Jinsi Lowassa alivyojichomeka sherehe za RC Ifakara na kumchefua kardinali Pengo

huyu lowasa wamshauri vizuri wanaomzunguka kuwa afanye mambo mengine suala la urais aachane nalo huyu si msafi na bado hajatubu dhambi zake kwa watanzania kwa kuiruka hatua hii itamtesa maisha yake yote.
 
wewae ndo unaropoka ovyo kumtukana kardinali kwa kigezo cha kufahamu cano law. Alichosema mwadhama kardinali ni kukiukwa kwa protocal, ujue yeye ni askofu mkuu wa dar es salam, majimbo ya ifakara, lindi, mtwara, morogoro, yapo kwenye arch diocese ya dsm ambayo pengo ndo msemaji wake.

Mkuu hapo kwenye red kuna matatizo kidogo, jimbo la lindi na jimbo la mtwara yapo chini ya askofu mkuu mtega wa jimbo kuu la songea, mengine nakubaliana na wewe!
 
@Pasco
Kanisa halibagui nani anaenda kanisani, na wala halijamuhukumu Lowasa! Kanisa lina taratibu zake na si kila mtu anapata jukwaa la kuzungumza. Lowasa angekaa kama muumini mwingine sidhani kama Pengo angesema!

Again kwenda Rome sio kigezo cha kuufahamu ukatoliki, ila HONGERA kwa kufika Vatican, personaly nimeshanote kuwa umefika Vatican!
Mkuu Kaunga, nakubaliana na wewe ila pia waumini safi ni wale ambao wanaujua usafi wa Kanisa Katoliki tangu kule jikoni Vatican ila tumejinyamazia, sasa kiongozi wetu mkuu anapokuja na kutoa kauli za kuwa sideline baadhi ya viongozi wetu kwa kuwanyooshea vodole hadharani kisa tuu sio Mkatoliki!. Unadhani Mkapa angekuwepo na Bendera kwa kutambua uwepo wa Mkapa na kumpa nafasi kusalimia unadhani Mwadhama Polycarp Cardinali Pengo angeyasema hayo aliyoyasema against EL?.
 
Mkuu Kaunga, nakubaliana na wewe ila pia waumini safi ni wale ambao wanaujua usafi wa Kanisa Katoliki tangu kule jikoni Vatican ila tumejinyamazia, sasa kiongozi wetu mkuu anapokuja na kutoa kauli za kuwa sideline baadhi ya viongozi wetu kwa kuwanyooshea vodole hadharani kisa tuu sio Mkatoliki!. Unadhani Mkapa angekuwepo na Bendera kwa kutambua uwepo wa Mkapa na kumpa nafasi kusalimia unadhani Mwadhama Polycarp Cardinali Pengo angeyasema hayo aliyoyasema against EL?
hata wakati wa kumsimika askofu gervas nyaisonga wa dodoma, mkapa alikuwepo, ila alitambuliwa uwepo wake na hakuhutubu,
pili mkapa ni rais msaafu, lowassa ni nani?
then kama kanisa si safi, maana yake hata imani linayoisimamia siyo ya kweli, unafanya nini humo?
 
Unataka kusema watu wanaompinga Lowassa ni wakatoliki tu? Kwamba KKKT yote inamkubali? Anglican yote inamkubali? Waislam wote wanamkubali? Na kama kanisa katoliki linampigia debe Wilibodi (nadhani unamaanisha Dr.Slaa) kwa nini wasimualike kwenye harambee za kanisa ili wamnadi vizuri? Na kama Lowassa hatakiwi na kanisa kwanini anajipeleka kwenye shughuli za hilo kanisa?

Mtazamo wangu: Hapa si Lowassa wala kanisa wanaweza kujiosha. Matukio ya kuunganisha pande hizi mbili yameanza kuongezeka siku hizi za karibuni. Ni bahati mbaya?
Mkuu FJM, kuna silent role ya Kanisa Katoliki katika politics za nchi hii!. Ndio maana EL haangaiki na ELCT bali na TEC!. Ile kauli ya JK ni chaguo la Mungu ilitolewa na Askofu Medhod Kilaini na ilimsaidia JK kupaa kwa ushindi wa over 80%!. Ilimcost Kilaini akatupwa kule pembezoni kufungwa mdomo!. 2010 TEC wakatoa waraka na matokeo ya JK sote tunayajua!. Yoyote anayefikiria kuwa mpangaji pale magogoni, lazima atafute uungwaji mkono wa TEC!.
 
Hivi nyie wamakanisani hamkomi tu kuwaalika wanasiasa kwenye shughuli zenu?
Mmesahau alichowaambia Rais Kikwete kule Songea kuwa mnauza unga?
Acheni mambo hayo, nyie fanyeni mambo yenu bila kuwahusisha,
Mnajiaibisha tu!
 
Kanisa katoliki na hasa Pengo wajifunze kutokana na hii blunder. Hiyo shughuli ilikuwa ya kanisa na sio ya mkuu wa mkoa. Kwanini wasi-take control ya shughuli yao badala yake kumwachia mwanasiasa? (Mkuu wa mkoa na harufu nzito ya siasa).

