Jina la Said Nassor Bagaile ndiye Hamis Andrea Kigwangalla?

Mbona hata yule mgombea wa jimbo la kigamboni ana uraia wa S. Africa lakini amepitishwa na chama? Alikimbia nchini baada ya kutumikia kifungo kwa muda, kisha akaona akakae mafichoni huko Kusini mwa africa, ila CCM wakimtaka mtu, ndiyo atakuwa, Bashe yeye mwenyewe anafahamu nini kina msibu, ajaribu kupambana kivyengine, c kupitia chaguzi za chama chake

Hapa umesema uongo wa waziwazi. Huyo mgombea wa CCM Kigamboni namfahamu binafsi, anaitwa Faustine Ndugulile, daktari bingwa. Huyu namfahamu sana na ndiye mgombea pekee huko CCM ninayemfahamu kiasi hicho kutokana na kufahamiana sana na mdogo wake na kuzoea nyumbani kwao tangu mdogo. Huyu ni mtanzania, mnyamwezi wa Tabora. Familia yao waliwahi kuishi Zimbabwe zamani ambako wazazi wake walifanya kazi. Hajawahi kutumikia kifungo chochote, uongo mtupu huu. Tena aliwahi kuwa mkurugenzi wa masuala ya udaktari wizara ya afya makao makuu, na mke wake ni profesa pale Muhimbili. Huko South Africa alikwenda kufanya kazi ya UN na wala hajatimka kama unavyodai. Usipende kukurupukia usiyoyajua.

Mimi siipendi CCM hata kidogo na wala sitaipigia kura, lakini siwezi kuvumilia mtu anapomtungia uongo hivi jamaa ninayemfahamu, haifai hata kidogo.
 
Sasa hayo ndio madudu ya CCM

Wao tatizo lao ni kuletewa habari na sio kutafuta au kuchunguza, walisema ati maaamuzi yalikuja wakati muda ni mdogo ulikuwa umebakia hii ni kutoka kwa propaganda wa CCM jana alihojiwa na chombo kimoja cha habari,

Sasa swali kama walikuwa hawana muda wa kujadili swala la urai wa bashe au kukaa na uhamiaji na kuchunguza swala hilo kwa umakinifu kabla ya kutoa uamuzi kwa kumpa mtu mwingine jimbo ndio wameoni ni sahii kwa maaamuzi hayo?
Mbona leo NEC yaenda kaaa kikao cha mwisho kuridhia majina ya wagombea nini maana yake? au ni ubabaishaji tuuu hapa?

Na haya maaamuzi ya kuamua haraka haraka na badara ya kumpa Selelii wao waka rukia kwa mshindi wa 3 wakizani wanamwangamiza seleliii kumbe wanajitosa kwa kaaa la moto jamani focus ya viongozi wetu wa CCM wamekalia siasa sana fitna majungu kuliko uchapakazi

Na kwa aibu zao watang'ang'ania kumpa huyo jamaaa ubunge ili wasijione wababaishaji lakini ukweli ni kwamba hatuelewi lipi ni la ukweli
 
Nimesikia katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa Dr. Hamis Kigwangale ni Mrundi na Jana amehojiwa zaidi ya Saa moja na maofisa uhamiaji na kujulikana hata jina analotumia ni la kufoji

Yaani kama ni mpira ndio kwanza kipindi cha kwanza tena sekunde ya kwanza tu mashambulizi makali yanapelekwa golini, sijui ngoja tusubiri matokeo tuone but i doubt utasikia yuko cleared kuwa ni mtanzania let wait and see
 
Ngoshwe,
Mama yake Hussein ni Mtanzania, maadam bashe alizaliwa Tanzania na kalelewa, kakulia na kusoma Tanzania na wazazi wake wote wawili, ingawa kwa muda wote huo baba yake hakuomba Uraia hadi kufikia miaka 10 ya Bashe..Kutokana na maisha yake yeye Bashe na sio mzazi wake haiwezekani asiwe raia wa nchi hii kwa sababu tu baba yake hakuomba Uraia.. muhimu ni kwamba waliishi kisheria na kukubaliwa kuendelea kuishi nchini inatosha.

Na nimesema wazi kuwa wapo mashombe kibao Tanzania ambao baba zao hawakuomba Uraia wala hawakuwa na haja ya kufanya hivyo, tena basi wameondoka nchini na kurudi makwao wakiwaacha watoto na mama zao. Hawa watoto waliozaliwa nchini na kukulia hapa ni Watanzania na nakuhakikishia kwamba hawahesabiwi na serikali za huko nchi za baba zao kama ni raia wa nchi hizo.

Kisheria sijui za Bongo, mtu yeyote aliyekwisha fikia zaidi ya miaka 18, huyu huitwa mtu mzima na mwenye uraia wake pasipo kutegemea tena wazazi wake. Maadam Bashe amekulia Tanzania na kaweza kupata pasi ya kibongo na sio ya Somalia, huyu ni Mbongo tu. Kinyume cha hapo hizi ni njama ambazo kusema kweli hazina nafasi kabisa. Kama mweli sio raia na muda wote kadanganya uraia wake nadhani jibu lrahisi ni kumpa masaa 24 aondoke nchini maanake kisha vunja sheria ya Uhamiaji.

Mbona wapo watu (Watanzania) wenye asili ya Tanzania - baba zao Watanzania, mama zao watanzania lakini sheria yetu inawaita ati sio Watanzania kwa sababu tu wanaishi nje?..kwa hiyo uraia wa baba sio sababu kabisa ya kumbagua mtu uraia wake..

Chiligati kwa kauli yake alisema Wazazi wote wawili ni wasomali. Je kuna anayemfahamu Mama wa huyu Hussein? Leta data.
 
mnakumbuka ahadi za tanu kwamba watanzania wote ni ndugu na afrika ni moja pia baba wa taifa alisisitiza kwamba hatuwataki wakabila wala makaburu na kwamba makaburu wa afrika kusini hawakupingwa kwa sababu ya rangi yao bali kwa matendo yao. kwa kuwa ccm wameanza dhambi ya ubaguzi naomba iendelee kuwatafuna ila mungu anisamehe:becky:
 
Me nafikiri tunaumiza vichwa sana katika suala hili la Bashe na kunyang'anywa nafasi yake kwa kisingizio cha uraia.. Ninachoamini mimi hapa kuna sababu za msingi ambazo Makamba na wenzake wanazijua na kupelekea kutoa jeuri juu ya uraia wa Bashe.. si dhani kama ni suala la uraia tu , nahisi kuna zaidi ya hilo.. na watu watajadili weeee mpaka watachoka ukweli hautapatikana hapa.. kama ni uraia kwanini sasa wasimpe Selelii mpaka waruke namba tatu? .....Hiyo ndio CCM bwana, ikimtaka mtu itamweka kiulainiiiii na isipomtaka itamtupa mbali tu...
Ukitaka kuamini haya ona idara zinatakiwa kutoa ufafanuzi zinavyopigiana mpira, mara niko mbali , mara nipeni muda kidogo, huyo wa uhamiaji anasubiri kuongea nini na Masha wakati ofisi yake ina document zote? hali kadhalika na masha amekana kuongelea chochote mpaka awasiliane na wakubwa... wakubwa gani? si anasubiri amri tu ya Kikwete na makamba???
Hii tanzania itafikia mahali lazima tumwage damu tu ndo heshima itapatikana.
 
Hussein Bashe ni mtu wa RA na EL. Seleli ni Msumali kwa EL na RA. Kwa hiyo Kuogopa RA na EL ambao CCM hawawezi kuwagusa kwa Vile wanajua Mengi ya Uozo nadani ta Uongozi wa Juu wa CCM; NEC walipomteua huyo Namba tatu walidhani atakuwa compromise candidate. Sasa Tusubiri ya Uraia wa Huyo Dr. Leta Data zaidi waungwana.
 
nilipokuwa milambo sec.pale tabora nilikuwa nikisika jina la dk kigwangwala kama mtaalamu wa tiba za asili na mmliki wa kingwangali herbalist clinic je ndiye huyu aliyegombea nzega? wenye data naombeeni
 
Nimesikia katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa Dr. Hamis Kigwangale ni Mrundi na Jana amehojiwa zaidi ya Saa moja na maofisa uhamiaji na kujulikana hata jina analotumia ni la kufoji
Mwenye uhakika na uraia wake nchi hii ni Idi Simba pekee maana mahakama ya rufaa ilithibitisha............tunaobaki wote akiwemo Makamba hatuna uhakika na ndiyo maana kesi za aina hii zinatokea mara kwa mara................ Hakuna atakeyemsumbua Idi Simba juu ya uraia wake.............. Lafudhi siyo tiketi ya uraia......hata kama unaongea kiswahili cha kisambaa ................bado.........
 
mgombealeo.jpg


Huyu naye ni Mrundi CCM kweli Kiboko, kwa vile ni chaguo lao utamsikia Makamba akisema, ni kweli vielelezo vinaonyesha si raia lakini mimi nasema ni raia uhamiaji hawajui kazi, kaaaazi kweli kweli.

