Jina linalofaa kwa wanandoa

Ambassador

JF-Expert Member
Jun 2, 2008
933
75
Ni kawaida kwa wapenzi kuitana majina matamu matamu kama sweetie, honey, sugar, darling, etc. Mapenzi yakikolea na wapenzi kufikia hatua ya uchumba mbwembwe huongezeka. Kwa wengi wetu baada ya ndoa majina haya hubadilika kadiri muda unavyokwenda na matukio kubadili hali ya ndoa. Mfano baadhi huanza kuitana 'mme wangu' au 'mke wangu'. Wengine hutana Mr au Mrs. Baada ya kupata watoto majina ya mama fulani, sijui baba Mwamini (Lalingeni upo?) hushamiri.

Kuna rafiki yangu mmoja amegoma kabisa kuitwa jina la baba fulani na kudai kwamba yeye ana jina lake na mkewe amuite hilo. Hata yeye binafsi humuita mkewe kwa jina lake la kwanza licha ya kuwa wana watoto watatu sasa. Rafiki yangu mwingine alikuwa anaitana 'shemeji' na mkewe mpaka mtoto akawa anawaita shemeji!

Kuna madhara yoyote kumuita mkeo au mmeo kwa jina lake la kwanza mbele za watu hususan watoto wenu? Je jina lipi linafaa kumuita mmeo au mkeo naye ajifeel vizuri?
 
Kuna rafiki yangu mmoja amegoma kabisa kuitwa jina la baba fulani na kudai kwamba yeye ana jina lake na mkewe amuite hilo. Hata yeye binafsi humuita mkewe kwa jina lake la kwanza licha ya kuwa wana watoto watatu sasa.

Hii ni nzuri.
 
Inategemeana mkeo au wewe unataka kuitwaje, kinachotakiwa usiige kuita jina fulani eti kwa sababu wanandoa wengine wanaitana. Mfano mimi mke wangu ananiita Dear lakini mimi huwa napenda kumuita jina lake kwa kuwa nafikiri dear ni common mno.

Kama mdau hapo juu alivyosema, kuna rafiki yangu mmoja wanaitana "Wife" and "Husband" kitu ambacho mimi naona kama ni utani haipnyeshi u-serious. Hivyo jamani nafikiri kuhusu majina ndani ya ndoa inategemeana na nyie wenyewe.
 
lile jina, majina mloitana uchumbani ndo yaendelee mpaka mwisho
kama mmeshazoea kuitana dear, honey, sweetie etc mkishakua na watoto kwakweli inakua sio hishma kuitana majina hayo mbele yao!, its better mkaitana we baba wawil, mama kidume etc.
binafsi hadi niko darasa la saba nilikua sijui jina la kwanza la mama yangu mzazi wala la baba yangu!!!, hadi siku nakumbuka tuliambiwa tupeleke kopi ya cheti cha kuzaliwa ndio nikaliona.
watoto wa siku hizi hawana adabu,, hamkawii kuitana majina yenu ya kwanza ukashangaa na mtoto wako nae siku anakuita jina hilo!!.
 
mie aniite tu jina langu " Kalunde linatosha " sasa mama Misoji mala mama Shilinde wapi na wapi ;)
 
mie aniite tu jina langu " Kalunde linatosha " sasa mama Misoji mala mama Shilinde wapi na wapi ;)

Hata mimi huwa naona inapunguza hata vionjo vya mapenzi. Mambo ya kuitana baba fulani au mama fulani waachieni majirani wawaite hivyo.....Nyie wenyewe mkiitana hivyo ni kama vile mnazeeshana mapema! :)
 
Ambassodor, mi nitapenda kumuita tu jina lake kama ni "macho" basi ndio hivyo hivyo ingawa wamama wengi wakishajaliwa mtoto/watoto hupendelea kuitwa kwa majina ya watoto. Kwangu mimi sina noma kabisa...aniite jina langu tu "Kimature" life goes on. Maana kiukweli suala la mapenzi siwezi kuamini kuwa kiwango mlichokuwa mkipendana mlipokuwa boy/girl friend hadi uchumba kitakuwa ni kile kile hata baada ya miaka 10 ya ndoa, si kweli..
 
kama mmeshazoea kuitana dear, honey, sweetie etc mkishakua na watoto kwakweli inakua sio hishma kuitana majina hayo mbele yao!, its better mkaitana we baba wawil, mama kidume etc.
binafsi hadi niko darasa la saba nilikua sijui jina la kwanza la mama yangu mzazi wala la baba yangu!!!, hadi siku nakumbuka tuliambiwa tupeleke kopi ya cheti cha kuzaliwa ndio nikaliona.
watoto wa siku hizi hawana adabu,, hamkawii kuitana majina yenu ya kwanza ukashangaa na mtoto wako nae siku anakuita jina hilo!!.

Mpwa iyo kali!!!

kuna rafiki yangu wao ktk familia walilelewa kiuzungu siju niseme mpaka tupo chuo mwaka wa kwanza baba anaitwa jina lake 'Daudi' na mama 'Becky'....kwa vile wakati wotw wazazi wao walikuwa wakiitana majina yao nao wakazoea hivo hata wakiwanunulia any greeting cards they wrote that.

I prefer kuitwa jina langu na mi nimwite lake!!!
 
mpwa iyo kali!!!

Kuna rafiki yangu wao ktk familia walilelewa kiuzungu siju niseme mpaka tupo chuo mwaka wa kwanza baba anaitwa jina lake 'daudi' na mama 'becky'....kwa vile wakati wotw wazazi wao walikuwa wakiitana majina yao nao wakazoea hivo hata wakiwanunulia any greeting cards they wrote that.

i prefer kuitwa jina langu na mi nimwite lake!!!
mnhh, umeona sasa hapo??
 
Back
Top Bottom