Jini hili jini gani?

mapango

Member
Nov 3, 2010
88
0
kama hili hulioni, macho yako yana kutu
meliona mie jini, langamiza wetu watu
zaidi ya subiani, kiziwi kupewa tutu
jini hili jini gani, chano chake damu zetu?
 
Jini hilo nimeliona, linaua bila huruma
Halijali maamuma, wala imamu
Jini hilo bwana, linatisha kama b52
Jini hilo ni ...........
 
Mbona mekaa kimya, au jini mwamogopa?
hata kama hana haya, vidonge vyake tampa
mie sioni vibaya, kwa mola wangu naapa
dawa ya baya ubaya, si museme hapa hapa!
 
Huyu Mtunzi kwanini Habari za Majini hakuwauliza wale wanaoyafuga na kusali nayo.????
 
Huyu Mtunzi kwanini Habari za Majini hakuwauliza wale wanaoyafuga na kusali nayo.????

Hili ni jukwaa la lugha, wee kama sio mtaalam wa lugha kaa kimya, huna haja ya kuchangia. Hapa imetumika lugha ya picha na hilo jini lililotajwa humo sio jini unalolifikiria wee. Unayotaka kuyaleta ktk jukwaa hili wala hayastahili.
 
Jini limekuwa gumzo bara na visiwani
Jini linanyonya damu na kuweka gizani
Jini hili twalijua na tutaliweka kiganjani
Jini hili si maimuna wala shubiani
Jini lenyewe jeupe kama "Muirani"
Jini limeng'angani halisikii la muadhini
Jini halikubali linataka kutulisha majani
Jini lina kibri, kushanda mumiani
Jini limejikita uraini mpaka bungeni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom