Jinsi CCM Itakavyomtumia Zitto Kushinda Urais 2015

Status
Not open for further replies.
Kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji,mtapiga kelele weeeeee lakini mwisho wa siku zitto ndie rais.timing nzuri kwa mwanasiasa mkongwe kama zitto ndo hiyo,kufika 2015 tayari jina lake litakuwa limeshazoeleka masikioni mwa walio wengi hasa vijana wapiga kura.
Bravo zitto,good timing,a well focused leader.

a well focused leader kwenye mafanikio binafsi... maelezo yako yanathibitisha roumors za ubinafsi wa zzk. halafu viongozi huwa hawaji kwa mtindo sa zzk. maoni yangu.
 
Maneno haya ya busara yanatosha kabisa kuwamaliza wale wote wana kaa na kuota. huu ujumbe umewafikia vyema na wameupata wale wote wachonganishi hasa ccmweli.

yan mh zitto tunashukuru umewambia ccmweli waziwazi nadhani sasa wataondokana na hii ndoto na watatafuta wimbo mpya wakuja nao maana huu umewashinda sasa. na kamwe hawataweza.

Nadhani sasa ccmweli mmeishiwa cha kusema.

Tambwe Hiza alisha wahi kujiapiza wakati fulani ya kuwa kuliko yeye kurudi ccm ni bora alale na mama yake kama alalavyo na mkewe, leo yoko wapi!!
 
Nakushukuru sana Bw.Kaldinali kwa mawazo na uchambuzi wako mpana.
Kwangu binafsi na mwingine yeyote anayeunga mkono mabadiliko ya uongozi hususani
mfumo wa chama kinachozolrotesha maendeleo ya nchi kiuchumi,basi utaungana nami kumpongeza
huyu mtoa maada.
Unajua kumekuwa na marumbano mengi sana ndani ya CDM hata mengine yasiyo ya msingi mbele ya wananchi kupitia vyombo vya habari ukiachana na Chibuda
VIONGOZI CHADEMA au chama chochote chenye nia na dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko, chondechonde acheni kuendekeza marumbano baina yenu inawapotezea uwezo wa kukubalika kwa wapiga kura.



Wakuu

Nadhani wote tunajua kuwa CCM inapanga kutumia kila mbinu on earth ili kuendelea kutawala mwaka 2015 kihalali au kwa zuluma. Sasa hivi, Chama Hiki (ambacho kwa sasa ni marehemu) kiko kwenye mikakati mikubwa na madhubuti ya kuhakikisha kitaendelea kutawala hata kama hakitapata kura za kutosha mwaka 2015. Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na:

Kumteua Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa makubaliano maalumu kuwa atapewa ulaji huo only if atakubali kuitangaza CCM kuwa mshindi wa Urais 2015 hata kama itapata asilimai 10 tu ya Kura (Lubuva Ameshakubali na atafanya hivyo)

Kuruhusu matokeo ya Urais kupelekwa mahakami ili kuja kumnyang'anya Slaa urais kupitia mahakani in case things fall apart and somehow someway CCM looses. So Lubuva Akishindwa kazi Othman Chande atafanya kazi ya kutangaza CCM kuwa mshindi no matter what.(Chande ameshakubali na atafanya hivyo)

Kupanga ugomvi wa CHADEMA na polisi ili watu wauliwe na hivyo kuwatisha watu kuwa CHADEMA ni wagomvi na ikiwezekana kuifuta CHADEMA kupitia kwa Tendwa. (Tendwa amekubali na yuko tayari kufanya hivyo ikibidi)

Na kama haya yote yakishindwa (Yaani Lubuva, Othman na Tendwa) then karata kubwa ya Mwisho ni Zitto Zuberi Kabwe.
Sijui kama yeye anajua hili ila CCM watakuja watamshawishi Zitto Kabwe agombee urais kama mgombea binafsi. Ushawishi huu utafanywa directly na CCM yenyewe na indirectly kwa CCM kuwapa hela rafiki zake Zitto wajerumani ili wajidai wanampsonsor ili agombee Urais kama Mgombea binafsi.

Lengo kuu la CCM katika hili ni kugawanya kura za CHADEMA ili kuishinda. Wanachotaka CCM ni hiki - Zitto akigombea basi Slaa anaweza kupata asilimia 37 za wapiga kura wote Tanzania na Zitto akapata kama asilimia 25 huku CCM ikiambulia kama asilimia 38. Mpaka hapo (Japokuwa CHADEMA itakuwa na asilimia 62) Mgombea wa CCM atakuwa ameshinda (ukichukulia watachakachua kura pia). Hii ni trick ya kudivide kura za CHADEMA na kuwafanya wagombea wote wa CDM wasipate kura za kutosha ilihali angegombea Slaa peke yake angepata asilimia 62. Kama hili litafanikiwa Zitto atakuwa ametumiwa kumnyang'anya Slaa kura huku akiipa CCM ushindi thru this divide and continue to rule trick. Tricky hii huwa inatumiwa sana Marekani na ndio kete ya mwisho ya CCM kuiangusha CDM thru Zitto Zuberi Kabwe.

CHADEMA PLEASE BEWARE OF THIS POWER MONGER YOUNG BOY ZZK! Anatamaa sana mpaka zinam-blind. Haoni chochote anaona sifa binafsi tu. I hope siku moja atakuja ataamka.
 
Naona mnatumia nguvu kubwa sana kumchafua zitto kwakuwa ni threat kwenu,katu njama zenu feki hazitofanikiwa,mmeona kijana kadhamilia kuongoza taifa hili mnaanza kuleta propaganda kwamba endapo akigombea kama mgombea binafsi basi kanunuliwa na ccm kugawa kura za cdm.
Tumewachoka na siasa zenu za majitaka,zitto atagombea by any means,na ndie rais ajae.
Hopeless.
You try to talk about slaa as a contestant of presidential position through chadema at the same time you act like you are not aware that mbowe also has mission to be a contestant of the same position,same year I mean 2015 through the same party!
Hopeless again.
Zitto must win the battle!

mwavuli..punguza mapovu.

Zito ni kiongozi mwenye vision nzuri sana ya hii nchi ielekee wapi. Anachokosa ni ile busara aliyonayo Mbowe, ya kujua ni wakati gani atake uongozi upi..nakuhakikishia Mbowe hana mpango wa kugombea 2015.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania kwa kuchezeana akiri hawajambo. Na hii thread ni katika kuchezeana akiri. Shukurani.

Sasa ntaanza kuingia na bakora ya mzee kifimbo cheza maana mnakera sana vipi kiswahili kiwashinde wakati ndio lugha mama?

Eti akiri.............!!!! Sio akiri ni akili
 
Hii ni hadithi ya kijinga tu isiyo na maana.

Naomba niseme, mimi ni mwanafunzi wa historia. Kamwe siwezi kuifanya historia inihukumu kwa mabaya. Siwezi kuwa sababu ya Taifa letu kushindwa kuandika historia mpya ya kuiondoa madarakani CCM iliyochoka na kutufukarisha. Historia ya maisha yangu imeandikwa kwa harakati za mageuzi na ndio maana sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya CHADEMA. Wakati vijana wasomi wengine walikwenda kutafuta mkate makazini au kwenye vyama vingine vya siasa vilivyokuwa vinang'ara wakati huo, mimi nilijiunga CHADEMA na kushiriki kukijenga mpaka hapa mnapokiona. Siwezi kufuta matumaini ya mabadiliko ya Watanzania.

Napenda ifahamike kuwa CHADEMA haina mgombea Urais wa mwaka 2015. Muda utakapofika taratibu za chama kupata mgombea zitatangazwa na tunaotaka kugombea tutajitokeza au tutaombwa na vikao vya chama.

Yeyote atakayeteuliwa na chama kupeperusha bendera ya chama chetu ndiye atakuwa mgombea wa chama chetu. Mimi binafsi nitamwunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa na chama. Kama CCM wanakuwa kama fisi kusubiri mkono udondoke wasahau. CHADEMA hatutogombana kwa sababu ya Urais. Kwangu mimi Urais sio an End. It is just a means to an end. Malengo haya haya niliyonayo yanaweza kutekelezwa na Rais Mbowe, Rais Mkuumbo, Rais Slaa au hata Rais Lissu. Uwezo na maarifa yangu siku zote nimeyaweka katika kuhakikisha Taifa letu linakuwa bora zaidi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Urais ni dhamana tu ya kufikia malengo hayo.

Mada kama hizi badala ya kujenga chama zinabomoa kwa kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwa viongozi. Mwandishi wa makala haya angetumia akili zake hizi kuandika mradi wa maendeleo ya kijiji ingesaidia sana badala ya kumwaga chuki na kuleta mfarakano.

Yeyote anayedhani kwamba ataivuruga CHADEMA kupitia kwa Zitto aandike maumivu. CHADEMA ni movement. Zitto ni sehemu ndogo sana ya CHADEMA kama ilivyo kwa mwanachma mwingine yeyote. Wengi tulioanza nao hatunao, na wengi tulionao sasa hatukuwa nao.
Hapo mzee umemaliza, kule ccm kuna msemo ccm ina wenyewe, na Chadema pia ina wenyewe, Zito kuondoa kabisa ushabiki wa kijinga, kwenye underline pale, ni kweli mkuu, tuwaulize waliopo humo wametokea wapi, na ni kwa nini, wengi walikuwepo sasa hv wako wapi, na hawa waliokuja wengi wao baada ya kukosa kuteuliwa kugombea ubunge, hebu wasomaji tupapambanue hapo na mtoa mada ajiangalie, kijana simama, chama hiki ni cha watanzania, hakuna mwenye hati milki na hasa hao vibaraka, kwanza Zito jipambanue kuwa umesimama, na endelea kusimama.
 
Mi siamini kama kwa mfumo wa nchi yetu kuna mtu anaweza kugombea binafsi nje ya chama na kupata japo 10% ya kura za urais, kama kweli Zitto au mwengine yeyote atakubari kufanya hivyo atakuwa amejimaliza kisiasa.
 
Mmenisema sana,mmenijadili sana,mmeniteta sana,sasa dec ntaongea na media kama ntagombea kama mgombea binafsi au ntagombea kupiticha chama changu CHADEMA.
 
Dawa ni CDM ikubali kuwa Zitto is a force to reckon yaani ni kijana anakubalika na vijana ni muislamu hivyo anakubalika kwa waislamu na ni msomi hivyo anakubalika kwa middle classs ambapo wakristo wengi wapo. Hivyo ana sifa zote. Binafsi kutokana na negative campaign anayofanyiwa Zitto simpendi lakini huo ndio ukweli. Tujifunze kumsamehe na tumgroom aje kukifaa chama chetu hatuna jinsi.

What a stupid thing to say "he will be accepted by muslims because he his muslim" Do you think or are you suggesting that muslim should support only muslim candidates? I dont whant this to sound like a personal attack to you but if we don't get rid of this mind set this country is not going anywhere forward.
If Zito is to win any office, he will because people trust him and they think he is a good leader and not because of what religion he believes in.

We saw in last years of Second Phase Government, where some people and magazine where defending and protecting the, then president just because he was from their religion, Now it is the same thing where the current President is being defendend by some because of his religion. They are not there for their religion benefits, they just look after their family and friends, unless you are one of them you better start to think different about supporting someone because they are Muslim,Christian or from your region.
 
a well focused leader kwenye mafanikio binafsi... maelezo yako yanathibitisha roumors za ubinafsi wa zzk. halafu viongozi huwa hawaji kwa mtindo sa zzk. maoni yangu.

Umeonyesha jinsi gani una maoni dhaifu.
Hopeless.
Slaa ndie anayewaza mafanikio binafsi kwanza kwakujiidhinishia mshahara wa million saba,pili kuchota ml 140 toka kwenye ruzuku na kwenda kumalizia deni lake la nyumba nayoishi.
Huu si ubinafsi?
Acha kulishwa upepo wewe,na kuishi kwa rumous.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom