Jinsi ya kuijua asali orginal

Simba Mkali

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
620
239

TUNAFAHAMU kwamba asali ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binaadamu, lakini watu wengi wamekuwa wakipigwa kwa kuuziwa asali feki, sasa leo nimeona niwape darasa wanunuzi wa asali ili wasiweze kununua asali feki.
Maana sehemu nyingi hasa Kariakoo, wafanyabiashara wamekuwa wakiuza asali ambayo haina ubora kwa kuchanganya maji na sukari guru.
Njia ya kwanza, chukua njiti ya kibiriti kisha ichovye sehemu yenye baruti kwenye asali unayotaka kuinunua, kisha iwashe njiti hiyo kwa kutumia kibiriti chako, ikiwaka, ujue hiyo ni asali kweli.
Njia ya pili, dondosha asali chini katika mchanga, ukiona sehemu ya mchanga iliyolowana ikijikusanya pamoja ujue hiyo nii asali orginal.
Njia ya tatu, Chukua karatasi jeupe, dondoshea asali njia juu yake, kama ikichelewa kutokea upande wa pili, ujue hiyo asali safi na inafaaa kwa matumizi ya binaadamu.
Bado kun njia nyingine ambayo hutumiwa na baadhi ya watu, kama vile kuimwaga katika kiganja cha mkono wako, ukiona tone la mwisho linabakia kwenye chupa kuja mkononi, hiyo ni asali, pia wengine huangalia kama ikiwa kwenye chupa huwa inatengeneza alama yenye mfano wa korosho. Nadhani hutaibiwa tena kwa kuuzia asali feki.
 
Asante kwa somo zuri, japokua kwenye kui test ndio mtihani, muuzaji hawezi kukubali kirahisi, hasa akishajua asali yake ni ya magumashi.
 
Somo zuri,ila sasa itabidi tu ukubali hasara kwa afya yako,baada ya kuinunua ndipo utest,na kama matokeo ni mazuri endelea nayo,na matokeo yakiwa mabaya usitumie!
 
Fafanua vizuri ikiwa nani ya chupa. Je kuna asali mbichi na iliyo iva?
 
Wa TZ bwana! kila kitu mnakuwa negative.
Mtu kajitolea kutoa elimu ya muhimu bure, mnaleta ukauz u.

Haya, ukiona ni sealed kafanyie uchunguzi nyumbani kwako then ukikuta feki ndio urudishe na vigezo ulivyoelekezwa.

Need we say more ?
kaka si wabongo tuna matatizo sana kila kitu kujifanya tunakosoa badala ya kushukuru..watu wanaojifanya wajuaji wananiuzi sana
 
Au chukua asali kidogo jipake halafu katiza mahala penye nyuki,ukiona khawakufati hiyo feki

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
"Asiyejua maana haambiwi maana"

hahahaaaaa,Hakyanani hii ndo JF. Hata siku yako ikiwa mbaya utafurahi tu.Asante mkuu kwa kuniongezea siku za kuishi.
 
TUNAFAHAMU kwamba asali ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binaadamu, lakini watu wengi wamekuwa wakipigwa kwa kuuziwa asali feki, sasa leo nimeona niwape darasa wanunuzi wa asali ili wasiweze kununua asali feki.
Maana sehemu nyingi hasa Kariakoo, wafanyabiashara wamekuwa wakiuza asali ambayo haina ubora kwa kuchanganya maji na sukari guru.
Njia ya kwanza, chukua njiti ya kibiriti kisha ichovye sehemu yenye baruti kwenye asali unayotaka kuinunua, kisha iwashe njiti hiyo kwa kutumia kibiriti chako, ikiwaka, ujue hiyo ni asali kweli.
Njia ya pili, dondosha asali chini katika mchanga, ukiona sehemu ya mchanga iliyolowana ikijikusanya pamoja ujue hiyo nii asali orginal.
Njia ya tatu, Chukua karatasi jeupe, dondoshea asali njia juu yake, kama ikichelewa kutokea upande wa pili, ujue hiyo asali safi na inafaaa kwa matumizi ya binaadamu.
Bado kun njia nyingine ambayo hutumiwa na baadhi ya watu, kama vile kuimwaga katika kiganja cha mkono wako, ukiona tone la mwisho linabakia kwenye chupa kuja mkononi, hiyo ni asali, pia wengine huangalia kama ikiwa kwenye chupa huwa inatengeneza alama yenye mfano wa korosho. Nadhani hutaibiwa tena kwa kuuzia asali feki.

Asante ndugu kwa elimu, Kwa mwenye kufahamu hili pia atufahamishe tafadhali, asali za nyuki wakali hutofautiana? kuna zinazoganda na kuna zisizoganda hapa shida huwa ni kitugani haswa?
 
Back
Top Bottom