua ubora wake. Pia ni huko maabara ndipo wazazi wanapoweza kujua jinsia ya mtoto wao kwa asilimia 100. Na hii ndiyo njia sahihi na ya uhakika zaidi,” alisema Dk. Colman.

Aliongeza kuwa katika siku zijazo, anaamini kuna wakati hospitali yao (Muhimbili) itatimiza lengo la kuanzisha Kitengo Maalum cha Matatizo ya Ujauzito na Uzazi ambako humo, watakuwa na fursa ya kuwasaidia watu wanaohitaji huduma ya upandikizaji wa mbegu kwa ajili ya kupata watoto.

Kliniki ya upandikizaji Dar
Katika uchunguzi wake, mwandishi wa Nipashe alipata bahati ya kutembelea kituo cha tiba kilichoanzishwa miaka ya hivi karibuni katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya uzazi huku pia kikiwa na teknolojia ya kupandikiza mbegu kiitwacho Dar IVF and Fertilizing Clinic.

Mkurugenzi wa Tiba wa kituo hicho, Dk. Tamale Sali, alizungumzia pia uwezekano wa wazazi kupata watoto wa jinsia watakayo kwa kutumia teknolojia ya upandikizaji na kuleta matokeo sahihi ya asilimia 100.

“Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa hii njia ya kuchagua jinsia ya mtoto kwa mzunguko wa hedhi hutoa matokeo ya asilimia 50 kwa 50. Siyo ya uhakika sana kwa sababu wazazi wanaweza wanaweza kufanikiwa au wasifanikiwe.

Lakini ya upandikizaji maabara ina uhakika zaidi katika kupata mtoto wa jinsia wanayoitaka wazazi,” alisema Dk. Sali.

Akieleza zaidi, Dk. Sali alisema kinachoweza kufanyika kwa wale wanaotaka kuwa na watoto wa kiume au wa kike kadri watakavyo ni kuchukuliwa kwa mbegu za mwanaume, kupelekwa maabara na huko ndiko uamuzi kuhusu jinsia ya mtoto unaweza kutolewa na wahusika.

Aidha, Dk. Sali aliongeza kuwa mbali na uamuzi kuhusu jinsia ya mtoto, wazazi hupata fursa pia ya kupata mtoto asiyesumbuliwa na maradhi kama ya kisukari na moyo.
“Mbali ya kupimwa jinsia ya mtoto, mbegu ya baba hupimwa pia magonjwa mengine kama ya moyo na kisukari… kama itabainika kuwa mbegu ina tatizo, inaachwa na kuchukuliwa mbegu nyingine,” alisema.

Dk. Sali alisema kuwa hadi sasa, tangu waanze kutoa huduma zao nchini, tayari wameshasaidia wazazi tofauti 15 kupata watoto wa jinsia waitakayo kwa njia ya upandikizaji huku wastani wa watoto wanaozaliwa nchini Uganda kwa mwaka kupitia njia hiyo katika kliniki yao iliyopo nchini humo ni 30.

Alisema wanaopaswa kutumia njia ya upandikizaji katika kupata watoto ni wanawake ambao mirija yao ya uzazi imeziba, wale walio na utasa na baadhi ya wagojwa wenye uvimbe kwenye ‘ovari’, vivimbe vya vimeleo kuzunguka mfuko wa uzazi, wanawake waliomaliza hedhi na bado wanahitaji mchango wa mayai, waliotolewa mfuko wa uzazi lakini ovari zao zimebaki na sababu nyingine za kijamii ikiwamo mume kusafiri kwenda masomoni au vitani.

Alisema kwa kawaida, wao hutoa matibabu kwa njia ya upandikizaji pale tu inapowalazimu wanandoa kufanya hivyo ikiwa ni njia ya mwisho baada ya njia nyingine zote za kupata mtoto kugonga mwamba.

Msimamo wa Serikali kuhusu jinsia za watoto
Baadhi ya watu hutamani kuwa na mchanganyiko wa jinsia katika orodha ya watoto wao na hivyo huwa tayari kufuata njia mbalimbali ili kuwapata watoto wa jinsia waitakayo ili kukidhi matakwa yao.

Hata hivyo, Nipashe imebaini kuwa baadhi ya njia haziruhusiwi nchini ikiwamo ile ya kukatisha uhai wa mimba ya mtoto wa jinsia wasiyoitaka wazazi wakati wa kutungwa kwake.

Mkurugenzi wa Uhakiki wa Ubora wa Huduma katika Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed Mohamed, alisema ni kosa kisheria kwa mama kutoa mimba baada ya kujua jinsia ya mtoto anayetarajia kumzaa.

Kuhusu upandikizaji alisema sheria inatambua wale wenye matatizo ya uzazi, wenye umri mkubwa na ukomo wa hedhi kuwa hawakatazwi kupandikiza lakini siyo wanandoa wenye afya njema na uwezo wa kupata watoto kwa njia ya kawaida.
===
BAADHI YA MAONI NA USHAURI ULIOTOLEWA NA WANAJF

Wakuu habarini!!!

Leo nimeamua kukushirikisha katika mjadala huu kuhusu siku gani mtoto wa kiume anaweza tungwa kwa kufata njia ijulikanayo kama kalenda.

Siku zote mwanamke huwa na siku 28 katika mzunguko wake wa hedhi,hivyo basi siku zake huwa zimegawanyika katika makundi kundi.

Kundi namba moja ni siku za hedhi,ambazo uchukua siku tano kwa mwanamke asiekuwa na matatizo 1--------5 ila wengine huwa damu inakata kwa siku tatu na wengine mpaka siku saba ambayo kisayansi mwanamke anaefikisha siku saba huwa na mattizo katika mzunguko wake uenda hata mimba asipate.

2.kundi la pili uchukua siku 6--------10.kitaalamu ujulikana kama siku salaama sana,yaani mwanamke akitoka hedhi tu anaweza Fanya mapenzi bila kupata mimba.

Kundi la tatu ni siku hatari ambazo kwa kawaida ndo mimba utungwa.uchukua siku ya 11-------17 toka siku ya hedhi. hizi siku huwa ni hatari San katika mzunguko wa mwanamke hasa siku za tarehe 12,13,14,15 hizi siku ndo hatari na hapo ndo mtoto wa kiume utungwa.

Mtoto wa kiume utungwa hasa siku ya 13 au 14 kwani bengu zinazoingia kwenye mfumo wa uzazi kutoka kwa mwanaume ni begu mbili ya kwanza ni "x" ambayo huwa ni mbegu za kike na "y" amabazo huwa ni bengu za kiume

Mbegu za kiume ukimbia sana kuwai yai katika mfumo wa uzazi ikilikuta yai halipo katika mfumo wa mwanamke ukaa pale nje na kusubili kwa Massa 48 yaani siku mbili.

Lakini mbegu za kike uenda taratibu wakati wa kufata yai.hivyo basi ukaa kwa muda mwingi kulisubili yai yaan siku siku mbili na nusu hadi siku tatu.

NJINSI YA KUZA MTOTO WA KIUME?

Itaendelea soon!

Zingatia, Nitakuletea picha tumbo la kike na kiume yanavyokuwa wakati mimba ishatungwa.View attachment 1107954
---
Njia ya kupata Mtoto wa Kiume kutumia siku 24 na 28

¤ Siku zote mtoto wa kiume hupatikana siku Mwanamke ameingia Ovulation/yai limetoka na anahamu sana na Mwanaume kuliko siku zote.(Zile I Miss U zinapokuwa zinazidi)

Sasa Mwanamke unatakiwa umpe Tunda mwanaume siku hiyo ya kwanza. Kwa wanawake wenye mzunguko wa siku 24 ni siku ya 12 toka alipobleed na Kwa wanawake wa mzunguko wa siku 28 ni siku ya 14 toka alipoanza kubleed. Hizi ni siku za Yai kutoka.

ikumbukwe kuwa mbegu ya kiume Y inawahi kufika kuliko X ndo maana nakushauri hivyo. Na pia Y inawahi kufa kabla ya X. Y inaishi siku 2 mpaka 2.5 wakati X inaishi mpaka siku 3 na 3.5

kwahiyo kama ukifanya siku hiyo Mbegu ya kiume itawahi kufika na kurutubisha Yai mapema. Na kumbuka kuwa Ili kuwe na uwezekano mkubwa wa kufika lazima Mwanamke awe Chini na Mwanaume awe juu wakati wa tendo la Ndoa ili kuleta mseleleko mzuri wa mbegu.

Na siku zote Mwanaume apige magoli mengi ili kuleta sperm count kubwa zitakazoweza kufika kwenye Yai. Na Mwanamme ukae style ya Missionary kwa mda Mrefu wakati uume upo kwenye uke mwishoni kabisa ili kufikia karibu na Cervix.

Note: Mwanaume anatakiwa asimove uume wake wakati amefika kileleni na hakikisha ameuingiza wote.


Goodluck
---
Conceiving a Boy: Ovulation Timing
How to Conceive a Boy

During my research on "how to conceive a boy", I found out that ovulation timing is one of the factors you'll want to consider. It's not the most crucial factor, but hey, every little bit helps, right? What "ovulation timing" means with respect to baby gender selection is timing when you have intercourse in relation to ovulation.

So, the question is should you have intercourse close the time the egg is release or a few days after? If you're trying to conceive a son, try to have intercourse as close to ovulation as possible. The means as soon as you think your about to ovulate (You can usually tell a few days prior. See the tips below.), have intercourse. Then, at the latest, have it again when you're fairly certain the egg has been released.

Make Sure Those Sperm are There and Ready for Action
Really the easiest way to make sure the male Y sperm are present and active enough to do some go is to make love every day as soon is you know your ovulation time is near. Now, you may be thinking all that lovin' is going to lower dad-to-be's sperm count and result in no pregnancy at all. For some reason, this is a fairly prevalent myth, but fortunately it's only partly true. In reality, having intercourse every two or three days shouldn't cause any problems.

How can you Time Your Ovulation?
New to ovulation timing? Don't worry, you're not alone. Plenty of parents just let nature take it's course and never worried about timing Mom's ovulation cycle, so it's not a big deal if you don't know how yet.

The easiest ovulation predictor is the regularity of your cycle. Just mark your calendar one the day your period starts. If you're cycle is fairly regular, about 14 days from then, you should ovulate again. The 9th to the 15th days are when you want to have intercourse because those days are when you're most fertile. Remember, though, if you've recently stopped birth control it can take up to six months for your cycle to normalize again.

Taking your temperature will give you some indication because your body temp will fall a little (usually to around 97º F). Right before you ovulate. To conceive a boy, start getting busy when you notice that temperature drop. Your vaginal fluids can also be an ovulation predictor. Right before ovulation, you'll probably be a little dry and the have relatively clear, smooth discharge during ovulation. Other times, any discharge will be rather sticky and yellowish.
---
Naomba kuongeza hapo.

Mbezu za kiume zinazoweza kutoa mtoto wa kiume huweza kukaa muda wa masaa 48. Na zinazoweza kutoa mtoto wa kike hukaa masaa 72. Kwa hiyo toka siku ya 11 mpaka siku ya 14 yai linapokuwa released ni masaa 72.KWA HIYO BASI, kama wataka mtoto wa kike wapaswa kufanya tendo la ndoa siku ya 11 au 12 maana mbegu za kutoa mtoto wa kiume zinakuwa zimeishiwa nguvu kabisa ifikapo siku ya 14 na za kike zitakuwa bado zinadunda.

