Jinsi Nilivyofedheheka:Baba wa bi harusi akatangaza jinai ile..

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
736
Quoted in April,2005

Mwaka 1988 nilipata kibarua katika kampuni iliyokuwa eneo la Vingunguti. Kampuni ilikuwa ikishughulika na vifaa na utengenezaji wa vyakula vya kuku wa kisasa.

Kazi yangu ilikuwa kusimamia upakiaji na upakuaji wa vifaa mbalimbali vya kampuni na kwa kiasi fulani nilikuwa napata fedha za hapa na pale. Nilianza kutanua kwa kunywa na wanawake.

Miazi minne tu baada ya ajira,nilishawajaza mimba mabinti wawili,tena mmojawapo alikuwa mwanafunzi! Lakini niliwatolea nje mabinti wale,kwamba hazikuwa zangu..
Kwa kuogopa mkono wa sheria hasa juu ya yule mwanafunzi,ilibidi niache kazi mwaka 1989.

Mwaka 1990,nilijiunga na kozi ya Uhasibu,na kuhitimu 1993. Nilipata kazi safari hii katikati ya mji.
Mwaka 1995 nilichukua maamuzi ya kuachana na mambo ya ujana na kuoa. Nilipata dada mmoja,na tukaanza mahusiano,hatimaye tukaamua tuoane. Zikaanza hatua za barua,nayo ikajibiwa na mahari ikatajwa.

Kisha ikatangazwa siku ya bwana harusi mtarajiwa kwenda kutambulishwa kwa wazazi wa mwanamke. Nakumbuka ilikuwa Jumamosi. Wazazi wa binti walikuwa wakiishi Mabibo External.
Tulipata mapokezi mazuri na kukaribishwa ndani.

Tukiwa sebuleni,nilimwona msichana mmoja akichungulia.Akachungulia tena,na kisha akajitokeza kabisa. Unajua kuna wakati jambo linaweza kutokea na ukahisi kabisa unaota tu!

Msichana aliyejitokeza,ni yule msichana mwanafunzi niliyempa ujauzito,na kisha kutoroka! Alisimama pale sebuleni bila kusalimia,na aliondoka kuelekea uani ambako tulisikia kilio.Halafu tulisikia kimya cha muda fulani.

Baadaye,baba wa bi harusi mtarajiwa akaja sebuleni na kutangaza kwamba ameshwasiliana na Polisi,kwani bwana harusi mtarajiwa alishatenda jinai kwenye nyumba ile. Nilielewa maana ya kauli ile,ingawa baba,mshenga,na rafiki yangu aliyenisindikiza,hakuelewa chochote.

Nilijua mambo yameshakuwa magumu,Polisi tena?! (miaka 30) Na kwa nguvu ambazo siwezi kuzielezea hadi leo,nilijikuta niko mlangoni,na nilitimua mbio nadhani kwa Tanzania hii,hakuna mwanariadha ambaye angenipita kwa kasi ile. Nikajikuta niko ndani ya Taxi.

Lakini ulikuwa ni ubwege tu,kwani baba,mshenga na rafiki yangu walikuwa wamebaki pale.

Sina haja ya kukupa maelezo mengi..ila kwa kifupi,yule binti aliyeangua kilio baada ya kuniona,ndiye mke wangu,na tuna watoto watatu sasa! Nikitaka kumchekesha mke wangu,huwa namkumbushia sakata lile...
 
Kwa hiyo ulifungwa miaka mingap?
Alifungwa pingu za maisha na binti aliyemtia mimba miaka ya nyuma(mwanafunzi) ambaye alikuwa wa familia moja na aliyetaka kumuoa,kwa lugha ingine alibadilishiwa mke tu na kesi kwisha.
 
Alifungwa
pingu za maisha na binti aliyemtia mimba miaka ya nyuma(mwanafunzi)
ambaye alikuwa wa familia moja na aliyetaka kumuoa,kwa lugha ingine
alibadilishiwa mke tu na kesi kwisha.
Sasa mchumba ambaye kwa sasa ni shemeji mapenzi yameisha?
 
Alifungwa pingu za maisha na binti aliyemtia mimba miaka ya nyuma(mwanafunzi) ambaye alikuwa wa familia moja na aliyetaka kumuoa,kwa lugha ingine alibadilishiwa mke tu na kesi kwisha.

Asante uporoto01
Ume-elaborate vizuri kabisa..
 
Sasa mchumba ambaye kwa sasa ni shemeji mapenzi yameisha?

Lazima yasiwepo.. Yaani si kuisha tu.. Yalikufa kabisa!

Na yeye mwenyewe alidevelop chuki fulani kwangu,ambayo imechukua muda mrefu kumpoa.. Imempoa miaka ya karibuni..
 
Inaitwa kukubali matokeo hahaha!

Hata na yeye alihisi fedheha mbele ya wazazi na ndugu zake wengine..

We mtu uliyekuwa unamfagilia kwa ndugu zako kama "Mr Right",halafu yawe hayo... Mchezo! Kwa wengine hata kuzimia angezimia!
 
Inakuwa ngumu.....!!

Mi mwenyewe nimekuwa nikimuogopa! Ilituchukua muda kukubali hali halisi..
-Yaani kwake kukubali mimi kuwa shemeji yake katika mazingira ya kuwa nilishatenda kitendo kiovu kwenye familia yao..
-Na mimi kuonekana kwake kama mtu mwenye tabia chafu sana huko nyuma,na ukizingatia nilikuwa nimemficha historia yangu..
Hata mimi kum-face ilikuwa taabu..
 
Kwa hiyo hata shemejio ulishawahi kumchakachua.
MP.

Niliwahi kukutana kimwili na mchumba wangu..

Mambo yalipoharibika akawa shemeji sasa.. Hakuna aliyejua kati yetu kama mimi naweza kuwa namfahamu hata mtu mmoja wa familia yao hapo kabla..
 
Back
Top Bottom