Jinsi nilivyoteswa na mama mkwe, alichoma vyeti vyangu vyote

Asante kwa ufafanuzi.
sasa huyu bwana mdogo tumshauri namna bora ya kutumia hizo hela, asije ajkajikuta anahonga zote kwa mashingingi wa magomeni, maana anaonekana bado ni mpweke na nafsi yake inahitaji tulizo na liwazo la kiuhakika.

Kwani mkuu vyeti kuchanwa na mama mkwe ni kwamba huwezi kupata vingine, Nenda karipoti polisi kuwa vyeti vyako vimechanwa na utapata barua kutoka polisi ambayo utaenda nayo kuanzia shule yako ya msingi then nenda baraza la Mtihani na Chuo ulichosoma ambapo watakutolea Certified Copies za vyeti vyako vyote.

Na utakakoomba kazi kokote unaambatanisha na ile barua ya polisi kuwa uliwahi kureport polisi juu ya uharibifu wa vyeti vyako na ndo maana una Cerified Copy. Mbona wengi wanapoteza vyeti au kuungua kwa moto au kuibiwa ila wanapata kazi

Inaonekana kuchanwa kwa vyeti vyako ndo umeona mwisho wa maisha yako, kuhusu biashara ngoja waje wataalam kukupa ushauri
Rock issue ya vyeti ni sensitive tusilete utani na vyeti hawezi pata cheti nje ya document za kumusadia alihitimu elimu gani na mwaka gani. jamani tujaribuni kufikiria zaid jinsi ya kumsaidia

Ebu jaribu kua serious kidogo we umesoma mpka university then unashindwa kujua ukipoteza vyeti utafanya nini ili uweze kutambulika kwa proffesional yako, haya bwana.

Ebu jaribu kua serious kidogo we umesoma mpka university then unashindwa kujua ukipoteza vyeti utafanya nini ili uweze kutambulika kwa proffesional yako, haya bwana.

Baraza la mitihani hawatoi tena vyeti. UDSM nimeripoti toka jumatatu, napigwa tu danadana hawaongei jambo lolote la kueleweka.

Baada ya kusimamishwa kazi mambo mengi yalikwama kiasi cha kutimuliwa kwenye nyumba nliyokuwa naishi anga za Sinza.
Mama mkwe alinibembeleza sana nikakae nyumbani kwake Tegeta ambako ana nyumba kubwa na anaishi peke yake.

Nilienda ili nikae kwa wiki moja then niondoke ili nirudi kijijini kwetu Nassa Jeneri ili nikauze ng'ombe na nije kuanza maisha upya.
Siku ya tatu ya ukaaji wangu ukweni nikiwa busy na JF mara sms ikaingia. Ile msg inaingia tu waif akaidaka simu na kukimbia nayo.

Akampelekea mama yake, ambaye akaja akiwa amekasirika sana. Mke wangu akaanza kunitukana kuwa mimi ni malaya na mama mkwe akaanza kuchana chana nguo zangu huku akinisimanga kuwa sina mbele wala nyuma na matusi mengine mengi mazito yasiyoelezeka.

Nguo zangu zikachanwa kiasi cha kuniacha mtupu kabisa, nikamwagiwa maji na kutolewa nje ya geti mchana kweupe.
Simu yangu, vyeti, laptop na vitu vyangu vyote vikabaki kwa mama mkwe wangu.Niliondoka hadi mitaa ya jirani ambako kuna rafiki zangu walionisitiri.

Baada ya siku chache nikaenda Mwanza kuuza ng'ombe wangu, sikuwa na simu wala namna yoyote ya mawasiliano.
Nikiwa Mwanza niliuza ng'ombe nikanunua simu na kumpigia mama watoto.

Akaniambia kuwa yale yote yalitokana na hasira, ndipo nikamuuliza kwani ile msg iliyoleta songombingo ilikuwa inasemaje?
Akaniambia ilitumwa na sekretari wangu na aliiandika Dear boss, hali ya ofisini ni mbaya sana amna amani, i m praying for you. Dah.. Nlivyo ambiwa hivyo nkatamani kucheka na kulia kwa wakati mmoja.

Nikauliza vyeti vyangu, nikaambiwa mama mkwe kachoma moto vyeti vyangu vyote vya sekondari hadi chuo.
Nliposikia hivyo niliumia sana.

Sasa nina mtaji wa milioni saba, wana jamvi anaombeni ushauri wenu je nifanye biashara gani kwa mtaji nilionao? Maana sina tena vyeti, biashara ndio maisha yangu yajayo.

