Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,316
- 33,125
Pindi unapobadilisha mtambo endeshi na kuweka mtambo endeshi wa aina ya Windows 7 au Windows Vista,basi mitambo hiyo huifadhi mtambo ulipita katika faili moja ambalo hulipa jina la Windows.old. Faili hili huifadhiwa kwenye C:\Windows.old,ambapo C: ni
sehemu mojawapo ya mgao wa kompyuta.Sio lazima iwe C:,inaweza kuwa yoyote kutegemeana na nafasi au wapi umehifadhi mtambo endeshi.
Umuhimu wa Windows.old ni kwa ajili ya mambo ya tahadhari kwani inawezekana ulifuta
au kuondoa windows ya zamani kimakosa hivyo kwa kutumia Windows.old unaweza kurudisha mtambo wako wa zamani.Windows.old huwa inajaza nafasi ya kompyuta.hivyo kama una uhakika kuwa huitaji tena mtambo endeshi wa zamani basi unaweza kulifuta hili
faili la Windows.old,lakini kazi sio rahisi kihivyo kama unavyoweza kufikiria.
Kutokana na ugumu wa jinsi ya kufuta hili faili,basi leo hii nitakuelezea ni jinsi gani unaweza kufanikisha hilo.
Fuata hatua zifuatazo:
1.Bonyeza My Computer utaweza kuziona diski zako zote,nenda kwenye diski ambayo umehifadhi mtambo endeshi.Bonyeza right click,chini kabisa bofya sehemu iliyoandikwa Properties. Kutatokea kijiboksi kipya kama kinavyoonekana chini.
2.Kwenye kidirisha kipya,bonyeza sehemu iliyoandikwa Disk Cleanup. Hii itatumia muda kwani itakokotoa kompyuta kwenye diski husika kuangalia ni mafaili yapi yanaweza kufutwa.
3.Baada ya kukokotoa kompyuta yako,basi kutatokea kidirisha ambacho kitaonesha mafaili yote yaliyopo kwenye kompyuta.Bonyeza sehemu iliyoandikwa Clean up system files.
4.Hakikisha umechagua sehemu iliyoandikwa Previous Windows installation(s) imewekea alama ya vema,kwani kwa hapo ndio sehemu yalipojificha mafaili yako.Baada ya hapo bonyeza OK.
5.Kutatokea kidirisha kipya,bonyeza Delete Files inayoonekana kwenye kidirisha kipya.
6.baada ya hapo basi tegemea mafaili ya zamani(windows.old) yatakuwa yamefutwa na kuondolewa toka kwenye kompyuta.
Mambo sio marahisi kama hivi ,kuna wakati mambo yanaweza mrama zaidi kwani kuna uwezekano ukawa umeshayafuta mafaili na vitu vilivyomo kwenye Windows.old lakini mafolder yake yanaweza kuwa hayajafutwa,hivyo unaweza tumia jiwe moja kuyafuta
haya mafolder vinganganizi.
Bonyeza Start na kwenda kwenye Search andika rd /s /q c:\windows.old bila kuacha nafasi.Hii itakuwa imemaliza kila kitu na sasa kila kitu kitakuwa kimefutwa toka kwenye kompyuta.
Ni matumaini yangu kuwa makala hii itakuwa na faida kwako mwana AfroIT,kama utakumbana na matatiuzo basi tuma maoni yako.