jikumbushe st. margaret Marangu Girls

Joyceline

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
1,010
166
Kwanza nadhani kwa wote waliosoma st. Magret wanakumbuka jinsi tulivyolima mashamba na kung'oa visiki vya kahawa.
Je mnakumbuka tulivyokuwa tunacheza netball na Ashira Girls wanatufunga tunawazomea tunawakimbiza na makele.
Mnakumbuka mto chapadindi siku ya shida ya Maji tunaenda kuoga wanafunzi wa olaleni sec wanatukimbiza.
Ha ha jirani zetu Marangu sec wasichana tulikuwa hatupatani eti wanasema tunawaibia wanaume wao.

Manamkumbuka Mwalimu mmoja hivi nimemsahau alikuwa akijua umejificha uvunguni anamwaga maji,
Mankumbuka tunaiba mahindi tunayachoma kwenye jalala kwenye matakaataka (bila kutoa maganda lakini)
Manamkumbuka heardmaster mwl. barati akitooka kulewa hata saa 8 usiku anatuamsha anatuambia tulale salama anafungua barua zetu anazisoma ananza kutuponda
Lakini na mkumbuka headmistress Mary alipofika tu akatunyoa nywele huyu mama alikuwa na roho mbaya san sijui sasa hivi yuko wapi

Lakini ilikuwa raha sana tunakumbuka
 
Ha ha jirani zetu Marangu sec wasichana tulikuwa hatupatani eti wanasema tunawaibia wanaume wao.
Hiyo shule yenu si ni ya utakatifu(St)? kumbe nyie ndio mnaotupa shida vigangoni mwetu kumbe mlianza zamani.......
anyway,ulimaliza mwaka gani? panfriend wangu alisoma hapo
 
Joyceline

ulisoma mwaka gani hapo st.margaret?

nikikumbuka kile kilimo kama vile tulikuwa tunasomea agriculture, huh!

mwalimu Makaka ulimkuta? yupo wapi siku hizi?

shule za moshi/arusha zilikuwa na changamoto sana..boarding lakini unakuwa mkakamavu.

nakumbukia mchakamchaka.
 
Mambo belinda

nakumbuka sana tulivyokuwa tunalima, kila mtu anakatiwa robo eka apalilie mwenyewe ukikutwa umeajiri mwanakijiji unakatiwa robo nyingine,

mchakamchaka kiboko tulikuwa tunakimbia tukifika njiani tunarudi tunasema tumekutana na kibwengo, boarding raha sana.

Mwl . Makaka nasikia alienda kujiendeleza ila sijui wapi

wewe ulimaliza mwaka gani?
 
Yes, mambo ya vibwengo usiku we acha tu ila ni kumbukumbu iliyobaki maishani mwetu.

mimi sikumaliza pale. nilihama mwaka 1997 kutokana na sababu fulani hivi.

nawakumbuka madada wa wakati huo kama Siah(Head girl), Vivian(anafanya ifm sasahivi), Dinah(anafanya itv) na wengineo.

Jamani maji ya kuoga yalikuwa baridi sana. na lile duka letu,ukinunua soda ulikuwa unajisikia sana maana zilikuwa adimu.

kasheshe kuvuna kahawa kila jioni ukichoka unachanganya na mbichi ili mradi ndoo yako ijaye ukapumzike then uoge na kwenda kusoma.

wakati ule alikuwa mkuu wa shule wa kike, jina limenitoka.
 
Back
Top Bottom