Kanisa lingeweza kuandaa list ya watoa salamu, na kumuita mtu mmoja mmoja kama walivyopanga atoe salamu. Hakuna ulazima wa kupanga 'matofali' ili kumuita mtu, kwa maneno mengine hakukuwa na ulazima wa kanisa kumuita mkuu wa mkoa ili huyo mkuu wa mkoa amkaribishe Mwinyi!!! Hizi ni protocol za kisiasa, kanisa liko huru kufuata protocol zake kwenye shughuli yao.

Kwa kifupi sikubaliani na maelezo ya Pengo, Kanisa katoliki lina intelligensia ya hali ya juu, wangetaka kujua Lowassa anafuata nini Ifakara wangejua, lakini either hawakufanya au walifanya na kuweka mambo kabatini. Na Lowassa hajanzaa kuongea kwenye shughuli za kanisa katoliki leo, alikuwa Mwanza,hivyo Ifakara ni mwendelezo tu.

Pengo akubali kanisa limeingia doa, and it is up to him kama kiongozi wa kanisa nchini Tanzania kutafuta 'jiki' vinginevyo waumini wengi wamefadhaika na huu mchezo wa harambee. Kanisa limeegemea mno hela! Jukumu la kuhubiri Injili linafifia. Na hii inatokea under Pengo's watch!
Mkuu FGM, whats a big deal kumruhusu mtu kusalimia?. Kanisa hilo hilo limekubali EL alichangishie mamilioni na kanisa kuyashangilia lakini leo EL kusalimia ndio limekuwa doa?!.

Siku hizi wenye vipochi vinene ndio wananyenyekewa?. Hata hayo makanisa ya wakovu wale unaowaona viti vya mbele na suti nadhifu ndio wenye nazo, akina sisi tunafichwa nyuma!.
 
acha kuandika pumba nenda ukachat na wenzako wa facebook....kwa hiyo unataka kusema EL NI MSAFI!!!!
 
Naomba niliweke sawa hili na ieleweke kuwa msemaji mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania ni Mwenyekiti wa TEC kwa sasa Mhashamu askofu Ruwaichi ambaye pia ni Askofu mkuu wa Mwanza. Hii ni kwa mujibu wa sheria za Kanisa(Canon Law). Pengo kazi yake ni kushauri Papa(Baba Mtakatifu huko Rome) na si vinginevyo. Cheo cha kiutendaji alicho nacho hapa nchini ni Askofu Mkuu wa Jimbo la DSM. Ukardinali haumpi mamlaka ya kuwa msemaji mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania hata mara mmoja. Hivyo kisheria kama kweli amesema maneno hayo basi hayo yanabaki kuwa maoni na mtazamo wake binfsi. Huu siyo matazama wala maoni ya Kanisa Katoliki Tanzania. Jamii ya watanzania inatakiwa kuzipuuza kauli nyingi zilizojaa utata na ubaguzi anazotoa Kardinali Pengo.Hayo yanabaki kuwa maoni yake binafsi kama Pengo.

Siku ya tukio;


Neno la MUNGu: Yesu Kristo yeye mwenyewe alisema: "Sikuja kwaajili ya wenye haki, bali wenye dhambi".Yesu Kristo alikula na wadhambi, alishirikiana na wadhambi bila yeye kuwa na dhambi.

OMBI
: Naomba nimkumbushe Pengo kuwa anapotoa kauli zake ajue kuku yeye ni mchungaji wa wema na wabaya. Ajue kuwa Mungu anawapenda watu wote bila ubaguzi.Hii ni aibu kwa mtu msomi wa Teolojia kama Pengo kukurupuka na kuanza kuropoka hovyohovyo namna hii.Atambue kuwa Raisi ndiyo kiongozi mkuu wa nchi, hivyo inastahili heshima zake. Pengo aache kuropoka ropoka hovyo hovyo kama mlevi.Mbona maaskofu wenzake wamekaa kimya? Yeye ni nani?
Mkuu uko sawia na unazijua vizuri taratibu za kanisa katoliki. Unajua watu wengi wanadhani Muadhama Polycarp Kardinali Pengo ndiye mkuu wa maaskofu Tanzania. Hawajui juu ya utawala wa kanisa ya kwamba kila jimbo linajitegemea. Kama alivyo Ruwaichi wa Jimbo kuu la MWanza ni sawa na Askofu Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na hakuna Askofu Mkuu wa Tanzania!

Mkuu safi sana kwa elimu yako.
 
Mimi ni Mkatoliki, kutokana na heshima kwa dhehebu langu sio busara kuujadili humu usafi wa Kanisa Katoliki ila kutaka kumtenga EL kwa kisingizio si msafi hakina mashiko. Kwani Masiya alikuja kwa ajili ya waliopotea na wasio wakamilifu. Nimebahatika kufika mpaka Rome na kuishuhudia lile dungu la dhahabu pale juu kwenye ule mduara, si wengi wanajua hìlo dungu lilitoka wapi na lilipatikanaje mpaka kufika hapo!. Sio wengi wanawajua the realy funders wa Vatican!. EL anauchafu gani wa kuwa despised na Kanisa Katoliki!. Tatizo la kanisa letu, the right men ni kwao ni Wakatoliki tuu kama alivyokuwa Julius, akaja Beninyamini na sasa wanampigia chapuo Berinado au Wilibodi!. Kwa vile EL ni Mlutheri, huyo kwao sio!.

Hapana Mkuu, Pengo ameelezea kukiukwa kanuni na taratibu za sherehe hizo baada ya mkuu wa mkoa kujipa maamuzi ya ratiba.Kwani Mbona Mwiny alialikwa,na yeye ni mwislam.Wakatoliki sio wabaguzi,Ila sio OPPORTUNISTS.Ukweli utabaki palepale LOWASSA hakualikwa na kanisa.Amejipeleka mwenyewe,May be Bendera ndo alimwambia njoo.Kumbuka siku chache kabla ya tukio hilo askofu wa jimbo husika alitoa ufafanuzi kwamba Lowasa hajaalikwa.
 
Mimi ni Mkatoliki, kutokana na heshima kwa dhehebu langu sio busara kuujadili humu usafi wa Kanisa Katoliki ila kutaka kumtenga EL kwa kisingizio si msafi hakina mashiko. Kwani Masiya alikuja kwa ajili ya waliopotea na wasio wakamilifu. Nimebahatika kufika mpaka Rome na kuishuhudia lile dungu la dhahabu pale juu kwenye ule mduara, si wengi wanajua hìlo dungu lilitoka wapi na lilipatikanaje mpaka kufika hapo!. Sio wengi wanawajua the realy funders wa Vatican!. EL anauchafu gani wa kuwa despised na Kanisa Katoliki!. Tatizo la kanisa letu, the right men ni kwao ni Wakatoliki tuu kama alivyokuwa Julius, akaja Beninyamini na sasa wanampigia chapuo Berinado au Wilibodi!. Kwa vile EL ni Mlutheri, huyo kwao sio!.


abomination!!
 
Mkuu FJM, kuna silent role ya Kanisa Katoliki katika politics za nchi hii!. Ndio maana EL haangaiki na ELCT bali na TEC!. Ile kauli ya JK ni chaguo la Mungu ilitolewa na Askofu Medhod Kilaini na ilimsaidia JK kupaa kwa ushindi wa over 80%!. Ilimcost Kilaini akatupwa kule pembezoni kufungwa mdomo!. 2010 TEC wakatoa waraka na matokeo ya JK sote tunayajua!. Yoyote anayefikiria kuwa mpangaji pale magogoni, lazima atafute uungwaji mkono wa TEC!.
unanamaanisha pamoja na kutunyima maisha bora kama alivyosema awamu ya kwanza, kukidhiri kwa ufisadi,mfumuko wa bei,ukosefu wa umeme nk kikwete angepata ushindi wa kimbunga hii awamu ya pili kama kanisa lingemuunga mkono?
 
Hongera sana wadau.
Nimejua kuwa WaTZ sasa wanajua kuchambua mambo.
UKWELI: Pengo is absolutely right kwa kutoa msimamo huo. Yeye ni mlezi,mchunguji na misimamizi wa maadili ya Kanisa katoliki. Sasa naomba wote tutambue kuwa Kanisa Katoliki ni Sauti ya wasio na sauti(voice of the voiceless).

HONGERA SANA KARDINALI PENGO! GOD BLESS YOU ALL THE TIME!
 
Mkuu FJM, kuna silent role ya Kanisa Katoliki katika politics za nchi hii!. Ndio maana EL haangaiki na ELCT bali na TEC!. Ile kauli ya JK ni chaguo la Mungu ilitolewa na Askofu Medhod Kilaini na ilimsaidia JK kupaa kwa ushindi wa over 80%!. Ilimcost Kilaini akatupwa kule pembezoni kufungwa mdomo!. 2010 TEC wakatoa waraka na matokeo ya JK sote tunayajua!. Yoyote anayefikiria kuwa mpangaji pale magogoni, lazima atafute uungwaji mkono wa TEC!.


Pasco, kwa kifupi unachosema hapo ni kwamba Lowassa (walau kwa sasa) anawinda support ya kanisa sio? Soma vizuri ujumbe wako.


Pili, kuna hoja yako nyingine hapo juu ume-hint 'utakatifu wa kanisa' na umeenda mbele zaidi kwa kusema wewe unalifahamu hilo! Pasco unapata wapi hizi habari? Unasoma vitabu gani? mimi ni mkatoliki, kanisa lina mambo mazuri tena mazuri sana, lakini upande wa pili wa shilingi sio mzuri. Kuna dark side vibaya na hili kwa sababu kanisa linaongozwa na binadamu. Huitaji kwenda Vatican (physically) kutambulia historia yake.
 
Back
Top Bottom