meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,349
- 4,674
nimebahatika kumuhoji kijana mmoja huko mjini arusha na kwa ufupi haya ndiyo aliyoniambia....
"kabla ya kumiliki Toyo nilikuwa kibaka nikivizia kinadada na walevi hasa nyakati za jioni na mapema asubuhi.siku moja nilishikwa na kupigwa vibaya na baadaye kulazwa hospitali ya mt.meru kwa muda wa miezi miwili.
Kitendo hiki kiliniuma na kuniabisha sana mbele ya familia yangu.hivyo baada ya kupona nilimuomba baba yangu auze shamba lake dogo kiasi cha milioni moja na nusu.nilitumia fedha hii kununulia Toyo(bodaboda).
Bodaboda hii inaniwezesha kulisha familia na kununua mavazi.uendeshaji wa bodaboda unaniweka kwenye hatari ya kutekwa au kupata ajali lakini sina jinsi!
Nimesikia wameondoa kodi kwa waendesha boda boda lakini wameweka kodi kubwa sana kwa wamiliki wake kama mimi.kwa kweli inaniuma sana''