Jinsi ya kuongoza ndoto za usiku utakavyo (Lucid Dreams)

mkuu kipindi nipo chuo nilishawah kuota nasoma notes zilikuwa kwenye slides,nilikuwa nina mpango wa kuamka kusoma ila nilijikuta nimechelewa kuamka but kila nilichosoma kwenye ndoto kilikuwepo kwenye slides,nilipoenda kwenye test nlikuwa nakumbuka mpaka page ambayo inajibu swali,je hiyo ni lucid dream mbona haijawah kunitokea tena?
 
Kuna ndoto
Haijalisha unaota ndoto gani, unaposema ndoto ni kwamba haujitambui.

Maono
Ni hari ya kua unajitambua na kuweza kuona katika ulimwengu wa roho wa vitu vilivyopo, vilivyo pita ama vijavyo

Kuahamishwa kiroho
Pale unaweza ukawa unamuona mtu kiroho kila kitu anacho kifanya mahala popote alipo

2 Wafalme 5 : 20

20 Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake.
21 Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani?
22 Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.
23 Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake.
24 Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.
25 Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali.
26 Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi?
27 Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.

Hiyo 2 wafalme 5: 20-27 inahusiana vipi na mada?

Daniel 7 : 1

1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danielii aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.

Hayo mengine ni kuwapoteza watu na kuwachanganya

Na kwa mujibu wa aya hiyo. kilichopotezwa nini kwa kuzingatia mada?

Hembu funguka.
 
mkuu kipindi nipo chuo nilishawah kuota nasoma notes zilikuwa kwenye slides,nilikuwa nina mpango wa kuamka kusoma ila nilijikuta nimechelewa kuamka but kila nilichosoma kwenye ndoto kilikuwepo kwenye slides,nilipoenda kwenye test nlikuwa nakumbuka mpaka page ambayo inajibu swali,je hiyo ni lucid dream mbona haijawah kunitokea tena?

Hiyo Sio Lucid Hiyo Ni Astral Projection..

"Rakims"
 
Jinamizi? kwanini halikuuwi? hiyo ni mind yako ukilala chali huja jinamini je ni kweli? ukijikunja koo kidogo unahisi unakabwa je ikiwa umejikunja na upo usingizini nini kinatokea jibu ni NDOTO A.K.A Jinamizi...

mungu kaumba kiumbe cha kukuniga usiku?? nonsense

"Rakims"

mmmm mwalimu mkali...
 
Sasa hapa inasaidia nini kuota tu, Umeota unamajumba makubwa, umeyapata sasa?. Umeota umetembea na Joketi, je umempata kweri? Kama ni kuota tu na hupati kitu katika ukweri ya nini kujihangaisha?
 
Mkuu Rakims mi nina miaka 9 sasa sijawahi kuota je? Nifanye nini ili nianze kupata ndoto.
 
Sasa hapa inasaidia nini kuota tu, Umeota unamajumba makubwa, umeyapata sasa?. Umeota umetembea na Joketi, je umempata kweri? Kama ni kuota tu na hupati kitu katika ukweri ya nini kujihangaisha?

Swali Zuri Sana...!

Ni Kwamba Ndoto Inasaidia Kukamilisha Mambo Yako Ya Ulimwengu Wa Kweli Kwa Asilimia Nyingi... Mfano Leo Umelala Umeota Unaendesha Gari Na Ni Gari Kweli Kweli Kila Kitu KEY,KRACH,BUTTON,USKANI,EKSLETA,BRAKE,HANDBRAKE Kila Kitu Sawa?

Hujawahi Kuendesha Gari Hata Siku Moja Mfano....

humo ndotoni ukaita mtu akakufundisha kila kitu Ukajua Ile Kumbukumbu Ukabaki Nayo Ukaamka Ukaenda Kujaribu Kama Maelekezo Ndotoni Yalivyokwenda Kila Unachofanya ndivyo kinavyokuja Je Ni Faida Au Hasara??? au hamna lolote uongo tu nilikuwa nimeona mtu anaendesha? ndio utakavyojijibu?

faida za kweli kuu za mwanzo ni kujiponya ubongo na kujifunza

"Rakims"
 
ushetani mtupu

Kweli kabisa yani upo sawa hujakosea hata robo maana consiciousness yalo inasoma hivyo?

lakini nikuulize swali?

"kukataa kuhusu hili ni sawa na mtu kukataa kuwaza au kufikiria, hapo ni sawa na kusema nawaza hapa nakumbuka ticher aliwahi kunisema vibaya haya ndio mawazo yako ya kila siku..

lets say leo umefikia ile kumbukumbu kila siku inakunyima raha hivi ukianza kuirudia hapo ilipoishia ukaamuru ubongo wako ufanye muendelezo kwa baada ya kunisema vibaya nikamuahidi nitajirekebisha nikajirekebisha baadae akaja kuniomba samahani kwamba hata siku ile yeye hakuwa vizuri mambo yakaisha.....

je hiyo ni ushetani au ni kusafisha ubongo na kujiondolea kukata tamaa?

endelea kuamini ushetani kama wewe kila ukiota unafanya mapenzi ni kubakana na mashetani halafu huna mke wala gf au bf wa kumaliza haja zako ukiota hivyo unaambiwa ushetani unakubali tu kwa ajili ya imani huko ni kupinga imani yako bila kujijua kwa maana zisipotoka zile mbegu zitatokea wapi? kama sio kitandani na ndotoni? labda ukafanya masterbertion bafuni....

"Rakims"
 
Jamii forum inamambo mm juzi nimeota nimepiga deal kuna mtu alinambia nimpelekee mtu daftari kwabahati nzuti huyo mtu nilietumwa nimpe buku nikamkuta yupo ktk mazishi ya kumzika mtu watu kibao mtu mwenyewe kavaa nguo nyeupe km za askari nikampa hilo daftari nikirudi nilipotumwa napata mijihelaa ya maana ila nataka nimpe mtu nikaapata ishara ya kwamba usimpe hilo daftati ghafla nikaamka. Aisee ndoto zengine ikawa mwendo wakucheka siku nzima jinsi nilivoota. Iyo sasa afadhali week iliyopita niliota naenda safari na sindikizwa km rais a.k.a president full polisi. Izo zote trela wakati mwengine naota ndoto ni mfano wa movie yaani ndoto endelevuu yaani ni shydaa
 
utajifunza mengi ukianza kuziongoza.

"Rakims"
 
Waweza Pia Kutengeneza Hadithi Ya Kusisimua Kupitia Lucid Dreams
 
Attachments

  • 1427121822204.jpg
    1427121822204.jpg
    19.2 KB · Views: 305

Similar Discussions

Back
Top Bottom