Jinsi CCM Itakavyomtumia Zitto Kushinda Urais 2015

Status
Not open for further replies.
Naona mnatumia nguvu kubwa sana kumchafua zitto kwakuwa ni threat kwenu,katu njama zenu feki hazitofanikiwa,mmeona kijana kadhamilia kuongoza taifa hili mnaanza kuleta propaganda kwamba endapo akigombea kama mgombea binafsi basi kanunuliwa na ccm kugawa kura za cdm.
Tumewachoka na siasa zenu za majitaka,zitto atagombea by any means,na ndie rais ajae.
Hopeless.
You try to talk about slaa as a contestant of presidential position through chadema at the same time you act like you are not aware that mbowe also has mission to be a contestant of the same position,same year I mean 2015 through the same party!
Hopeless again.
Zitto must win the battle!

Whether its Slaa au Mbowe mwisho wa siku ZZK atatumika kuwaangusha. Mark my words!
 
Mtoa mada ana upungufu wa akili mwilini. Hebu tumia akili ya kawaida, uchaguzi ufanyike, kura zipigwe, matokeo fake yatangazwe na lubuva, au ikishindikana waende mahakamani kumpora Dr. Slaa ushindi kupitia Othman chande. Ikishindikana wamtumie zitto kuwa mgombea binafsi. Kwa hiyo zitto atagombea baada ya uchaguzi na mbinu za kwanza kufeli? Au kuna chaguzi mbili? Za kuambiwa changanya na yako
 
WABHEJASANA Sasa nimekuelewa kweli ni bongo lala hili jamaa maana hajui kiswahili sijui mmalawi huyo
 
Last edited by a moderator:
Hii ni hadithi ya kijinga tu isiyo na maana.

Naomba niseme, mimi ni mwanafunzi wa historia. Kamwe siwezi kuifanya historia inihukumu kwa mabaya. Siwezi kuwa sababu ya Taifa letu kushindwa kuandika historia mpya ya kuiondoa madarakani CCM iliyochoka na kutufukarisha. Historia ya maisha yangu imeandikwa kwa harakati za mageuzi na ndio maana sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya CHADEMA. Wakati vijana wasomi wengine walikwenda kutafuta mkate makazini au kwenye vyama vingine vya siasa vilivyokuwa vinang'ara wakati huo, mimi nilijiunga CHADEMA na kushiriki kukijenga mpaka hapa mnapokiona. Siwezi kufuta matumaini ya mabadiliko ya Watanzania.

Napenda ifahamike kuwa CHADEMA haina mgombea Urais wa mwaka 2015. Muda utakapofika taratibu za chama kupata mgombea zitatangazwa na tunaotaka kugombea tutajitokeza au tutaombwa na vikao vya chama.

Yeyote atakayeteuliwa na chama kupeperusha bendera ya chama chetu ndiye atakuwa mgombea wa chama chetu. Mimi binafsi nitamwunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa na chama. Kama CCM wanakuwa kama fisi kusubiri mkono udondoke wasahau. CHADEMA hatutogombana kwa sababu ya Urais. Kwangu mimi Urais sio an End. It is just a means to an end. Malengo haya haya niliyonayo yanaweza kutekelezwa na Rais Mbowe, Rais Mkuumbo, Rais Slaa au hata Rais Lissu. Uwezo na maarifa yangu siku zote nimeyaweka katika kuhakikisha Taifa letu linakuwa bora zaidi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Urais ni dhamana tu ya kufikia malengo hayo.

Mada kama hizi badala ya kujenga chama zinabomoa kwa kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwa viongozi. Mwandishi wa makala haya angetumia akili zake hizi kuandika mradi wa maendeleo ya kijiji ingesaidia sana badala ya kumwaga chuki na kuleta mfarakano.

Yeyote anayedhani kwamba ataivuruga CHADEMA kupitia kwa Zitto aandike maumivu. CHADEMA ni movement. Zitto ni sehemu ndogo sana ya CHADEMA kama ilivyo kwa mwanachma mwingine yeyote. Wengi tulioanza nao hatunao, na wengi tulionao sasa hatukuwa nao.

Wewe ni jembe ndio maana watu hawalali juu yako'mbona shibuda hawanyimi usingizi na hawana habari nae? Ila wewe tu faham kuwa wewe ni jembe tena la trekta never give up boy mimi ntakusapoti mpaka mwisho faham hilo
 
I don't agree with with what you, but i will defend to death your right to say it.... Zitto, zitto, Zitto...nadhani ni wakati muafaka sasa kuhamishia nguvu hii tunayopoteza kwenye mambo ya msingi na yenye maslahi kwa nchi yetu
 
Hii ni hadithi ya kijinga tu isiyo na maana.

Naomba niseme, mimi ni mwanafunzi wa historia. Kamwe siwezi kuifanya historia inihukumu kwa mabaya. Siwezi kuwa sababu ya Taifa letu kushindwa kuandika historia mpya ya kuiondoa madarakani CCM iliyochoka na kutufukarisha. Historia ya maisha yangu imeandikwa kwa harakati za mageuzi na ndio maana sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya CHADEMA. Wakati vijana wasomi wengine walikwenda kutafuta mkate makazini au kwenye vyama vingine vya siasa vilivyokuwa vinang'ara wakati huo, mimi nilijiunga CHADEMA na kushiriki kukijenga mpaka hapa mnapokiona. Siwezi kufuta matumaini ya mabadiliko ya Watanzania.

Napenda ifahamike kuwa CHADEMA haina mgombea Urais wa mwaka 2015. Muda utakapofika taratibu za chama kupata mgombea zitatangazwa na tunaotaka kugombea tutajitokeza au tutaombwa na vikao vya chama.

Yeyote atakayeteuliwa na chama kupeperusha bendera ya chama chetu ndiye atakuwa mgombea wa chama chetu. Mimi binafsi nitamwunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa na chama. Kama CCM wanakuwa kama fisi kusubiri mkono udondoke wasahau. CHADEMA hatutogombana kwa sababu ya Urais. Kwangu mimi Urais sio an End. It is just a means to an end. Malengo haya haya niliyonayo yanaweza kutekelezwa na Rais Mbowe, Rais Mkuumbo, Rais Slaa au hata Rais Lissu. Uwezo na maarifa yangu siku zote nimeyaweka katika kuhakikisha Taifa letu linakuwa bora zaidi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Urais ni dhamana tu ya kufikia malengo hayo.

Mada kama hizi badala ya kujenga chama zinabomoa kwa kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwa viongozi. Mwandishi wa makala haya angetumia akili zake hizi kuandika mradi wa maendeleo ya kijiji ingesaidia sana badala ya kumwaga chuki na kuleta mfarakano.

Yeyote anayedhani kwamba ataivuruga CHADEMA kupitia kwa Zitto aandike maumivu. CHADEMA ni movement. Zitto ni sehemu ndogo sana ya CHADEMA kama ilivyo kwa mwanachma mwingine yeyote. Wengi tulioanza nao hatunao, na wengi tulionao sasa hatukuwa nao.
Zitto,
All I can say is: this is inspiring.
 
Zitto Nashukuru kuwa Mheshimiwa Mbunge Zitto Zuberi Kabwe umekejua mwenyewe kujibu hii hoja. Na hili ndio hitimisho la hii mada. Na kwahakika mada hii imetimiza malengo.

Kwakuja hapa na kujibu hii hoja Zitto ameonyesha kuwa anasikiliza maoni ya wananchi na anayajali. He is one of us and he is amongst us-ni mwenzetu. Na kikubwa zaidi ni kwamba inaonyesha kuwa japokuwa jambo hili ni gumu kwake lakini Ndugu Zitto anajitahidi kwa nguvu sana kuwa muelewa, kujaribu kusoma alama za nyakati na matakwa ya wengi na kwamba yeye ni msikivu na mwenye busara.

This is what i really wanted out of this thread- CCM ni manyang'au na wazandiki na ni muhimu kuwaelewa, kuwang'amua na kujiandaa kukabiliana na unyang'au na uzandiki wao. Suala la kumshawishi Zitto aje kugombea na kugawanya kura in the future ndio lengo kuu la CCM kuruhusu mgombea binafsi (na pia kumruhusu Lowassa kugombea mambo yakiwa magumu NEC) kwa hivyo nimefurahi kwamba kila mtu (akiwemo Zitto) amepata ujumbe juu ya njama hizi za CCM na sasa we are in the same page katika harakati za kujiandaa kushinda kila njama ya CCM na kuipa CHADEMA ushindi.

Nafurahi kuwa Zitto amekuja na kuandika mwenyewe hapa (for the record) kuwa ataheshimu maamuzi ya chama na kumsupport yoyote atakayechaguliwa na chama (hata kama ni yeye mwenyewe). Nimeanzisha dialoge hii ili tuweze kusemezana na kutafakari pamoja jinsi ya kuendeleza mapambano zidi ya Marehemu CCM. Na nnafurahi kuwa hilo limefanikiwa bila kutukanana wala kudhihakiana.

Aksanteni sana wote kwa michango yenu. Tumesemezana, tumetafakari pamoja, tumebadilishana mawazo na tumejifunza pamoja leo tarehe 22 September, 2012. Mimi nimejifunza, wewe umejifunza, Zitto amejifunza, pamoja tumejifunza jinsi ya kukabili kila njama ya CCM na jinsi ya kuihakikishia CHADEMA ushindi mwaka 2015. Hakika CHADEMA ni chama kilichokomaa! Kidumu Chama Cha CHADEMA.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kuwa Mheshimiwa Mbunge Zitto Zuberi Kabwe umekejua mwenyewe kujibu hii hoja. Na hili ndio hitimisho la hii mada. Na kwahakika mada hii imetimiza malengo.

Nafurahi kuwa Zitto amekuja na kuandika mwenyewe hapa (for the record) kuwa ataheshimu maamuzi ya chama na kumsupport yoyote atakayechaguliwa na chama (hata kama ni yeye mwenyewe). Nimeanzisha dialoge hii ili tuweze kusemezana na kutafakari pamoja jinsi ya kuendeleza mapambano zidi ya Marehemu CCM. Na nnafurahi kuwa hilo limefanikiwa.

Aksanteni sana wote kwa michango yenu. Tumesemezana, tumetafakari pamoja, tumebadilishana mawazo na tumejifunza pamoja leo tarehe 22 September, 2012. Mimi nimejifunza, wewe umejifunza, Zitto amejifunza, pamoja tumejifunza jisni ya kukabili kila njama ya CCM na jinsi ya kuihakikishia CHADEMA ushindi mwaka 2015. Hakika CHADEMA ni chama kilichokomaa! Kidumu Chama Cha CHADEMA.

Kigeugeu
 
Kwanza nani kakwambia dr slaa atagombea chadema?kaa usubili uongozi wa chadema ufanye uteuzi wa nani agombe kiti cha urahisi acha porojao,lazima ccm waondoke madarakani

CHADEMA mtaishia kunawa tu, hivi mnafikiria kuwa watanzania wako tayari kuongozwa na wazushi, waongo na wazandiki kama CHADEMA? Mnajidanganya tu. Halafu siyo kwamba nyie wan CHADEMA mko above the average katika kufikiria. Mawazo yenu mengi yapo superficial na mmejawa na rhetoric sana kuliko realism. Kazi mnayo
 
