Jinsi nilivyofedheheka: Ati Niliitwa "MSOMI MALAYA"....

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
736
Ilikuwa mwaka 1973,nikiwa sekondari ya serikali,kidato cha pili. Na dhahama hilo lililtokea nikiwa likizo nyumbani Korogwe,Tanga.
Kipindi hicho mtoto kufaulu ililuwa jambo la ujiko sana..hata jamii ya kijijini kwetu ilikuwa ikiniheshimu sana.

Wakati huo ndiyo naanza kubalehe,nilikuwa nampenda sana dada mmoja aliyekuwa akisoma darasa la saba. Shida ni kwamba alikuwa anabanwa sana na familia yake hivyo kuonana ilikuwa taabu ingawa naye alishakubali maombi yangu.

Siku moja ya Jumapili tulikutana kanisani na tulipotoka tukapanga mpango,ambapo aliniambia nimfuate nyumbani kwao usiku wa saa 8! Nalimwuliza kwa nini muda huo akajibu,kuwa kwao huchelewa kulala hadi saa 6 usiku,hivyo saa 8 wanakuwa wameshazama kwenye usingizi mzito.Nikakubaliana naye.

Kwangu kutoka haikuwa shida kwani nilikuwa naishi mabanda ya uani. Nilipofika kwao,nilijibanza karibu na mlango wa ua na ndipo nilipoona mlango wa ua ukifunguliwa taratibu,na mtoto akatoka. Ingawa kulikuwa na gizagiza nilitambua alikuwa amevaa khanga,nami nikamrukia na kumkumbatia kwa mahaba.Akanivuta ndani kwa fujo kidogo,badala ya mahaba,nikashangaa lakini nikahisi itakuwa ni sababu ya woga.

Aliniingiza uani kwao ambako hakukuwa na taa,lakini ghafla taa ziliwashwa! Nilistuka kwani niliona kuna kikundi cha watu pembeni. Halafu nilipomwangalia kwa makini yule niliyedhani ni yule binti,nilitamani kupiga yowe kwani alikuwa ni mama yake mzazi!

"Haya mkwe wangu sema utanipa mahari kiasi gani nikupe binti yangu"alisema mama yule. Nilipotazama kwa makini lile kundi pembeni,nilitamani ardhi ipasuke kwani alikuwa ni baba na mama yangu na kaka yangu mkubwa! Nikiwa nimeduwaa,nilijaribu kuangaza bila mafanikio nikimtafuta yule binti.. Kwanini hakuwepo sikupata majibu.

Lakini baba yangu alikuwa na majibu... Kwani alikuja na kunibana mbavu,akanidunda sana kama mbwa mwizi!ilibidi waliokuwepo pale kuingilia.. Kaka yangu mkubwa naye aliniwasha vibao hevi kama vitatu vya haraka. Nasema hevi maana niliona nyota nyingi sana!

Wakati huu yule binti aliletwa akaamriwa kulala chini,nami nilale chini. Hapo tulitandikwa sana bakora. Wakati huo majirani walishasikia zogo lile na walishajaa uani pale..Tulichapwa na tulilia kama watoto wanaonyonya!

Baada ya adhabu hiyo,baba alichukua tenga na mauchafu-chafu mengine ambayo naamini alikuwa ameyaandaa,akanifunga mwilini na kuniambia twende nyumbani. Wakati huo aliwaomba majirani wanizomee. Nilizomewa njia nzima na huku wengine wakinirushia mchanga! Walikuwa wakiimba "msomi malaya,msomi malaya"
Hadi nafikishwa nyumbani nilikuwa hoi. Kufika asubuhi habari ile ilishaenea karibu kijiji kizima. Kwa kweli nilijisikia fedheha sana.Bahati na likizo ilikuwa ndiyo inaishaisha.

Baadaye nilikuja kujua ni mdogo wa yule binti,ambaye walikuwa hawaelewani,alikuwa amejificha huku akisikiliza mpango wetu,na akaenda kumwambia mama yake,mpaka yakatokea hayo yaliyotokea..

Hata hivyo baada ya kuwa nimeanza kazi,yule binti alikuja kuwa mpenzi wangu..
 
Wa chuo kikuu kwa sasa akifanya uliyofanya.no cares calling 'msomi malaya'
 
Inaonyesha huyo mkweo ulimpa hug ya nguvu na rasharasha ya vijidenda vya hapa na pale,. Kweli we ulikuwa kidume dinda.. Nachelea kwa mdadi ulokuwa nao them days utakuwa umemshika hata sehemu khatwari huyo mama mkwe... Na ilikuwaje ushindwe kudoubt mwili wa demu wako na bimaza akee????@trachomatics
 
pole mkuu, stori nzuri sana

Asant NS...

Sema ni ya kweli... Na ingawa hainihusu mimi,ila ni kisa kilichomtokea huyo baba miaka hiyo.
Na nitaendelea kuwapatia experience za watu mbalimbali ya mambo,vituko,na visa viivyowakuta Watanzania wenzetu..
 
Hiyo style ya kusindikizwa na kushangiliwa ilikuwa inaitwa 'kindumbwendumbwe'
Hii stori imenikumbusha wazazi wa zamani walivyolea watoto wao kwa ushirikiano. Siku hizi ukimuambia jirani mwanao anamfukuzia binti yangu, hukawii kukimbizwa na binduki!
 
Wa chuo kikuu kwa sasa akifanya uliyofanya.no cares calling 'msomi malaya'

Hiyo zamani Bei Mbaya...

Enzi hizo,mtoto wa mwenzio ni wako... Yaani nikimwona mtoto wa jirani anafanya kosa ni ruksa kumuadabisha hata kwa kumchapa,na hata mzazi wake akija,akielezwa anaelewa.

Siku hizi huwezi kufanya hilo..
 
Inaonyesha huyo mkweo ulimpa hug ya nguvu na rasharasha ya vijidenda vya hapa na pale,. Kweli we ulikuwa kidume dinda.. Nachelea kwa mdadi ulokuwa nao them days utakuwa umemshika hata sehemu khatwari huyo mama mkwe... Na ilikuwaje ushindwe kudoubt mwili wa demu wako na bimaza akee????@trachomatics

Hata kidogo... Hakukuwa na na denda...
Ilikuwa ni environment ya hofu na mfadhaiko. So hug haikupokelewa na ndiyo maana nilidoubt huyo dear wangu kunivuta kwa fujo ndani kwao...

Ilikuwa ndiyo game yangu ya kwanza kama ningefanikisha... Nikafail Vanmedy! Kwa kuwa hakuwa manzi wangu,ndiyo tulikuwa tuanze mahusiano.. nilikuwa sijamzoea kuweza kumtofautisha,na ukichanganya na giza tena,ndiyo hivyo...
 
Hiyo style ya kusindikizwa na kushangiliwa ilikuwa inaitwa 'kindumbwendumbwe'
Hii stori imenikumbusha wazazi wa zamani walivyolea watoto wao kwa ushirikiano. Siku hizi ukimuambia jirani mwanao anamfukuzia binti yangu, hukawii kukimbizwa na binduki!

Yeah... We unajua...

Kindumbwendumbwe...

Siku hizi mzazi amshikishe adabu mtoto wa mwenzie hajipendi....
 
Uhuni tu....mmefunga ndoa?

Aah wapi...
Wajua kazi enzi zile si lazima ufanyie kwenu... Na pia haimaanishi alikuwa mpenzi wangu wa kudumu... Ni kwamba,tuliwahi kupeana mapenzi,huenda stori jinsi ilivyo inajieleza..

Umeona movie ya Titanic? Watu walipendana siku moja tu! Lakini umeona ilivyokuwa... So mapenzi yana athari nyingi,+ve na -ve...
 
Back
Top Bottom