Ila kwa siku ya 13,14 yenyewe ukifanya tendo la ndoa mara nyingi posibility ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa maana speed ya mbegu zitoazo mtoto wa kiume ni kubwa kuliko zitoazo mtoto wa kike. Na itakuwa ni ndani ya masaa 48 .
---
Ni kweli kuhusu spidi ya mbegu lakini tendo siku ya 14 kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 lina uwezekano mkubwa wa kutoa msichana. Siku ya 14 ni siku ambayo yai utoka katika ovari (yaani ovulation) kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28. Yai linachukuwa siku kadhaa kutoka katika ovari kufika kwenye fallopian tubes ambako huonana na mbegu na kutunga mtoto. Y kama ulivyosema ni "sprinter" aina ya Usain Bolt.

Hukimbia haraka na kuchoka haraka. Ikiwekwa ndani ya mwanamke siku ya 14 itakufa kabla ya yai kufika katika fallopian tube. X ambayo inakwenda taratibu lakini ni "marathon runner", itakuta Y alikwishakufa na itafanya kazi yake ya kurutubisha na kutoa msichana. Ukisubiri tendo mpaka mwisho wa ovulation - pengine siku ya 16 ama 17 ya mzunguko, yai litakuwa katika fallopian tube tayari, Y atakimbia haraka kama kawaida yake na kulikuta yai katika sehemu ya kurutubishwa tayari na kutunga mimba ya mvulana kabla X hajafika.

Ukiwa na OVULATION KIT (ambazo zinauzwa pharmacy) inasaidia sana. Unapima hormone za ovulation katika mkojo. Unaona ovulation inapooanza na ukiendelea kupima utaona inavyokwisha. Ovulation kit inasaidia sana hasa kwa akina mama ambao mzunguko wa siku zao hubadilika badilika.

Mwisho wa siku Mungu ndiye mtoaji.

Omusolopogasi (Gynaecologist)
===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII:
- Mjadala: Je, ni siku zipi ambazo mwanamke huweza kupata ujauzito katika mzunguko wake wa kila mwezi? - JamiiForums
 
Jamani pole... Usiwe na stress sana especially ukiwa unataka kuonana na baba kwenye mambo yetu yale! Af maswala ya mtoto mshirikishe Mungu na pia usali sana mama kwa sababu Mungu wetu ni mwaminifu... Mshkuru sana Mungu kwa hao wawili aliokupa na hongera sana coz wapo wanaotafuta hata kushika mimba tuu na hawafanikiwi hivyo usivunjike moyo hata kidogo.

Ila pia baba mtoto anatakiwa kubadili mtazamo wake kuhusu watoto... Mtoto ni mtoto jamani inategemea tu na utakavomlea. Kuna familia nyingine zna watoto wa kiume ila unakuta wa kike wanaout shine hata wale wa kiume hivyo ni swala la mtazamo tu.. Hata hivyo tuwasubiri wataalamu wa hayo mambo nna uhakika watakusaidia zaidi.
 
pole sana,kwa ushauri tu,kama unataka mtoto wa kiume,chukua vijiko vitatu vya chakula vya sodium carbonate,changaya na liter moja na nusu ya maji,tumia mchanganyo huo kujisafisha sehemu za faragha kabla ya kukutana na mzee,kitu kitajibu
Naomba msaada wenu,nimeolewa na nina watoto 2 wa kike.nifanyeje ili nipate mtoto wa kiume mana mme wangu anapenda sana watoto wa kiume hivyo ananikosesha raha.
 
Mtoto wa kike: Hesabu siku tatu za mwanzo yaani siku ya 11,12 na 13 baada ya Mp na
mtoto wa kiume: hesabu siku tatu za mwisho yaani siku ya 14,15 na 16 au 17 baada ya M
p.