Hii ni hadithi ya kijinga tu isiyo na maana.Naomba niseme, mimi ni mwanafunzi wa historia. Kamwe siwezi kuifanya historia inihukumu kwa mabaya. Siwezi kuwa sababu ya Taifa letu kushindwa kuandika historia mpya ya kuiondoa madarakani CCM iliyochoka na kutufukarisha. Historia ya maisha yangu imeandikwa kwa harakati za mageuzi na ndio maana sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya CHADEMA. Wakati vijana wasomi wengine walikwenda kutafuta mkate makazini au kwenye vyama vingine @@@@@ BIG UP ZANA ZA KILIMO. BAAMBILE BAKAE BAKIJUA MU KICHWA. historia ya nchi hii ni ndefu mdogo wangu. waloanzisha vuguvugu la kudai uhuru ni alina DOSSA,SKAY na wengi lkn mwisho wa siku kwa umoja wao wote wakakubaliana kumwita mwalimu toka pugu bila kujali dini wala upwani.wao walicchoshwa na kutawaliwa basi. swala la NYERERE katokea wapi ana dini gani haikua ajenda yao wazee wetu hao. sasa iweje leo tujadili UNYERERE ili hali zimwi linlotutafuna hatujaliondoa???? Nawaomba ndugu zangu tupeane mbinu za kuliondoa hili dudu ambalo sote limetuchosha.wamarekani walitupatia funzo. walichoshwa na utawala wa vita wa BUSH wakamua kwamba democrat hata wakiteua jiwe watalichagua.WAKUU TATIZO LETU SIIO ZITO WALA MBOWE AU SLAA. TATIZO LETU LILILO MBELE YETU NI CCM BHAAAAAAASIIIII
 
Umejuaje mgombea wa CHADEMA atakuwa Slaa? au Zitto? Au yoyote? Acheni uchonganishi wenu nyie vibaraka wa magamba! CHADEMA haijapitisha mgombea wake bado, subirini acheni kiwewe!

well said! Kwani nimeshagundua kuwa magamba wana2mia kila njia kumchonganisha Zitto na CDM ili tusimuamini na tumuone as a stranger kitu ambacho hakikubaliki, Kama Zitto alishafanya makosa huko nyuma lakini sio kigezo cha kumchafua daily mitandaoni na binafsi na mimi muda fulani nilitaka kuamini kuwa Zitto hafai kabisa lakini sasa nasema tuachieni Zitto wetu na CHADEMA yetu tukalikomboe taifa letu.
 
Hiyo itakuwa "possible" tu kama katiba ya sasa itaendelea kutumika. Kama katiba mpya itataja mshindi wa urais kupata zaidi ya aslimia hamsini badala ya sasa ya "smple majority" haitawezekana mtu mmoja kugawa kura za washindani wakuu kwenye kinyang'anyiro.
 
Well said Mh. ZZK n wakati wakujenga CHADEMA wakat wa urais ukifika ndio 2jadili hayo

I hope muda utahapofika, na shetani akapata nguvu hatakuja na kauli ya namna hii "CHADEMA sio mama wala baba"; I just hope!
 
Hii ni hadithi ya kijinga tu isiyo na maana.

Naomba niseme, mimi ni mwanafunzi wa historia. Kamwe siwezi kuifanya historia inihukumu kwa mabaya. Siwezi kuwa sababu ya Taifa letu kushindwa kuandika historia mpya ya kuiondoa madarakani CCM iliyochoka na kutufukarisha. Historia ya maisha yangu imeandikwa kwa harakati za mageuzi na ndio maana sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya CHADEMA. Wakati vijana wasomi wengine walikwenda kutafuta mkate makazini au kwenye vyama vingine vya siasa vilivyokuwa vinang'ara wakati huo, mimi nilijiunga CHADEMA na kushiriki kukijenga mpaka hapa mnapokiona. Siwezi kufuta matumaini ya mabadiliko ya Watanzania.

Napenda ifahamike kuwa CHADEMA haina mgombea Urais wa mwaka 2015. Muda utakapofika taratibu za chama kupata mgombea zitatangazwa na tunaotaka kugombea tutajitokeza au tutaombwa na vikao vya chama.

Yeyote atakayeteuliwa na chama kupeperusha bendera ya chama chetu ndiye atakuwa mgombea wa chama chetu. Mimi binafsi nitamwunga mkono mgombea yeyote atakayepitishwa na chama. Kama CCM wanakuwa kama fisi kusubiri mkono udondoke wasahau. CHADEMA hatutogombana kwa sababu ya Urais. Kwangu mimi Urais sio an End. It is just a means to an end. Malengo haya haya niliyonayo yanaweza kutekelezwa na Rais Mbowe, Rais Mkuumbo, Rais Slaa au hata Rais Lissu. Uwezo na maarifa yangu siku zote nimeyaweka katika kuhakikisha Taifa letu linakuwa bora zaidi kiuchumi, kijamii na kisiasa. Urais ni dhamana tu ya kufikia malengo hayo.

Mada kama hizi badala ya kujenga chama zinabomoa kwa( kupandikiza mbegu za chuki )miongoni mwa viongozi. Mwandishi wa makala haya angetumia akili zake hizi kuandika mradi wa maendeleo ya kijiji ingesaidia sana badala ya kumwaga chuki na kuleta mfarakano.

Yeyote anayedhani kwamba ataivuruga CHADEMA kupitia kwa Zitto aandike maumivu. CHADEMA ni movement. Zitto ni sehemu ndogo sana ya CHADEMA kama ilivyo kwa mwanachma mwingine yeyote. Wengi tulioanza nao hatunao, na wengi tulionao sasa hatukuwa nao.

Maneno haya ya busara yanatosha kabisa kuwamaliza wale wote wana kaa na kuota. huu ujumbe umewafikia vyema na wameupata wale wote wachonganishi hasa ccmweli.

yan mh zitto tunashukuru umewambia ccmweli waziwazi nadhani sasa wataondokana na hii ndoto na watatafuta wimbo mpya wakuja nao maana huu umewashinda sasa. na kamwe hawataweza.

Nadhani sasa ccmweli mmeishiwa cha kusema.
 
Nashukuru kuwa Mheshimiwa Mbunge Zitto Zuberi Kabwe umekejua mwenyewe kujibu hii hoja. Na hili ndio hitimisho la hii mada. Na kwahakika mada hii imetimiza malengo.

Kwakuja hapa na kujibu hii hoja Zitto ameonyesha kuwa anasikiliza maoni ya wananchi na anayajali. He is one of us and he is amongst us-ni mwenzetu. Na kikubwa zaidi ni kwamba inaonyesha kuwa japokuwa jambo hili ni gumu kwake lakini Ndugu Zitto anajitahidi kwa nguvu sana kuwa muelewa, kujaribu kusoma alama za nyakati na matakwa ya wengi na kwamba yeye ni msikivu na mwenye busara.

This is what i really wanted out of this thread- CCM ni manyang'au na wazandiki na ni muhimu kuwaelewa, kuwang'amua na kujiandaa kukabiliana na unyang'au na uzandiki wao. Suala la kumshawishi Zitto aje kugombea na kugawanya kura in the future ndio lengo kuu la CCM kuruhusu mgombea binafsi (na pia kumruhusu Lowassa kugombea mambo yakiwa magumu NEC) kwa hivyo nimefurahi kwamba kila mtu (akiwemo Zitto) amepata ujumbe juu ya njama hizi za CCM na sasa we are in the same page katika harakati za kujiandaa kushinda kila njama ya CCM na kuipa CHADEMA ushindi.

Nafurahi kuwa Zitto amekuja na kuandika mwenyewe hapa (for the record) kuwa ataheshimu maamuzi ya chama na kumsupport yoyote atakayechaguliwa na chama (hata kama ni yeye mwenyewe). Nimeanzisha dialoge hii ili tuweze kusemezana na kutafakari pamoja jinsi ya kuendeleza mapambano zidi ya Marehemu CCM. Na nnafurahi kuwa hilo limefanikiwa bila kutukanana wala kudhihakiana.

Aksanteni sana wote kwa michango yenu. Tumesemezana, tumetafakari pamoja, tumebadilishana mawazo na tumejifunza pamoja leo tarehe 22 September, 2012. Mimi nimejifunza, wewe umejifunza, Zitto amejifunza, pamoja tumejifunza jinsi ya kukabili kila njama ya CCM na jinsi ya kuihakikishia CHADEMA ushindi mwaka 2015. Hakika CHADEMA ni chama kilichokomaa! Kidumu Chama Cha CHADEMA.

mkuu mada kama hizi pia hazijengi bali wakati mwingine zina bomoa chama!
 
Huwa sitii neno lolote ZZK anapobezwa humu,najua na naamini hawezi kuleta hujuma za popo.
Zitto anamengi ya kutiwa moyo kuliko matusi atukwanayo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom