Jinsi ya kuachana na mwanamke bila ugomvi

Msenyele

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
338
86
Ni miaka mitatu tangu nianze na mahusiano ya mapenzi na mdada mmoja. Naye, tulikuwa na mahusiano ambayo lengo halikuwa kuoana. Lakini kinachonishangaza ananing'ang'ania kiasi kwamba nashindwa hata kupumua. Hata hivyo katika mahusiano yetu tumebahatika kupata mtoto wa kiume nje ya ndoa. Kimsingi nilikuwa sikujiandaa kuoa na bado nasoma na natamani kuendelea kusoma masomo ya juu mwaka huu. Kilichoharibika zaidi ni pale alipofahamu getoni kwangu kupitia kwa marafiki zangu, ndipo siku moja akatinga na begi la nguo kuja kuishi. Mtoto kwa sasa anakaribia miaka miwili na anaishi kwa mama mkwe. Huwa natoa matumizi madogo madogo kwa mtoto ili hali akiwa kwa bibi yake. Ujio wa mwanamke huyu ulinishitua sana na niliwaza sana na pengine hata alisababisha kuvuruga hali ya kiutendaji wa kazi nilizokuwa nafanya. Kwa kuwa nilihisi pengine nikimfukuza anaweza kuniharibia kazi hata kwa bosi wangu. Nilipiga moyo konde na nikakubali kukaa naye ili niendelee kukusanya vijisenti ambavyo vitaweza kunisaidia katika masomo yangu nitakapokuwa masomoni. Nataraji kujiunga na chuo kikuu mwaka huu.
Sababu zinazonifanya nimwache huyu binti ni kama ifuatavyo:-
1. Ni mtu jeuri na mwenye kiburi kuanzia kwangu, kwa jamaa na marafiki wakiwemo hata ndugu zangu.
2. Alishanitamukia ataniua mbele ya mwenyekiti wa mtaa.
3. Elimu yake ni ndogo na hivyo huwa anajihisi ninavyomtendea sivyo.
4. Hanidhamini kama mme wake japokuwa sijaafiki kuwa mke wangu.
5. Huwa anataka kupigana pale ambapo makosa yamefanyika.
6. Hapendi na hataki kurekebishwa kwa kile ambacho anaamini ni kweli.
7. Alishamtukana mama yangu matusi ya nguoni kwangu yalishanizoea mwishoe.
8. Hapendi kukaa na ndugu wa pande zote mbili na hii huwa inadhihirika pale anapokuwa amesafiri wageni kwangu huwa hawakatiki na wengine huwa wanadiriki kuuliza mkeo yupo na ukisema yupo hawaji.
9. Ugomvi wake huwa anachukua vitu vikali kama vile visu ama stoo au chupa za soda.
10. Anapenda maisha ya juu sana na uwezo huo sina.

MY TAKE:
Kuna uwezekano wa mimi kuuawa eidha kwa dawa ama kwa kitu kingine kikali ama kizito. Na ninavyoandika huu ujumbe nina majeraha shingoni ya makucha yake na kwenye mkono nina jeraha la meno na mkono sasa umekufa ganzi.
Sasa wanajf na nyie majumbani kwenu pako hivyo? Na kama pako hivyo huwa mnakabilianaje na hiyo hali kwa kuwa sioni wanaume wengine wanatembea na makovu? Na kama hapako hivyo nifanyeje ili nitoke kwenye dimbwi hili la utumwa?
NAOMBENI USHAURI WANAJF.
 
piga chini mwandikie maneno machache tu kama haya..

"From today onward take your time don't dare to call me, don't even reply my sms"
 
Ilikuwaje mpaka ukazaa nae? Haya matatizo yameanza/umeyafahamu kuanzia lini hasa? Unasema tangu mwanzo ulikuwa huna nia ya kumwoa, je suala hili uliliweka wazi kwake? Nini yalikuwa makubaliano yenu?
 
Pole ndg,ila inakuwaje mahusiano miaka mitatu umem-hold mtu na hunafuture naye...ina maana hizo hisia za kutaka kuolewa na wewe mpaka kujileta nyumbani zimemtokeaje? nadhani mtakua na mambo ya kuweka sawa maana haiwezekani muda wote huo mliokuwa pamoja hukuchukua maamuzi yoyote mpaka leo ndio uorodheshe mapungufu yake...i think you need sometime alone to think about it..chukua likizo nenda hata hotelini kakae mwenyewe au kwa bibi yako kama yuko mbali kijijini ..this happen sometimes in relationship....but it wont last forever blv me
 
hee,huyo ni muuaji.maybe ana stress za kutovalishwa pete.kazania masomo yako ili baadae uweze kumhudumia vizuri mtoto wako.na huyo hafai hata kuwa mke.ikiwezekana tafuta sehemu nyengine ya kuishi,na huo dada achana nae kabisa.ila huyo mtoto chonde chonde,hakikisha unamjali kama baba.sio baba jina tu,na next time wrap kikojoleo,ili kuepukana na mimba,unless uwe umepanga kuzaa tena.
 
huyo si mke mwema, achana naye ikiwezekana mkimbie muachie chumba kaa mbali naye ila mwanao usimuachie, ukifanikiwa kwa hilo kuwa makini kutafuta mke mwingine
 
Ilikuwaje mpaka ukazaa nae? Haya matatizo yameanza/umeyafahamu kuanzia lini hasa? Unasema tangu mwanzo ulikuwa huna nia ya kumwoa, je suala hili uliliweka wazi kwake? Nini yalikuwa makubaliano yenu?

naogezea,,,una uhakika gan kama huyo ni mwanao??????
 
mkuu anzisha mji mwingine, hapo muache akae mwenyewe atashika adabu!kwa sasa hajajua maisha ni nini

Umenena kiongozi, mwanamke mkorofi ni kumkimbia tu, aanze kugongwa na mabwana mchanganyiko, awafanyie vurugu wamdunde kisha wasepe! Siku 2 / 3 utamkuta ameshikilia opena baa jirani anafungua vizibo.

Nasisitiza: piga chini amia airtel!
 
Back
Top Bottom