Jimbo Lingine la Chadema Hili hapa endapo wakiamua kulibeba kirahisi

rimoi

Member
Mar 9, 2012
13
11
kuna jimbo ambalo wananchi wake huwa wanapima nani mkweli na nani ni muongo kisha wanampa kura, sio jingine bali ni jimbo la moshi vijijini! kwa jinsi navyoelewa watu wa moshi vijijini chadema wakiweka nguvu kidogo sana wanachukua lile jimbo kama kumsukuma mlevi vile!

changamoto yangu ni kwamba lile jimbo ni potential na huwa hakuna propaganda, kama mnataka kujua watu hawa walivyo mwulizeni agustino lyatonga mrema! watu hawa wa moshi vijijini si sawa na arumeru au songea au morogoro au dodoma. wako tofauti kabisa wanaweza kukupa asilimia 90 ya kura kama una bahati na ukaeleweka kwenye kauli zako si kama za kina lusinde

chadema andaeni kichwa kwa ajili ya kulichukua hili jimbo, mbunge wa sasa hakuna anachokifanya tena ni mgonjwa
 
Hivi hilo jimbo lishawahi kuwa chini ya Upinzani?

Lishawahi kuwa chini ya Ngotolainyo wa NCCR Mageuzi kwa vipindi viwili tofauti......Muulize Mkapa si tulishamstukia zamani kuwa ni fisadi alivyoingia hapo tukampopoa na mayai visa. That was year 2000.
 
Hata Tomas Ngawaiya wakati huo akiwa TLP kabla ya kurudi kwa Magamba
 
Watu wa Njombe ni kama vile hawana mbunge. Yaani huyu jamaa ni kilaza haijawahi kutokea. Lakini kwa bahati mbaya CHADEMA haijawahi kusimamisha mtu makini katika jimbo lile. Hebu CHADEMA anzeni kuandaa mtu wa kwenda kulichukua lile jimbo 2015. Kwa hakika mkipeleka mtu makini lile jimbo mnachukua bila shida. Wale jamaa wanataka mabadiliko lakini hawajapata mpinzani wa Ukweli. Alatanga anaonekana mbabaishaji tu. Mara leo yupo NCCR, Kesho TLP, keshokutwa CCM, akishindwa kote anarudi CHADEMA. Nani amchague huyu?
 
Kinachotakiwa ni kuchukua majimbo yote na si moja tu hilo!



Pamoja Kamanda!
Tunahitaji UKOMBOZI kwa kila Mtanzania!

Tunachukua mpk makao makuu ya kile chama cha majambazi na vyote vinavyohusu wao na kuwa mkononi mwa raia!

Haiwezekani wajilimbikizie mimali kiasi hiki!
Na ikiwezekana wale viongozi wao wote wapelekwe mbele ya vyombo vya DOLA hakuna kulala mpk kieleweke!

Nchi yetu bila ccm inawezekana kbs!
 
Mipango ya chama chochote cha siasa ni kusonga mbele zaidi ya pale ilipofikia uchaguzi uliopita, na hatimaye kufikia lengo kuu la kushika dola ili kutekeleza ilani yake kwa wananchi! Ilipofika sasa Chadema ni hatua nzuri na ni dhahiri ya kwamba wananchi wanadhani inaweza kuwa ndio chama mbadala cha kuwaongoza!
Ningependa wadau tuorodheshe majimbo 120 hapa ambayo tunadhani chadema tukijipanga basi hatukosi 100 Mwaka 2015.
1.Arusha Mjini............ Hili litabaki CDM
2.Arumeru........ Litabaki
3. Karatu......... Litabaki
4. Mbeya Mjini.......litabaki
5. Kigamboni....... Aandaliwe mgombea kutoka maeneo ya mbagala, msafi, mtu wa watu, akirudi mgombea wa sasa wa CCM chadema itashinda
6. Mkuranga......... Adam Malima akigombea, CDM itashinda
7. Hai............Kamanda ubaki hapo!
8. Igunga........ Chama kirudi kikateke analau ahadi mbili tatu though hatukushinda
.................
 
9. Singida vijijini, kamanda Lissu anabaki
10. Mr presidaa, tuandalie kiongozi wa kumuacha kigoma kskazini.
 
11. Kawe Mh Mdee hana mpizani atabaki,
12. Ubungo Mh Mnyika hana mpizani atabaki.
 
13. Mbeya Vijini CDM iandae mtu Makini, atakayeunda Team na Sugu! Ni rahisi sana kubebaa pale!
 
Jimbo la mbozi kwa Nzunda linaweza chukuliwa jamaa kapima upepo hatasimama!!
 
9. Singida vijijini, kamanda Lissu anabaki
10. Mr presidaa, tuandalie kiongozi wa kumuacha kigoma kskazini.

Kuhusu Singida mashariki kamanda lissu ataenda kugombea singida mjini then vijijini atasimamishwa kamanda mwingine.....mark my words!
 
Unamaanisha Njombe Mashariki?
Watu wa Njombe ni kama vile hawana mbunge. Yaani huyu jamaa ni kilaza haijawahi kutokea. Lakini kwa bahati mbaya CHADEMA haijawahi kusimamisha mtu makini katika jimbo lile. Hebu CHADEMA anzeni kuandaa mtu wa kwenda kulichukua lile jimbo 2015. Kwa hakika mkipeleka mtu makini lile jimbo mnachukua bila shida. Wale jamaa wanataka mabadiliko lakini hawajapata mpinzani wa Ukweli. Alatanga anaonekana mbabaishaji tu. Mara leo yupo NCCR, Kesho TLP, keshokutwa CCM, akishindwa kote anarudi CHADEMA. Nani amchague huyu?
 
Na makete nao tumeshawasha moto wa mageuzi,Lakini kunavizee fulani vilaza wamechana bendera yetu nakutupa choo,Vijana tumeshaliwasilisha swala hili police limeanza kushughulikiwa,Mkitaka kulijua swala hili mtafuteni m/kiti Chadema wilaya ya makete.Nawasilisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom