Jiko

Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,928
5,615
Ninapokuwa nimetulia, huwa napenda kuandika kidogo....

JIKO
Yapo aina nyingi, bei yazidiana,
Ya tofauti shilingi, pia kulitumia,
Kuna ya ujuzi mwingi, na ule wa kawaida,
Jiko lako aina gani?

Kuna la kuni, hili la asilia,
Lavuma vijijini, wengi limetulea,
Hadi usukumani, kina mama wanalitumia,
Jiko lako aina gani?


Kuna jiko la mkaa, lipo zaidi mjini,
Lahitaji fedha, kuleta mkaa toka shambani,
Lahitaji cha kuwashia, mafuta au moto kwa jirani
Jiko lako aina gani?


Sijasahau la mafuta, kazi ya mchina,
Halina kufurukuta, njiti ya kiberiti lawaka,
Mpishi tafuta, haraka litawaka,
Jiko lako aina gani?



La gesi kama jeshi, ghafla laweza lipuka,
Katu halina moshi, halileti mafua kwa anayepika,
Rahisi kwa mpishi, chakula huiva haraka,
Jiko lako aina gani?

Lengo si majina, bali chakula cha kufaa,
Usiwe na haraka, pishi utalichukia,
Sharti kuelewa kwanza, pasi haraka kurukia,
Jiko lako aina gani?

Linalowaka taratibu, kamwe usilikimbize,
Ama sivyo utaharibu, daima likuchukie,
Nakusihi usijaribu, ya kobe kumpa ngedere,
Jiko lako aina gani?

Si kawaida ya jiko kusema, bali kimya kunung’unika,
Ukiwa na haraka utahema, bila kufika muafaka,
Kabla mate halijatema, ndugu yangu wajibika.
Jiko lako aina gani?

 
Am so proud of you, cku nyingi kweli kumuona au kumskia mtu mwenye ujuzi huu..
 
Amejitahidi kuandika lkn bila vina wala maneno ya kulingana, unapaswa kuyafanya maneno 8 na herufi za kati au mwisho zilingane.
but keep up.
 
Amejitahidi kuandika lkn bila vina wala maneno ya kulingana, unapaswa kuyafanya maneno 8 na herufi za kati au mwisho zilingane.
but keep up.
Sure, thnx. mm mwanafunzi sana ktk anga hizi. I just do 4 pleasure. 2gether, let's do it without worrying about the rules of the game. We can get there gradually.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom