Jimbo Lingine la Chadema Hili hapa endapo wakiamua kulibeba kirahisi

Hili jimbo la Moshi vijijini liko complex kidogo. Muundo wake na ukubwa wake unakipa CCM urahisi wa kulichukua.
Haswa wakati Chami akionekana kama mtetezi mzuri wa waKibosho. Jimbo kama sijakosea linajumlisha Kibosho, Uru na Old Moshi. Sababu za kizamani na kiushindani kati ya makundi haya ya kichaga, Mkibosho wa zamani hatakubali kutawaliwa na mu-OldMoshi au mtu wa Uru. Wa Uru nao hawatajisikia kutawaliwa na m-oldMoshi and vise versa.
Huu upuuzi bado upo akilini mwa wazee wa kichaga. Jambo ambalo ni muhimu kufahamu ni kuwa Wakibosho ni wengi sana kupita hayo makundi mengine yote. Kwahiyo kama CDM itataka kulichukua kirahisi kwa kuanzia wampate kijana Makini Mkibosho.
Lifanyiwe mkakati, ni jimbo muhimu sana Kilimanjaro. Watu wa jimbo hilo la Moshi vijijini wanamezea mate sana mambo yanavyokwenda Moshi Mjini kwa Mzee Ndesa.
Pia jimbo la moshi vijijini liko upandwa wa kusini mwa Moshi mjini( Bonite, TPC n.k). Nakubali maelezo yako kwamba kibosho wanaushawishi wa nani awe mbunge Moshi Vijijini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom