Jimbo la Spika lawaka moto!

M-bongo

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
338
71
Jimbo la Urambo leo lilizima kwa maandamano makubwa ya kumpokea kamanda mteule Bwana Ally Maswanya ambaye ni kurugenzi wa kampuni ya Zain kanda ya Ziwa, maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumsimika u-kamanda bwana maswanya ambaye pia anatajwa kulinyemelea jimbo hilo.
Maandamano hayo yaliyotanguliwa na msafara wa pikipiki karibu 70 na tax 50 zilizofuatiwa na magari ya kifahari karibu 30. hata hivyo katika hali ya kushangaza Bwana Spika aligoma kuhudhuria sherehe hizo zilifanyika mbele ya jengo la ccm wilaya ya Urambo, habari zaidi zinasema mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa bwana Edwin sanda (MNEC Uvccm) ambaye alimwakilisha katibu mkuu Uvccm Martin Shigela aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi.
akihutubia wananchi wa Urambo Bwana Maswanya ambaye kwa umri bado anaonekana kijana aliwaahidi vijana wa Urambo kuwapatia vyombo vya usafiri baada ya kuona kuwa vijana hao wamekosa mtu wa kuwajali kwa kipindi kirefu
 
Akufukuzae hakwambii toka, Sitta muda wako wa kukaa CCM umeshakwisha...your targeted...
 
Huyu Edwin Sannda ni mmoja wa vijana wa shoka mwaka huu, an enterprising man ... na nina imani naye but THIS is strange... sitta ameogopa nini badala ya kukaa nao kujua vijana wana nini zaidi yake???
 
Nchi hii ushabiki umezidi, mara nyingine watu hata hawajui wanashabikia nini? Sijui ni kwa sababu hatuna mafanikio ya kushangilia? Sasa huyu kuwaahidi vijana usafiri ana maana gani? Halafu haya mawazo ya mtu kutaka uongozi kwa kusema atanunua hiki kwa fedha zake, ni lazima aulizwe anazipata wapi?
 
Nawaza kwa jinsi Bunge lilivyoendeshwa atleast kidemokrasia msimu huu hata kama ni ni kwa 0.5% democracy, ni hatua kwa Tanzania.Kwa miaka yangu michache niliyoishi na kulitazama Bunge,nimefurahia sana Sitta alivyothubutu kuruhusu baadhi ya mambo kujadiliwa live bungeni, Sikatai baadhi ya madhaifu yake ila nawaza kama Sitta atangolewa basi nani atamrithi. Generally alijaribu hata kama alikua ana agenda ya siri.
 
Nchi hii ushabiki umezidi, mara nyingine watu hata hawajui wanashabikia nini? Sijui ni kwa sababu hatuna mafanikio ya kushangilia? Sasa huyu kuwaahidi vijana usafiri ana maana gani? Halafu haya mawazo ya mtu kutaka uongozi kwa kusema atanunua hiki kwa fedha zake, ni lazima aulizwe anazipata wapi?

Imekuwa ni tabia ya kawaida kwa uongozi wa Tanzania kugombaniwa kwa ahadi hewa> Watanzania wamefikishwa pahala kuwa hata sherehe au pesa ya siku moja basi lazima uchangamkie kwa vile viongozi hawajali wananchi na hufanya hivyo pale tu wanapotaka kuwafanya wananchi ngazi. Ukikataa raha ya siku moja haisaidii kitu kwa wanaotaka madaraka kwani CCM itahakikisha inampitisha na kuchaguliwa yule inayoona ataendeleza sera zao za kujinufaisha.
 
WaTanzania wengi ni wabangaizaji tu, kwa hiyo uwezo mkubwa wa kufikiri unakuwa haupo na mwisho wa yote tunarudi kwenye Kauli ya Mkuu wa Mjengo "WATANZANIA WENGI WANAFATA MKUMBO"
 
Cheap politics!~
watTZ ndo wanapenda hii............nitawanunulieni usafiri.
 
Lyatonga naye alibebwa juu juu akaambulia patupu. Labda kama hao waandamanaji wamejiandikisha kupiga kura na watapiga kura hizo. Kama hajawa mbunge tayari anaandamana na magari ya kifahai 30 na mapikipiki 70 anadhibitisha ufisadi wake hata kabla hajakalia kiti. Hamjasikia yule mhindi fisadi wa Tabora analalamikiwa na watu wake kwamba hawamwoni kusikiliza matatizo yake? Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Kwamba Sita aligoma kuhudhuria asitupiwe mawe hata bila kujua sababu yake. Labda hakualikwa?
 
Nyerere aliwahi kusema kwamba ata jeneza urtembezwa kwa maandamano. Vijana tusimamie katika hoja kwa ajili ya manufaa ya taifa hili na kuachana na mambo ya siasa za bei powa[cheap politics]. Nakutakia heri Bwana Maswanya.
 
Pikipikini ni za kukodi, taxi ni za kukodi, magari ya kifahari pia ni ya kukodi kama ambavyo wengi tunavyofanya kwenye harusi. Wingi wa magari sio lazima iwe ni kiashiria cha mapenzi ya watu kwa mtu bali huenda pia ikawa ni mvuto wa pesa.

Halafu nadhani heading ingekuwa Jimbo la Urambo Mashariki na sio jimbo la Spika, spika hana jimbo.
 
Jimbo la Urambo leo lilizima kwa maandamano makubwa ya kumpokea kamanda mteule Bwana Ally Maswanya ambaye ni kurugenzi wa kampuni ya Zain kanda ya Ziwa, maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumsimika u-kamanda bwana maswanya ambaye pia anatajwa kulinyemelea jimbo hilo.
Maandamano hayo yaliyotanguliwa na msafara wa pikipiki karibu 70 na tax 50 zilizofuatiwa na magari ya kifahari karibu 30. hata hivyo katika hali ya kushangaza Bwana Spika aligoma kuhudhuria sherehe hizo zilifanyika mbele ya jengo la ccm wilaya ya Urambo, habari zaidi zinasema mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa bwana Edwin sanda (MNEC Uvccm) ambaye alimwakilisha katibu mkuu Uvccm Martin Shigela aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi.
akihutubia wananchi wa Urambo Bwana Maswanya ambaye kwa umri bado anaonekana kijana aliwaahidi vijana wa Urambo kuwapatia vyombo vya usafiri baada ya kuona kuwa vijana hao wamekosa mtu wa kuwajali kwa kipindi kirefu

Kama watamchagua huyu basi wa urambo wamekwisha. Yaani kwake kipaumbele ni vyombo vya usafiri. Watanzania ( sio wa Urambo mashariki tu ) tuwe serious na matatizo yanayotukabili watu wanaokaa mjini na kututembelea kila baada ya miaka mitano hawajui shida zetu.

Anadhani tutakula chombo cha usafiri, tukiumwa chombo cha usafiri kitasaidia.
 
uaweza kuthibitisha manaeno haya?
Unataka ushahidi gani Mkuu wakati kila kitu kipo wazi? kaka kuwa targeted si lazima bastola iwe sikioni - ni matendo tu anayofanyiwa huyu kamanda kweli yanaashiria mwisho wa Sitta CCM. na hata akin'gan'gania kubakia humo bado atakuwa na misukosuko mingi sana kuelekea uchaguzi mkuu.

Kitendo cha UVCCM kukabidhiwa majimbo yote ya hawa wapiganaji kuhakikisha yanachukuliwa na wao ni kitendo tosha kwamba wameshawachoka.

Mtera - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Urambo - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Nzega - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Simanjiro - Jimbo limekabidhiwa kwa UVCCM nk

UVCCM watapata kila support kutoka makao makuu kuhakikisha list hii hapa chini hairudi bungeni kwa tiketi ya CCM

Kwa hiyo, Sintashangaa kutowaona Malecela, Selelii, Sitta, Sendeka, Mwakyembe, Sherukindo, Shibuda kwenye bunge lijalo - ni vizuri tu waanze kujipanga mapema kukabiliana na vita hii ndani ya CCM.
 
Tunahitaji vijana zaidi. One of these days Sitta atafukuzwa na kunyang'anywa kadi ya CCM. Lets wait and see...Kwa tabia yake ya kuzungumzia mambo yao ya ndani yaliyotokea kwenye vikao vyao kwenye hadharani, na kwa CCM ninaifahamu nadhani watachukua jukumu la kumwadabisha huyo mzee. Hivyo inabidi aangalie mambo katika kona zote!!!!!!
 
Unataka ushahidi gani Mkuu wakati kila kitu kipo wazi? kaka kuwa targeted si lazima bastola iwe sikioni - ni matendo tu anayofanyiwa huyu kamanda kweli yanaashiria mwisho wa Sitta CCM. na hata akin'gan'gania kubakia humo bado atakuwa na misukosuko mingi sana kuelekea uchaguzi mkuu.

Kitendo cha UVCCM kukabidhiwa majimbo yote ya hawa wapiganaji kuhakikisha yanachukuliwa na wao ni kitendo tosha kwamba wameshawachoka.

Mtera - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Urambo - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Nzega - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Simanjiro - Jimbo limekabidhiwa kwa UVCCM nk

UVCCM watapata kila support kutoka makao makuu kuhakikisha list hii hapa chini hairudi bungeni kwa tiketi ya CCM

Kwa hiyo, Sintashangaa kutowaona Malecela, Selelii, Sitta, Sendeka, Mwakyembe, Sherukindo, Shibuda kwenye bunge lijalo - ni vizuri tu waanze kujipanga mapema kukabiliana na vita hii ndani ya CCM.
Mkuu kwa Sendeka, lazima apite, jina lake limepanda sana hasa baada ya kushinda kesi ya Millya. Millya pia alikosea alipofuatwa na wazee wa kimila wa kimasai kwa kuombwa suluhu akawatoroka. Hata Askofu naye alimwomba kuwa patana na ndugu yako akakataa pia. Sasa kwa desturi za Kimasai mtoto ambaye hasikii wazazi ni mtovu wa nidhamu. Halafu pia imewachukiza sana baadhi ya Wamasai kwa kitendo kile ambacho kijana inaonekana anatumiwa na kigogo!!!!
 
Mmh isije ikawa ni mchezo wa mafisadi wanataka ku-plant mtu wao. Kwa hali ya kawaida mtu anawaahidi vijana usafiri katika mkutano wa hadhara i!!!!!!!Je ni pikipiki, au bajadi na wakizipata hizo itakuwa mwisho wa matatizo yao? Je fedha atakuwa amezipata wapi? na atazirudishaje? kwa hali hii rushwa kuisha Tanzania ni ndoto. Mzee wangu Sitta wala usikate tamaa. Mtu mzima hatishiwi nyau
 
Back
Top Bottom