Jina la Said Nassor Bagaile ndiye Hamis Andrea Kigwangalla?

Habari zilizozipata kutoka nzega kwenye chanzo changu ni kuwa Dk. Hamisi Kingwangala alihawi kugushi jina ili kujiendeleza kielimu. Mpo hapo?

===================
UPDATE:

Majibu ya Dr. Kigwangalla (MB)

Jaribu kusoma hapa kigwangalla.blogspot.com na utapata wasifu wangu kama nilivyouandika mwenyewe nilipotangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Nzega.

Pia waweza cheki hapa PEERCORPS - Home kwa taarifa zaidi kuhusu shughuli zangu za kijamii, na jaribu kusearch kwenye Google unawezapata some hits zinazomhusu Kigwangalla.

Kuna watu wengi sana humu wamewahi kusoma na au kufanya kazi na mimi sehemu mbalimbali, wanaweza kukupa majibu mengine na ya ukweli na uwazi zaidi kuhusu mimi na uwezo/uzoefu wangu wa uongozi, kuhusu credibility n.k., n.k.

Jina langu kamili ni hili hapa: Dk. Hamisi Andrea Kigwangalla (wengine huandika jina langu la ukoo kama Kigwangala) hivyo unaposearch jaribu kuweka yote mawili na utapata taarifa nyingi kidogo kuhusu mimi...

Ukitaka kujua zaidi kuhusu mimi na kutoka kwangu, nipigie kwenye namba za simu zilizopo kwenye blogu yangu [kwenye tangazo langu la nia.

Ahsante sana mniMiguwa mwichane [nilisoma Mwanzoli shule ya msingi mnamo mwaka 1991.

Regards,
H.K.

Mimi naitwa Hamisi Andrea Kigwangalla, kama kuna mtu anadai jina langu ni lake na kwamba nililinunua jina lake, sasa si alishaliuza (ha ha ha aaa), ukiuza kitu bado kinabaki kuwa cha kwako tu?

CHADEMA wanafanya siasa kwenye mambo wasiyoyajua. Mimi sijawahi-iba, nunua au hata kusomea shule jina la mtu! Kama yupo mwenye malalamiko hayo si afuate utaratibu wa kudai jina lake??? (Kama amedhulumiwa?)

Haters hamtofanikiwa kunishusha kama Mungu ameamua kunipandisha! You will struggle but you will never be successful since GOD is on my side and time is on my side!

Mjadala huu ulikuwepo sana enzi za kampeni na maelezo yalitolewa na yakatosha. Maajabu yameanza kuibuka upya yaleyale ya zamani baada ya kuona nafanya kazi nzuri jimboni kwangu na wanaolitaka jimbo kushtuka na kuona kimbunga Kigwangalla hakizuiliki!
 
Hilo litakuwa bao la kisigino kama ni kweli, wacha achukue fomu tuu.
 
Habari zilizozipata kutoka nzega kwenye chanzo changu ni kuwa Dk. Hamisi Kingwangala alihawi kugushi jina ili kujiendeleza kielimu. Mpo hapo?

I saw this coming! Will the real Kigwangala please stand up?

Wapinzani wanapaswa kutulia avute form. Hili jimbo lao, without a fight!
 
game ndo 15min sasa!! refa kashapoteza filimbi!! na game inaendelea............source please!!au tuwekee copy ya cheti chake hapa!
 
Duh..inawezekana maana miaka ya nyuma mambo haya ya kurudia shule kwa majina tofauti au kuendelea kwa kutumia jina la mtu mwingine yalikuwapo sana. Huyu tabibu ni member hapa, labda atakuja kuuondoa huu 'ukungu' hapa!
 
By the way, kwa nini ccm wameamua kumpa mshindi wa tatu (Kingwangala) badala ya yule wa pili (Selelii)?
 
Wapo wengi sana CCM wa aina hii Richard Ndasa aliyekuwa Mbunge wa Sumve naye alinunua cheti cha jamaa na kugombea Ubunge! Mwenye jina yuko Mwanza anavua samaki!
 
Habari zilizozipata kutoka nzega kwenye chanzo changu ni kuwa Dk. Hamisi Kingwangala alihawi kugushi jina ili kujiendeleza kielimu. Mpo hapo?

Nafikiri tuchukulie kwa mtazamo mwingine....kuwa aliamua ku-officilize ile 'alias' i.e. Said Nassoro Bogoile alias Hamis Kingwangala. Sasa cha msingi ni kuwa hiyo elimu aliyopata kupitia alias ni kweli au vyeti ni vya kufoji! Kama elimu yake through alias haina mashaka, sioni tatizo. Turudi kwenye utanzania wake kama una shaka hapo ndipo tuseme, lakini kama la sioni hoja.

By the way alias watu walitumia sana huku kwetu enzi hizo kujikomboa wakati wa vita, manake hata elimu ilikuwa vita. Angalia mfano hapo jirani UG akina Generali Salim Saleh et. al. almost wote walitumia alias katika kupokea taaluma zao. Tusisahau mapema hivyo kuwa huko tulipotoka kielimu alias zilitumika sana kutafuta elimu, tumpongeze badala ya kumbeza.
 
hizo sio kampeni za seleli au bashe kumchafuaa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Nzega??? nasikia kuungwanaa amemwahikishia hamisi ushindiii
 
Nafikiri tuchukulie kwa mtazamo mwingine....kuwa aliamua ku-officilize ile 'alias' i.e. Said Nassoro Bogoile alias Hamis Kingwangala. Sasa cha msingi ni kuwa hiyo elimu aliyopata kupitia alias ni kweli au vyeti ni vya kufoji! Kama elimu yake through alias haina mashaka, sioni tatizo. Turudi kwenye utanzania wake kama una shaka hapo ndipo tuseme, lakini kama la sioni hoja.

By the way alias watu walitumia sana huku kwetu enzi hizo kujikomboa wakati wa vita, manake hata elimu ilikuwa vita. Angalia mfano hapo jirani UG akina Generali Salim Saleh et. al. almost wote walitumia alias katika kupokea taaluma zao. Tusisahau mapema hivyo kuwa huko tulipotoka kielimu alias zilitumika sana kutafuta elimu, tumpongeze badala ya kumbeza.

Nadhani ishu ni namna hata hiyo 'alias' ilivyopatikana! Kuna wengi tu huko vijijini walikosa kuendelea na sekondari kwa kuambiwa 'wamefeli' na kumbe walifaulu vizuri tu lakini nafasi zao zilichukuliwa na wajanja wachache 'waliofeli'.

Kwa makosa ya jinai kama haya na kuharibu maisha ya watu wengine kwa hakika hatutakiwi kuyafumbia macho!
 
This is the F that is going on man!!.take it from me.
Lol... at least i laughed for hte first time in four days kwenye jukwaa hili la siasa na uchaguzi

surely that is the F'ing going on

Acidis in the house
 
Nadhani ishu ni namna hata hiyo 'alias' ilivyopatikana! Kuna wengi tu huko vijijini walikosa kuendelea na sekondari kwa kuambiwa 'wamefeli' na kumbe walifaulu vizuri tu lakini nafasi zao zilichukuliwa na wajanja wachache 'waliofeli'.

Kwa makosa ya jinai kama haya na kuharibu maisha ya watu wengine kwa hakika hatutakiwi kuyafumbia macho!

Umenichekesha sana...! Tukubali kuwa 'alias' zipo na zina meaning in life. Then twende one step further kujua 'alias' ilipatikana vipi;

1. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua jina la mtoto mtoro, then mwenye bidii akapewa akaliendeleza kwa kwenda kurudia shule sehemu nyingine. Kundi hili ni kubwa sana Tanganyika, wengi wako kwenye high profile sasa.

2. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua cheti cha ndugu/jamaa/rafiki ambaye anabidii na ameshajiendeleza (mfano yuko university, then mtu anachukua cheti chake cha form four anaenda chuo cha ualimu.....nk). Kundi hili ni kubwa sana Tanganyika hii, na limeenea kwenye sekta za umma zenye kubeba manpower kubwa.

3. 'alias' iliyopatikana kwa kuchukua jina la aliyefanya vizuri na kumpa asiyestahili ili aendelee kielimu. Kundi hili ni dogo kwa vile aliyepewa jina hana uwezo wa kumudu mikiki mikiki ya elimu hivyo nae huwa hafiki mbali.

4. 'alias' iliyopatikana katika utu uzima, kwa kujaribu kudanganya umma ghafla ili kujipatia unafuu wa mambo. Kundi hili ni matapeli. Mfano Dr. Kihiyo.
 
4. 'alias' iliyopatikana katika utu uzima, kwa kujaribu kudanganya umma ghafla ili kujipatia unafuu wa mambo. Kundi hili ni matapeli. Mfano Dr. Kihiyo.

Nimeipenda hii!
 
Back
Top Bottom