Jimbo la Segerea: Liwike lisiwike kutakucha tu!!

Status
Not open for further replies.

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,397
92,728
Wakuu nawasalimu wote kwa jina la aliye mkuu,
Sikuwa na ulazima wa kuanzisha thread hii lakini nimelazimika kuianzisha thread hii mapema ili kuondoa mikanganyiko isiyokuwa na ulazima

Ikumbukwe kesho ndio tarehe 2 may, kwa sisi wapiga kura wa Segerea tunategemea kutendewa haki yetu na Mahakama kuu kuhusu kesi ya Fred Mpendazoe vs Makongoro Mahanga.

Sasa basi si nia yangu kupendekeza udikteta au ukiritimba wa Habari, bali kutokana na mfumo mbovu unaooneshwa na baadhi ya Member wenzetu hapa katika kupashana habari napendekeza hivi:
Invisible kesho ndiyo abebe jukumu la kuanzisha thread kwa Mtindo wa LIVE ili members wengine ndio watakuwa wanatupia habari kwenye thread, kwa Sababu kesi hii iko Mahakama kuu Dar es salaam nina uhakika watu wengi watakuwa na access ya kuleta habari Immediate.
Hayo ni maoni yangu tu wadau, au mnasemaje?
 
Kutokana na mfumo mbovu unaooneshwa na baadhi ya Member wenzetu hapa katika kupashana habari napendekeza Invisible kesho ndiyo abebe jukumu la kuanzisha thread kwa Mtindo wa LIVE ili members wengine ndio watakuwa wanatupia habari kwenye thread.

Matola,
Katika hali ya kawaida mwanzisha thread ndiye anatakiwa awe eneo la tukio kwa ajili ya kutoa habari. Sasa hili wazo lako naona halipo kiuhalisia maana utakuwa unaendeleza tabia zilezile za baadhi ya member ambao wanakurupuka kuanzisha thread alafu wanategemea wengine wajaze habari. Mi nashauri mtu atakae kuwa Mahakamani ndiye aanzishe thread ya Live.

Invisible kazi yake iwe kumodarate thread kwa kuidentify member yupi yupo mahakamani then aifanye thread yake ndiyo ibebe kichwa cha thread zote zitakazokuwa zinajitokeza. Tuendeleze utamaduni wetu wa kila member kuwa huru kuanzisha thread na tuwaache moderators wafanye kazi yao.
 
well said mkuu, maana bila hivyo kesho humu itakua vurugu kila mmoja atajifanya ni reporter.. Invisible tunakuomba mkuu kama hautajali ufanye kama mkuu Matola alivyotoa pendekezo
Manyanza Asante kwa kunielewa mtizamo wangu maana walisema miluzi mingi humpoteza Mbwa, Tunaomba Invisible azingatie ushauri huu ili kutokuwachosha watu humu kesho kuzungukazunguka.

Mimi nikiwa kama mdau wa Maendeleo Segerea najuwa fika ni nini kitatokea kesho na ndio maana naomba hata walioko ughaibuni wajione kama wako LIVE mahakamani kufuatilia hukumu ya kesho.
 
Last edited by a moderator:
Matola,
Katika hali ya kawaida mwanzisha thread ndiye anatakiwa awe eneo la tukio kwa ajili ya kutoa habari. Sasa hili wazo lako naona halipo kiuhalisia maana utakuwa unaendeleza tabia zilezile za baadhi ya member ambao wanakurupuka kuanzisha thread alafu wanategeme wengine wajaze habari. Mi nashauri mtu atakae kuwa Mahakamani ndiye aanzishe thread ya Live.
TUMBIRI ni kwa nini una underestimate the power of JF Team? umetumia akili zako kufikri kabla ya kuandika au umeandika halafu ndio unaanza kufiri?

Yaani matukio makubwa kama haya yatokee Dar es salaam halafu JF Team isiwepo pale kuripoti hivi umeshirikisha ubongo wako katika hili?
 
Last edited by a moderator:
Manyanza Asante kwa kunielewa mtizamo wangu maana walisema miluzi mingi humpoteza Mbwa, Tunaomba Invisible azingatie ushauri huu ili kutokuwachosha watu humu kesho kuzungukazunguka.

Mimi nikiwa kama mdau wa Maendeleo Segerea najuwa fika ni nini kitatokea kesho na ndio maana naomba hata walioko ughaibuni wajione kama wako LIVE mahakamani kufuatilia hukumu ya kesho.

Hivi mtani wangu unaqoute kivipi ili jina litokee kama hapo kwenye red? sorry out of topic:help::wave:
 
Hivi mtani wangu unaqoute kivipi ili jina litokee kama hapo kwenye red? sorry out of topic:help::wave:

[h=2]
icon1.png
Tag someone on JF[/h]
Tuna marafiki na jamaa ndani ya JF. Tunaanzisha mijadala au tunaona mijadala ndani ya JF na tungependa wafahamu juu ya mjadala husika na tunakosa namna ya kuwashtua ili aidha washiriki au wasome mjadala husika. Tumeona vema tuanzishe MENTION ili tuweze kuwashirikisha kwa notifications (si emails/PM) hapahapa JF.

Kama ukitaka mtu asome thread yako basi tumia hii "@" ikiwa imeungana na jina la mtu mfano:
Code:

type : @ followed by the name of the person you want to tag. For example : @Invisible @RussianRoulette
Invisible na Fang ni mods wakorofi sana.

Au MNYISANZU na Preta ni members wasumbufu ktk JF.

Check settings: https://www.jamiiforums.com/usertag.p...action=options

Hiyo ni mifano tu, don't take it serios lol​

TUMBIRI ni kwa nini una underestimate the power of JF Team? umetumia akili zako kufikri kabla ya kuandika au umeandika halafu ndio unaanza kufiri?

Yaani matukio makubwa kama haya yatokee Dar es salaam halafu JF Team isiwepo pale kuripoti hivi umeshirikisha ubongo wako katika hili?

mkuu Matola nimemshangaaa sana Tumbiri, kama watu waliweza kutoa report ya kila kitu kilichokua kinaendelea kwenye msiba wa Kanumba, itashindikana kwa hili la hukumu ya ya kesi ya Segerea? tena jambo ambalo ni la muhimu kwa ustawi wa wapenda mabadiliko

Dah watu tumetofautiana katika fikra..
anyway tunamuomba Invisible kesho asimamie mwenyewe kama atakua ana nafasi
 
TUMBIRI ni kwa nini una underestimate the power of JF Team? umetumia akili zako kufikri kabla ya kuandika au umeandika halafu ndio unaanza kufiri? Yaani matukio makubwa kama haya yatokee Dar es salaam halafu JF Team isiwepo pale kuripoti hivi umeshirikisha ubongo wako katika hili?
Matola
Bahati nzuri wewe ni Mchadema mwenzangu na wote tunaishi Segerea. Kwa kifupi sijaunderstimaete the power of JF team. Ninachokwambia ni kwamba tuwaache moderators wafanye kazi zao na sisi members tuendelee kuenjoy haki yetu ya kuleta na kupokea habari humu Jamvini. Kwenye hoja yako labda ungeweka msisitizo kwamba atakaekuwa mahakamani ndiye aanzishe thread na awa anaupdate. Hapo ningekuelewa.

Ukumbuke pia Invisible ni mwanadamu kama sisi. Wewe unataka kesho aanzishe thread ya Live ya hukumu ya Jimbo la Segerea, Je unajuaje kama kesho Mungu atamjalia pumzi (Ingawa sipendi itokee)? Na kama atakuwa hai unajuaje kama ataamka saa tisa jioni? Je huoni kwamba watu watakuwa kwenye tension ya kusubiri na kutafuta thread ya Invisible wakati may be Invisible wakati huo labda katingwa na majukumu mengine? Au unadhani Invisible anashinda JF?

Matola,
Bahati nzuri wewe ni Mchadema mwenzangu na wote tunaishi Segerea. Kwa kifupi sijaunderstimaete the power of JF team. Ninachokwambia ni kwamba tuwaache moderators wafanye kazi zao na sisi members tuendelee kuenjoy haki yetu ya kuleta na kupokea habari humu Jamvini. Kwenye hoja yako labda ungeweka msisitizo kwamba atakaekuwa mahakamani ndiye aanzishe thread hapo nimekuelewa.

Ukumbuke pia Invisible ni mwanadamu kama sisi. Wewe unataka kesho aanzishe thread ya Live ya hukumu ya Jimbo la Segerea,
Je unajuaje kama kesho Mungu atamjalia uhai (Ingawa sipendi itokee)? Na kama atakuwa hai unajuaje kama ataamka saa tisa jioni? Je huoni kwamba watu watakuwa kwenye tension ya kusubiri na kutafuta thread ya Invisible wakati may be Invisible wakati huo labda katingwa na majukumu mengine? Au unadhani Invisible anashinda JF?

duh! mkuu hua tunaishi kwa imani maana hakuna anayejua kesho, ndio maana maandiko huwa yanasema usihangaikie kesho itajihangaikia yenyewe...
 
Hili wazo nadhani ni sahihi sana Matola..!
Katika mazingira ya sasa member wengi wanakuwa na hisia kali pale kunapokuwa na tukio kubwa, na mara nyingi inapelekea vurugu na kupotea kwa mtirirko wa habari, pia huwa inawaongezea kazi zisizo za ulazima Mods wetu!

Pia ni kweli uzi akianzisha Invisible unabeba kiasi kikubwa cha kuaminiwa!
 
Last edited by a moderator:
Matola
Bahati nzuri wewe ni Mchadema mwenzangu na wote tunaishi Segerea. Kwa kifupi sijaunderstimaete the power of JF team. Ninachokwambia ni kwamba tuwaache moderators wafanye kazi zao na sisi members tuendelee kuenjoy haki yetu ya kuleta na kupokea habari humu Jamvini. Kwenye hoja yako labda ungeweka msisitizo kwamba atakaekuwa mahakamani ndiye aanzishe thread na awa anaupdate. Hapo ningekuelewa.

Ukumbuke pia Invisible ni mwanadamu kama sisi. Wewe unataka kesho aanzishe thread ya Live ya hukumu ya Jimbo la Segerea, Je unajuaje kama kesho Mungu atamjalia uhai (Ingawa sipendi itokee)? Na kama atakuwa hai unajuaje kama ataamka saa tisa jioni? Je huoni kwamba watu watakuwa kwenye tension ya kusubiri na kutafuta thread ya Invisible wakati may be Invisible wakati huo labda katingwa na majukumu mengine? Au unadhani Invisible anashinda JF?

Hili nalo neno
 
Last edited by a moderator:
Hili wazo nadhani ni sahihi sana Matola..!
Katika mazingira ya sasa member wengi wanakuwa na hisia kali pale kunapokuwa na tukio kubwa, na mara nyingi inapelekea vurugu na kupotea kwa mtirirko wa habari, pia huwa inawaongezea kazi zisizo za ulazima Mods wetu!

Pia ni kweli uzi akianzisha Invisible unabeba kiasi kikubwa cha kuaminiwa!
Umenena vyema, nadhani hata Mods wataungana na wewe kwa sababu tunawasumbuwa sana kulazimika kuziunganisha thread kila wakati.

Siku hizi umezuka mtindo hapa JF mfano kuna reporter wa TV station fulani anaripoti habari muhimu basi kabla hajamaliza kuripoti ile Habari unashangaa hapa JF mtu kashaanzisha thread yenye heading tu bila maelezo yoyote zaidi ya Source ITV news!! haya ni mambo tunayopaswa kuyapiga vita kwa nguvu zote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom