Jiji: Machinga complex ipigwe mnada, fedha za kulipa mkopo wa NSSF haipo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mamlaka ya jiji imeomba kuipiga mnada jengo la Machinga Complex kwa kuwa hawana fedha za kulipa deni hilo linaloelekea zaidi ya bilioni 32
 
Hata Planning ya Kulitumia wameshindwa!! Meya wa ilala amebaki Kuvaa mapete Makubwa (Kijana Mdogo) na kubadilisha suti Tu!!
 
huku kikwete alitoa ahadi 2010 ya kujenga jingine kinondoni na temeke!NSSF tuambieni madeni yasiyolipika ni kiasi gani?
 
huku kikwete alitoa ahadi 2010 ya kujenga jingine kinondoni na temeke!NSSF tuambieni madeni yasiyolipika ni kiasi gani?

Tatizo sio Madeni yasiyolipika bali ni kuna mpango Gani wa kuliendeleza na kulitumia umeratibiwa? Mimi Niliwashauri wafanye Haya ili soko liweze Kutumika

1: Waboreshe Njia zote za Kuingia na kutoka sokoni (Pedestrian route na kituo cha public buses)

2: Wawaondoe wafanya Biashara wote wanaofanya Biashara karibu na jengo hilo ili Watu washawishike Kuja kununua hapo

3: Si lazima Watu kuendelea kufanya biashara barabarani maeneo ya Kongo, Msimbazi, Uhuru na kwingineko wakati Jengo lipo!! (Sheria kali kuwaondoa)

4: Kuwapa Tax holiday (Kuwasamehe Kodi kwa muda wa miezi sita kama wanavyosamehewa wawekezaji wengine) Wajasiriamali wote

5: Lianziswe Eneo Jingine ambapo wajasiriamali hawa ambao watakuwa wamekosa nafasi waweze Kuhamishiwa Hapo (Eneo linunuliwe na kuwekewa miundombinu) ili wasizurure karibu na mradi wa jengo (Sheria Kali zitumike)

6: Yafanywe matangazo kwenye TV kuwaelimisha watu Umuhimu wa kunua Bidhaa kwenye maeneo yanayotambulika na huyo mfanyabiashara awe na reference place!! where you can contact him / she.

Kwa hiyo mimi siku zote huwa namlaumu sana huyu meya wa ilala (Eye of the City) Kwa kushindwa kutujengea ustaarabu ndani ya jiji!! amekuwa akipiga siasa Tuu (Shame on this Kijana)
 
Aiseee baba yangu yale majengo ni bora 2fuge kuku ngombe na mbuzi wa kisasa
 
Huu ni upungufu wa Akili Kichwani yaani UAKI! Yaani serikali iandike business proposal ya kuanzisha Machinga complex, ikope hela kwa kutumia hiyo proposal na ishindwa kuzalisha na kushindwa kulipa mkopo! Huu ni UAKI. Na bado Rais alitoa ahadi wakati wa uchaguzi mkuu kuwa zitajengwa NYINGINE TANO! Sasa tuseme hao Jiji wanataka kuvuruga ahadi za Rais? Jamani msimwangushe Rais endelezeni mradi huu.
 
Hela zetu kupitia NSSF! Na bado mnategemea ukifikisha miaka 55 ama 60 kuwepo na hela za kukulipa mafao yako??!!??
alafu eti NSSF wanataka wakawekeze na Nairobi pamoja na Maputo.
Tuombe Mungu hii serikari itoke madarakani mapema ili kuusuru kidogo kilichobaki maana hawa watu inaelekea malengo yao sio mazuri, wanaangalia 10% tu
 
nilikuwa naifikiria hii habari tangu jana.
Nasikia pale NSSF wana department ya watu 'walioenda shule' ya property valuation na project feasibility study lakini uki sample out hii project moja tu ndipo utajua kuwa projects zote wanazofadhili huu ndio mwelekeo wake!
Na je, kama hili jengo linauzwa unadhani wataweza kupata hata robo ya pesa walizowekeza Machinga Complex?

Lawama zote inabidi ziende serikalini maana hii NSSF ni shirika la Umma na City ni sehemu ya umma hivyo tungelikuwa na Uongozi wenye upeo wa kuona mbele wasingeruhusu mradi kama huu kutake off!
 
Hii ndio jibu la kwa nini jamaa wanaanzisha sheria za kipumbavu za kutaka wanachama wasichukue mafao yao,
hii ni moja tu kuna mikopo mingapi ya NSSF kama hii isiyoweza kurejeshwa.Naichukia hii serikali na sekta zake.
 
Nakubaliana na suala la kuwa soko kwa kuwa hatua kadhaa kutoka pale Soko la Ilala limefurika kiasi kwamba wafanyabiashara wameziba mitaa.
 
Hili nalo ni dili lingine,sibiri uone.Wameshapiga hesabu tunapataje hilo jengo na utaona watakao nunua walewale na baada ya muda watapangisha watu kwa bei za kariakoo na mtashangaa jiji limeshindwa nini?LET US WAIT AND SEE
 
Inafaa aliyeandika "feasibility study" ya huo mradi anyongwe kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa

kosa kubwa lililofanyika ni kutaka kugeuza matching guys kuwa walipa kodi za maduka. Walitanganza watu waombe vibanda ndipo mafisi wa nchi hii wakapata nafasi ya kugawia ndugu zao wasiokuwa na vigezo umiliki wa eneo la biashara. Wanachotakiwa kufanya sasa hivi ni kuachana na mambo ya watu wanaotaka kuomba watume maombi. Tangaza wale wote wanaohitaji vibanda wafike eneo husika siku ya ugawaji wakiwa na document za muhimu kama kitambulisho, barua ya mtaa, pasport na nyie mkijiandaa kuwa na mkataba wa kuingia nao siku hiyo. Atakayewahi anapata kibanda mkataba unaingiwa anaendelea na biashara. Kodi ya pango ipunguzwe isiwe kama maduka ya mtaani, kodi ya mapato wasamehewe kwa muda wa miezi sita ili wajijenge kiuchumi na kuanza kulipa tax. Watu wengi waliotakiwa kupata nafasi waliomba na hawakupewa wakapewa wenye uhusiano na wenye mamlaka ya ugawaji. Waliopewa wenyewe hawakuwa tayari kufanya biashara na mabanda yakabaki wazi na machinga wakarudi mtaa wa kongo na mchikichini.
 
usungilo "feasibility" study haikueleza utaratibu utakaotumiwa kuwapata wapangaji? Kama jibu ni ndiyo, utekelezaji umezingatia hilo? kama jibu ni hapana hao waliosimamia utekelezaji ndivyo sivyo bado ni watumisha wa umma? Kama jibu ni ndiyo kwa nini tusiazime sheria za China ili zitumike kurekebisha hili tatizo "once for all"?
 
Last edited by a moderator:
usungilo "feasibility" study haikueleza utaratibu utakaotumiwa kuwapata wapangaji? Kama jibu ni ndiyo, utekelezaji umezingatia hilo? kama jibu ni hapana hao waliosimamia utekelezaji ndivyo sivyo bado ni watumisha wa umma? Kama jibu ni ndiyo kwa nini tusiazime sheria za China ili zitumike kurekebisha hili tatizo "once for all"?
hizi lugha za 'feasibility', projects, michakato nk zinawasidia sana wenzetu kupata maendeleo lakini hapa kwetu ukizisikia tu ujue ni umasikini!!!
Pamoja na rasilimali zote bado hatuna maendeleo yoyote ya maana!
Kweli wahenga walikuwa smart pale waliposema "penye miti hakuna wajenzi"!

 
Inafaa aliyeandika "feasibility study" ya huo mradi anyongwe kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa

inaonekana hii ni very well planed mission ya kuichukua hiyo ardhi, kama ni kuuza basi wauze collateral iliyotumika kuchukulia mkopo, na kabla ya kufanya hivyo, ifanyike kama ulivyopendekeza.
Kwa maneno mengine wametutia ndimu!!!
 
Back
Top Bottom