Pole sana, I cried when i read you post, i'm very sorry for what happen to you, how is you wife by the way? is she still with you? Its very difficult situation, they have spoil your life for what they have done, but believe in God things will turn good. I know nothing about bzns, i hope friends in here will tell you what to do, again POLE SANA.

Rock issue ya vyeti ni sensitive tusilete utani na vyeti hawezi pata cheti nje ya document za kumusadia alihitimu elimu gani na mwaka gani. jamani tujaribuni kufikiria zaid jinsi ya kumsaidia

Mkuu naomba nitofautiane na wewe
Chuo chochote kile wanatoa Certified Copy yaani huwezi tena pata original copy ya kile cheti ila wanakupa certified copy baada ya kutoa na kupeleka taarifa ya polisi inayoonyesha upotevu wa cheti husika either kwa moto, kupotea, wizi au janga lolote lile. Chuo au shule (tuseme baraza la mitihani) hawawezi kukunyima hata Certified Copy ya cheti chako iwapo umetoa taarifa za upotevu au kuharibika ambako hakuwezi kuwa repair na taarifa hizo kutangazwa kwenye vyombo vya habari kama magazeti. Ingekuwa hivyo wale wanaopoteza vyeti kwa kuunguliwa hata nyumba zao wasingekuwa na kitu cha kujustfy kuwa walikuw ana vyeti au waliwahi kupitia shule.
Mkuu naelewa cheti ni kitu sensitive sana ila huwezi ukawa blamed for something ambacho hujafanya au is beyond your control

Baraza la mitihani hawatoi tena vyeti. UDSM nimeripoti toka jumatatu, napigwa tu danadana hawaongei jambo lolote la kueleweka.

Swala sio kureport swala ni je umekamilisha masharti maana wale wanapokea taarifa ya polisi na taarifa ya tangazo litakalotoka kwenye vyombo vya habari
Na kwa kuwa vyeti vyako vimechanwa taarifa utakayowapa polisi ni kuwa vimepotea au kuungua moto ili wakuandikie taarifa ambayo utaitangaza
Then UDSM wao wanachotaka ni taarifa ya polisi inayoonyesha sababu ya kuwasukuma wao watoe Certified Copy ya cheti chako

kamshtaki kuwa amechana nyaraka za serikali, ila Mpwa hii story ni kweli? na hizo 7M umezipataje fasta hivyo jamani?? haya pole bana, nenda Dubai kanunue nguo ufungue Boutique au wanavyofanya wenzio wenye mtaji kama wako wametafuta chumba cha biashara Mwenge na kununua Ngua kariakoo na kuja kuziuza kwa bei mbaya akijifanya ndio ametoka kuchukua Dubai au china, ila kama utafungua biashara ya ngu basi ziwe ni za watoto, nakwambia zinalipa sana...all da best

Hata mie mkuu nimepata wasiwasi M7 fasta hivyo kweli na wasiwasi naona shigongo anakosa vijana wa kazi wazuri sana

haiingii akilini mama mkwe achane vyeti kwa kesi ya sms moja tu
sasa akikuharibia maisha,huyo binti yake utaishi nae vipi??????

The Boss;

Mambo ya mke na mama mkwe sio ya muhimu kwangu, kwasasa cha muhimu ni future yangu. Walisema sina mbele wala nyuma... Ngoja nitafute mbele na nyuma

Duuh pole sana mwana kweli inachoma kwa mwanaume kuambiwa huna mbele wala nyuma, ila kaza buti ndugu usije uka give-up, na kuhusu kazi ni bora ukaanza nakazi ambayo unaujuzi nayo...

haiingii akilini mama mkwe achane vyeti kwa kesi ya sms moja tu

sasa akikuharibia maisha,huyo binti yake utaishi nae vipi??????

kuna watu wakiona tu dear wanajua ni mapenzi.
Sikulazimishi usadiki, nimeandika ili kupunguza sononi moyoni mwangu na msongo wa mawazo. Pia nilikuwa nahitaji ushauri wa namna ya kuinvest wisely my 7million

Chakufanya wakati una wait ufanye nn, mtafute kanumba then muuzie iyo script, unaweza pata kiasi cha mboga, ila mm haijaingia kwenye kichwa kabisa, ambae alitakiwa kufanya ivyo ni mkeo na si mama mkwe, mi nibigwa wakuandika story ilo nimegundua,

Back
Top Bottom