Hebu jamani angalieni pua yake anaonekana mtusi au mhutu.
 
Boniface Meena,Gazeti la Mwananchi;August 18/2010

SUALA la uraia limezidi kuwa mwiba mchungu kwa CCM baada ya mgombea aliyepitishwa na halmashauri kuu ya chama hicho kuwania ubunge wa jimbo la Nzega, Dk Hamis Andrea Kigwangala kukamatwa na maofisa wa idara ya uhamiaji na kuhojiwa dhidi ya tuhuma kuwa ni raia wa Burundi.
Dk Kigwangala, ambaye alizua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya mawasiliano ya kompyuta baada ya kutangaza nia ya kuwania jimbo hilo, alishika nafasi ya tatu kwenye kura za maoni za jimbo la Nzega, lakini akapitishwa kuwania kiti hicho baada ya mshindi wa kura za maoni, Hussein Bashe kudaiwa kuwa ni Msomali huku mshindi wa pili, Lucas Selelii akidaiwa kuwa amepoteza mvuto.

Lakini wakati akiwa kwenye maandalizi ya mikikimikiki ya ubunge, Dk Kigwangala alijikuta akitakiwa amalizane kwanza na tatizo la uraia wake, ikiwa siku mbili kabla ya siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu kwenye Tume ya Uchaguzi (Nec).

Mbali na uraia, mtaalamu huyo wa afya ya jamii pia anadaiwa kuwa hatumii jina halisi na kwamba jina lake ni Said Bagaile ambaye alimaliza elimu yake ya msingi mwaka 1990 kwenye Shule ya Msingi ya Kitongo iliyo wilayani Nzega.

Habari zinasema kuwa maofisa wa Idara ya Uhamiaji walimchukua Kigwangala kwenye ofisi za CCM wilayani Nzega ambako alikuwa akisaka udhamini kabla ya kwenda kuchukua fomu na kurejesha tayari kwa pilikapilika za kugombea ubunge.

Huku tuhuma za kufanyiana njama kwa kutumia uraia na umri zikizidi kushamiri ndani ya CCM, Dk Kigwangala hakuwa mbali na hisia hizo wakati alipohojiwa na Mwananchi kuhusu uraia wake.

"Hizo ni fitina za Bashe ili anichafue kwa kuwa tayari ana matatizo ya uraia," alisema Dk Kigwangala alipoongea na Mwananchi kwa njia ya simu jana.

"Ni kweli nimehojiwa na Uhamiaji kuhusu uraia wangu... mimi ni mzaliwa wa Tabora na sijawahi kufika wala kukanyaga ardhi ya Burundi.

"Mpaka hivi sasa ninavyoongea na wewe nahojiwa na nimetoa nyaraka zangu zote kuthibitisha kuwa mimi ni Mtanzania halisi na zinafanyiwa uchunguzi."

Alisema kuwa uhamiaji wanaendelea na uchunguzi wa taarifa zake na kwa kuwa fitina hizo zinafanywa na Bashe atamshtaki kutokana na kumchafua.
"Bashe ananichafulia na nitamshitaki kwa kufanya haya ambayo yananichafulia jina langu," alisema Dk Kigwangala.

Alisema kuwa jina lake kamili ni Hamis Kigwangala na amekuwa akilitumia siku zote tangu akiwa shuleni.

Alipotafutwa kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na Dk Kigwangala kuwa ndiye anayemchafua, Bashe hakupatikana.

Wakati Dk Kigwangalla akijitetea kuhusu urai wake, sakata la jina limeibukia kwenye chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi ambako mwenyekiti wake, James Mbatia ameeleza kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho kwenye jimbo la Nzega anaitwa Hamis Andrew.

Mbatia alidai kuwa Dk Kigwangala alikuwa akitumia jina la Hamis Andrea ili aendelee na elimu na kwamba jina lake halisi ni Said Nassor Bagaile.

Mbatia alidai kuwa Kigwangala alichukua jina la Hamisi Andreaw Kigwangala baada ya kutopata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari wakati Hamisi Andrew alikuwa amefaulu na hivyo kukubaliana atumie jina hilo.

Mgombea huyo wa NCCR-Mageuzi anatarajiwa kuchukua fomu kupambana na Dk Kigwangala.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Florence Horombe hakuweza kupatikana kuzungumzia taarifa hizo za kukamatwa kwa mmoja wa wagombea wa ubunge wilayani kwake.

Taarifa tulizopatikana jana usiku zilisema kwamba Kigwangala alienda juzi Mahakama ya Wilaya Nzega kula kiapo kwa jina hilo lenye utata. Habari zaidi zinasema maofisa wa Uhamiaji walimwita Dk Kigwangala juzi kwa ajili ya mahojiano, lakini hakutokea na ndipo walipoomba polisi kumkamata wakati akitafuta wadhamini kwenye ofisi ya chama.

Chanzo cha habari kutoka Nzega kinasema kwamba Dk Kigwangala aliruhusiwa jioni kwenda kufuturu na baadaye alitakiwa kurejea ofisi za Uhamiaji kwa mahojiano.

Hii si mara ya kwanza kwa wanachama wa CCM kujikuta kwenye tuhuma za kutokana uraia wao wa zamani, hasa inapofikia wakati wa uchaguzi.
Akiwa mbunge wa Ilala kati ya mwaka 200-2005, waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Idd Simba alijikuta akifurumushiwa tuhuma kwamba si raia wa Tanzania wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo.

Simba alituhumiwa kuwa ni raia wa Burundi, lakini baadaye mahakama ilithibitishiwa na hati kutoka nchini Burundi kuwa mbunge huyo wa zamani ni raia wa Tanzania.

Mbunge wa zamani wa CCM wa jimbo la Kigoma Mjini, Azim Premji pia aliwahi kuvuliwa ubunge kwa tuhuma za kutokuwa raia wa Tanzania.
 
Mbatia alidai kuwa Kigwangala alichukua jina la Hamisi Andreaw Kigwangala baada ya kutopata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari wakati Hamisi Andrew alikuwa amefaulu na hivyo kukubaliana atumie jina hilo

Makubaliano HALALI!
 
Me nachooka kweli kweli na mambo ya CCM...lol.. lazima nimpigie Slaa apate asipate shauri yangu
 
Mimi nadhani kwanza mwanzilishi wa mada hii amekosea kujibandika mamlaka ya uhamiaji kusema kuwa Dr. Kigwangalla ni Mrundi, katika siasa lolote linawezekana na je mleta mada huyu atasemaje uhamiaji wakimhoji na baadaye kugundua kuwa ni raia???

Kwa taarifa yako wewe mwenyewe ninaweza leo kwenda kushitaki uhamiaji kuwa wewe siyo raia na ukahojiwa, ni pale tu uhamiaji watakapogundua kweli wewe siyo raia ndipo watakutafutia uraia. Tanzania hii yote ni ya wakimbizi, kuna warundi, wapo wasauzi (wangoni), wahabeshi(wakondoa,etc). Pia kuna wakimbizi wengi tu kutoka rwanda/burundi waliokimbia kwao miaka ya 60 ambao walishapatiwa urai.

Binafsi naichukia CCM lakini nadhani Dr.Kingwala ni baadhi ya vijana ambao tunawahitaji katika siasa zetu.
 
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo (tarehe 18/08/2010) mteule wa CCM kwa jimbo la Nzega badala ya Bashe, Dk. Hamis Andrea Kigwangala, naye sio raia wa Tanzania na amekuwa akitumia jina la bandia.

Jina lake halisi la anayejiita Dr. Hamis Kigwangala, kwa mujibu wa Gazeti hilo, ni Said Bagaile. Inasemekana alilipata jina lake la sasa ili aendelee na elimu ya sekondari baada ya kufeli darasa la saba. Inasemekana ameshahojiwa na maofisa wa uhamiaji kuhusiana na suala hilo.
 
Back
Top Bottom