Jinsi Nilivyofedheheka: "...akasogeza kiti na kupandisha gauni,...akasema...."

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
736
Hii yangu sikui niite fedheha ama la... Ingawa waliokuwepo waliichukulia kama mzaha wa mhusika,nadhani ni katika kupunguza kiwango cha fedheha kwao we yewe..

Mwaka 1999 nilikuwa katika kuhangika kutafuta kibarua,nilijikuta katika ofisi moja ya jamaa yake baba(walikuwa wakifahamiana). Walikwisha kuwasiliana na baba,hivyo nilienda kuangalia uwezekano wa kupata ajira pale.

Nilifika ofisi hiyo saa mbili na robo hivi asubuhi. Mapokezi ilikuwa ikitumika kama ofisi kwa watu wengine. Nikaongea na "receptionist",akanieleza kuwa bosi hufika kuanzia saa tatu,hivyo nimsubiri.
Mgeni nilikuwa peke yangu,na pale ofisini palikuwa na akina dada watano pamoja na yule dada wa mapokezi.So,mwanaume nilikuwa peke yangu.(alikuwepo mmoja,ambaye nilipishana naye anatoka wakati naingia.

Nilikaa kwenye makochi,na mbele yangu kulikuwa na mwanamke aliyekuwa anafanya kazi zake.Mara akusanye makaratasi ayabane,mara aandikeandike,mara achukue faili,mara.... Ili mradi alikuwa bize.. Sasa tatizo mwanamke huyu,alikuwa amekaa "kihasara" kweli!
Yaani alikuwa amevaa gauni fupi,na ameachia mapaja yake bila wasiwasi. Nikiwa kijana shababi,niliona bora niifaidi sinema ile ya bure... Nikimwona mama yule ananitazama...., nageuza macho,na kujifanya simuangalii yeye.

Niliendelea na sinema ile kama robo saa tu,kabla yule mama hajaacha kufanya kazi zake. Aliinuka,na kuchukua kiti chake,na kuja nacho kwenye makochi nilipokuwa nimekaa.. Sikujua alikuwa na lengo gani,maana aliweka kiti kile mbele yangu,na kisha alipandisha gauni lake fupi hadi juu kabisa!
Kisha alikaa kitini na kunitazama. Wale wanawake wengine waliacha kazi zao na kushikwa mshangao..." ...vipi mwenzetu,kuna nini kimekupata..?" mwanamke yule akajibu,"..nataka ayatazame mapaja na vingine kwa karibu ili afaidi vizuri.Naona anapata shida sana kuibaiba,haya tazama baba,uridhishe nafsi yako..."

kila mmoja alielewa maana yake,nikiwemo mimi. Ni kweli nilikuwa nikimtazama kwa hila,lakini haikuwa na maana nilikuwa namchungulia. Nilibaki nimeduwaa,na sikuwa na niliyemzoea labda niombewe radhi,hata mdomo nao ulishikwa na kigugumizi,wala sijui kilipotokea!
Mmoja kati ya wale akina dada alisema,"dada Glady naye haishi vituko,hebu mwache kijana wa watu..."
Mwingine alidakia,"...utamweza dada Glady vituko vyake basi?!" Yule mwanamke ambaye nilikuja kumjua kwa jina Glady,akasema"...hapana,wanaume wengine bwana hawana adabu,macho wayuwayu sana. Nataka kiu yake iishe leo..." akanigukia tena,..." hebu cheki sasa uridhike.."

Mlio wa gari la bosi wao ndiyo ulioniokoa kutoka katika kadhia ile. Aliposikia mngurumo wa gari,aliinuka na kushusha gauni lake,akachukua kiti na kukirudisha kwenye deski lake huku akisema," ... Bahati yako,ungeniambia leo,nini kinang'aa zaidi...,nyota au mbalamwezi.."

Una haja ya kujua kilichoendelea? kama unataka kujua zaidi,njoo hapa Victoria,ndipo ofisi hizi zilipo,nami nafanya kazi hapo,na yule mama yupo,nafanya naye kazi..
 
hii hadithi mbona sio mara ya kwanza kuisikia...hebu ngoja nikumbuke niliisikia wapi vileeee
 
mumeshaanza kumcopy mzee Mtambuzi bila kumuacknowledge?aibu....

Una haki ya kusema unachoamini...

Ila kwa faida yako nakujulisha kuwa,mimi na Mtambuzi,tuna "same source of these true life experiences"... Na zaidi ya hapo,tuna mawasiliano ya hadi kwa PM... So,no enemity between us all...
 
Kwani wewe kila siku unavaa nguo mya? Ukirudia wewe unaona sawa, akirudia mwingine basi ndo mnaweka na viinglishi

Asante Ngalikihinja..
Halafu,tatizo liko sehemu moja... Source ya hizi news kwa Mtambuzi,ndiyo source yangu mimi pia! So kujua mwenzangu kama alishapost article fulani,ni vigumu...

So,mimi ntaendelea kuwapatia yale ninayoona yanaifaa JF kama kuburudisha,kuelimisha,na vinginevyo itakavyoonekana inafaa...
Kama itakuwa ni marudio,someone will say,otherwise,wapo watakaobenefit.....
 
Asante Ngalikihinja..
Halafu,tatizo liko sehemu moja... Source ya hizi news kwa Mtambuzi,ndiyo source yangu mimi pia! So kujua mwenzangu kama alishapost article fulani,ni vigumu...

So,mimi ntaendelea kuwapatia yale ninayoona yanaifaa JF kama kuburudisha,kuelimisha,na vinginevyo itakavyoonekana inafaa...
Kama itakuwa ni marudio,someone will say,otherwise,wapo watakaobenefit.....
Kuna watu wao ni kuangalia nani kakosea nini... na nani kauliza kitu ambacho kwao wanakiona cha kijinga
 
Back
Top Bottom