Jina la 'Guantanamo' Lavunja Ndoa ya Miaka 17

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039


3361470.jpg

Jina la "Guantanamo" limevunja ndoa ya miaka 17 Tuesday, October 20, 2009 2:23 AM
Ndoa ya miaka 17 imevunjika nchini Saudi Arabia baada ya mume kulihifadhi jina la mkewe kwenye simu yake kama 'Guantanamo' (Jina la jela ya Marekani) badala ya jina lake halisi. Mwanamke mmoja nchini Saudi Arabia amefungua madai ya talaka mahakamani baada ya kugundua kuwa mumewe ameliandika jina lake kwenye simu yake kama 'Guantanamo' badala ya jina lake la kweli au majina ya kimapenzi kama vile honey, sweet na mengineyo.

Guantanamo ni jela yenye ulinzi mkali ya Marekani iliyopo visiwa vya Cuba ambayo watuhumiwa wa ugaidi duniani wanahifadhiwa.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Watan kasheshe hilo lilianza baada ya mwanamke huyo kumpigia simu mumewe na kugundua kuwa mumewe ameisahau simu yake nyumbani.

Katika kuiangalia simu ya mumewe wakati ilipokuwa ikiendelea kuita alishangaa kuona jina la 'Guantanamo' likitokea katika simu ya mumewe wa ndoa ya miaka 17.

Gazeti la Al-Watan liliendelea kusema kwamba mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake aliamua kufungua kesi ya madai ya talaka mahakamani kuivunja ndoa yao ya miaka 17.

Mbali na talaka mwanamke huyo anadai fidia ya kuharibiwa jina lake.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3361470&&Cat=2
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom