Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,853
Kuna hadithi moja naikumbuka. Inasema hivi: kwamba Mzee Tata ( maarufu kwa magari ya Tata,machimbo n.k) alienda siku moja kwenye hoteli moja mashuhuri pale Bombay ( siku hizi Mumbai)wakati wa ukoloni wa mwingereza. Alipofika akaambiwa hawezi kupitia mlango wa waheshimiwa, aende akapitie mlango wa nyuma ambao watu kama yeye ndiko wanakopitia. Yule muungwana hakufanya hivyo, bali alijenga hoteli nzuri mara dufu ya ile ambamo watu wote walipitia mlango mkubwa. Sasa sijui ukweli wa hadithi hii lakini fundisho ni kwamba; kama hawa mabwana wanatudengulia, tujenge za kwetu ambapo hakuna mtu atatudharua. Tuko zaidi ya asilimia 90 ya nchi lakini kwa nini tunaruhusu kuendelea kudhalilishwa? Wenyewe tukijenga tunaweka bei hizo hizo za ajabu ambazo ukweli wenzetu wengi hawawezi kuzimudu. Dawa si kuwanyang'anya hizo nyumba zao. Dawa ni sisi wenyewe kuinvest katika sector hii na kujaza nyumba zenye bei inayoeleweka halafu tuone kama kuna mpuuzi atakayemdengulia mteja! Haya shimeshime ndugu zangu mliokuwa nje, mie niko tayari kuwapangia matofali!