ILA bado itasubiriwa mwanaume atatupia nini, coz mwanamke huwa ni XX wakati mwanaume huwa XY sasa hapo mwanaume akitupia Y basi unapata jaribu hiyo, kuna mtu wa mzunguko wa siku 28 alitumia mbinu hii na akapata kama alivyotaka, ikiwaje ni PM nkueleweshe kwa undani.
 
Mtoto wa kike: Hesabu siku tatu za mwanzo yaani siku ya 11,12 na 13 baada ya Mp na
mtoto wa kiume: hesabu siku tatu za mwisho yaani siku ya 14,15 na 16 au 17 baada ya M
p.

ILA bado itasubiriwa mwanaume atatupia nini, coz mwanamke huwa ni XX wakati mwanaume huwa XY sasa hapo mwanaume akitupia Y basi unapata jaribu hiyo, kuna mtu wa mzunguko wa siku 28 alitumia mbinu hii na akapata kama alivyotaka, ikiwaje ni PM nkueleweshe kwa undani.

Kama sikosei mwanaume ndio ana determine jinsia ya mtoto na kuna ambao wapo wachache huwa wanatoa jinsia moja tu hata azae na wanawake kumi (hapa wataalamu watanisahihisha maana nilisoma biology ya kujibia mtihani tu hivyo naweza nikawa sipo sahihi kabisa)
 
Tell him to stop that patriarchy behavior kabla Mungu haja chukua uamuzi juu ya hiyo
tabia yake na mwambie akumbuke kuwa kuna wanao muomba MUNGU awape hata wa kike
ambao yeye anawaona sio kipaumbele.
 
Jamani shida ya Christa si tatizo la mmewake na wala hajaomba ushauri juu ya mmewake kutaka mtoto wa kiume na inawezekana mme wake hayuko siriasi kiivyo katika kutaka huyo mtoto wa kiume isipokuwa ni yy Christa ili kufanya mamboresho kaomba ushauri ili kama inawezekana apate mtoto wa kiume na ndo maana kauliza jinsi ya kutaka mtoto wa kiume! tujaribu kuelewa muhitaji anataka msaada gani/upi!
 
baking powder ile ni sodium carbonate,unajua majimaji ya ukeni yana acid ambayo ni weak,sasa sodium carbonate ni weak base,ambayo inaanfanya neutralization proces na kufanya yale majimaji kuwa hayana acid,mbegu za kiume huweza survive katka hali hiyo,za kike haziwezi kusurvive
chakula cha sodium carbonate ni kip?/kinapatikana wap?
 
Ni rahisi sana subiri siku ya tatu baada ya breed kuanza utaona utando mweupe na mzito sasa hapo unaweza kumpa mimba mkeo I mean kukojoa shahawa zako na mimba ya mtoto wa kiume itapatikana.

=================================================
Naomba kuongeza hapo.

Mbegu za kiume zinazoweza kutoa mtoto wa kiume huweza kukaa muda wa masaa 48.na zinazoweza kutoa mtoto wa kike hukaa masaa 72. Kwa hiyo toka siku ya 11 mpaka siku ya 14 yai linapokuwa released ni masaa 72.KWA HIYO BASI, kama wataka mtoto wa kike wapaswa kufanya tendo la ndoa siku ya 11 au 12 maana mbegu za kutoa mtoto wa kiume zinakuwa zimeishiwa nguvu kabisa ifikapo siku ya 14 na za kike zitakuwa bado zinadunda.

Ila kwa siku ya 13,14 yenyewe ukifanya tendo la ndoa mara nyingi posibility ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa maana speed ya mbegu zitoazo mtoto wa kiume ni kubwa kuliko zitoazo mtoto wa kike. Na itakuwa ni ndani ya masaa 48 .
 
basi hedhi niliipata hii mwaka jana nikajaribu kwa baadhi ya watu kama kumi wakafanya na wake zao na mimi nikafanya kwaka jana nikafanikiwa kupata motot wa kiume
 
Back
Top Bottom