Jinsi ya kupata GPA kali, kuepuka supplementary na jinsi ya kutodisco chuoni.

Hongera sana kaka.
Nakutakia kila la kheri, I will say a prayer for you in a few minutes to come. Mungu akusimamie ndoto zako. Ushauri uliopewa umetosha. Usisahau ulikotoka, zingatia kila mtu ametoka kwao ana anajua kaandaliwa nini. Usiige tembo kunya, utapasuka msamba.
 
Ndugu zangu wote waliopata mkopo na wale waliokosa kwanza kabisa nipende kwa pamoja sote tumshukuru Mwenyezi Mungu kwani ana mipango na sisi wanadamu aijalishi umepata mkopo au la. Basi ndugu zangu bila kuwachosha nilete yangu yalo moyoni na atakayeweza kunipa mawazo, maoni na msaada mwingine naomba atupie hapa. Mimi ni kijana niliyezaliwa katika kijiji kidogo nikiwa mtoto wa 17 kati ya watoto 30 wa baba yangu nikimaanisha kuwa kuna wakubwa zangu wasio na uwezo mzuri kiuchumi 16 na wadogo zangu ambao pengine wananitegemea 12. Kutokana na hali hiyo ya familia niliamua kukimbilia kutafuta elimu ambayo itakuwa ni mkombozi kwangu na hata familia na jamii kwa ujumla. Basi kwa neema ya Mungu nilifanikiwa kufaulu kidato cha nne kwa kupata dalaja la kwanza (16 ) na baadae kujiunga kidato cha tano na cha sita nikafaulu kwa dalaja la kwanza (9) basi kama ilivyo furaha ya wengi hata mimi mwenzenu mimefanikiwa kuchaguliwa Bachelor of science in nursing university of Dodoma na kupata mkopo 4,032,500/= lakini baada ya kusikia kuwa mtu anapopata GPA kali mfano 5 inakuwa ni lahisi kutoka kielimu na pengine kubakizwa chuoni kuwa assistance lecturer nimekuja kwenu wa jf na great thinkers muweze kunipa/kutupa mawazo au ushauri sisi sote ili kuepukana na supplementary, kuto disco na hatimae kupata GPA kali hili kuweza kukomboa familia kama yangu na zaidi kupata elimu ambayo itakuwa ya manufaa kwa jamii na wala si elimu ya kukariri ukizingatiwa nitadili na afya ya binadamu. ASANTE KWA KUNISIKILIZA , NAKARIBISHA MAWAZO/ Ushauri WENU.

Obviously GPA ya 5 hutapata, kulingana na historia yako...lakini komaa, piga msuli kama wa form six, tafuta discussion groups za watu wenye akili timamu..epuka vitu kama hivyo hapo kwenye red, hudhuria vipindi vyote na ukae mbele..zaidi sana mtangulize Mungu,,atakutuliza akili
 
Kihalali:
Fanya assignents vizuri.
Usipitwe na quiz hata yenye max1,uwe unajizoeza kusoma kwa uelewa lecturer anapofundisha somo fulani. Uwe unapunguza mzigo wa notes ambazo hazijasomwa ,kwa kupitia kidogo kidogo na siyo 'fayatingisha' karibu na mtihani. Kikubwa ni uelewa..na kupangilia muda wako na ratiba yako vizuri. Na yote yanawezekana ukimtanguliza mbele 'MUNGU MWAMINIFU',kwa Kila jambo,katika Masomo na Maisha yako.

zamani kule o level nilikuwa nikidharau marks au masomo fulani ila kaka umenikumbusha Mungu anisaidie sitakosa hata kwenye 1+[_]=2
 
Rule 1: Go do what you are supposed to do, not what you want to do.
Rule 2: Rule 1 shall always prevail, mutatis mutandis!

Ahsante, masomo mema.

asante kaka ila hiyo mutandis sijailewa.
 
Rule 1: Go do what you are supposed to do, not what you want to do.
Rule 2: Rule 1 shall always prevail, mutatis mutandis!

Ahsante, masomo mema.

Nimeipenda hii....hiyo mutatis mutandis bila shaka ni kama cetiris paribus
 
Mtegemee MUNGU wa KWELI katika kila jambo,
Kumbuka kuomba/kusali siku zoteza maisha yako,
Fuata kwa usahihi ratiba zote za chuo,
Achana na maisha ya UJANA na ambayo hukuyazoea i.e USHARO
Hakikisha kila course work,quiz,test na exams unafaulu kwa kiwango cha JUU,
Then, mshukuru MUNGU kwa kila jambo.
Hapo utafanikiwa
 
Nami Nimejifunza kitu kupitia thread hii....sasa kazi ni kwangu tu...stay blessed jf members
 
Nami nawashukuru wote mliotoa ushauri kwani nami pia nimepata muongozo fulani. Asanteni
 
kaka asante sana iyo tutorial ndo nimechanganya na assistance ki ukweli ushauri wako mzuri sana ingewezekana ningeprint page lakini naomba unisaidia hapo namba 5. Kuhusu boo control maana huku nyumbani familia nzima wanafanya sherehe wakisema boom likiwa linaingia natuma hata laki 250 kwa ajili ya wadogo zangu huku wakisisitiza kuwa health related fields zote huwa wanaongezewa hata motisha je kwa wale wazoefu inawezekana nikajibana vip ili niweze kusatisfy pande zote nyumbani na mi mwenyewe.

Be carefully kwanza tambua sio kwamba utakuwa unapata hiyo millioni nne mkononi kabisa. Ninachofahamu ni kuwa,hapo bodi ya mikopo wameweka na ada. Hivyo basi wewe urakuwa unapokea kiasi cha pesa ambacho ni kwa ajili ya chakula,malazi na stationary. Na kwa sasa ni shs laki tisa kwa semester. Sasa basi utakapopata hiyo pesa hakikisha unatenga kwa ajili ya chakula na kulipia malazi. Kwa sababu vitu vikubwa muhimu sana chuoni ni kupata chakula na kuweza kulipia pa kulala. Alafu hakuna ukweli kuwa ukipata GPA kubwa unaweza ukabakishwa chuo,kwa sasa kama unataka kuwa Lecturer unaomba ajira kama mtu mwingine yeyote. Siri ya kufanikiwa ni kusoma.
 
kufaulu vyuo inabidi ufuate huu mwongozo-pray hard,study hard,work hard then kufaulu kwako ni guarantee.
 
1. Ukifika chuo chakwanza tafuta kadi ya CCM...
2. Soma tu kile unachofundishwa, usijidai kichwa uanze kutafuta sources nyingine za materials. Hata kama mawalimu
anatumia slides, komaa na hizo hizo.
3.Solve as many past paperz as possible cuz walimu wengi wa chuo ni wavivu kutunga maswali mapya
 
Nimeipenda hii....hiyo mutatis mutandis bila shaka ni kama cetiris paribus

Mutatis mutandis si sawa na ceterius paribus ,ila ungesema ni terms ambazo zipo ktk field moja ya economics,ceterius par-means other things being constant/same,while mutatis mutandis-imply that ,certain thing happen because of appearance of certain situatim.hiyo ni maana rahisi ili kumwezesha layman aelewe maana ya hz terms.
 
Cha muhimu chuo demu wa professor muogope kama ukoma .. hilo tu ndio nyongeza yangu kwako
 
Obviously GPA ya 5 hutapata, kulingana na historia yako...lakini komaa, piga msuli kama wa form six, tafuta discussion groups za watu wenye akili timamu..epuka vitu kama hivyo hapo kwenye red, hudhuria vipindi vyote na ukae mbele..zaidi sana mtangulize Mungu,,atakutuliza akili

thank you for your prayer lakini GPA hiyo sio lazima iwe 5 hata ikipungua point kidogo lakini kilicho cha muhimu ni kutoka kikamilifu ktk hayo masomo ya chuo.
 
nimepata kitu...hongera kwa mleta mada..hongera kwa wachangiaji...jf forever...
 
zamani kule o level nilikuwa nikidharau marks au masomo fulani ila kaka umenikumbusha Mungu anisaidie sitakosa hata kwenye 1+[_]=2

Asante Kiny, Me i'l b prayn 4u na wote wanaoanza maisha ya Chuo, Mungu atawaongoza tu, Trust him.
 
Back
Top Bottom