Jiji la mbeya na changamoto zake

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,488
257
JIJI LA MBEYA NA CHANGAMOTO ZAKE

Katika hali ya kawaida na iliyopo miongoni mwa watu wengi na hususani waliopo nje ya mkoa wa Mbeya wanapopata fursa ya kujadili ama kusikia habari za jiji la mbeya huvutiwa sana na hata wengine wamesikika wakidai Mbeya ni zaidi ya Mwanza, na hata Arusha. Hali hii imekuwa ikichukuliwa kama mzaha fulani kwa wenye Mbeya yao, hasa ukizingatia rasilimali asili zilizopo, jiografia na hali ya hewa inayoruhusu mji kukua ikiwa ni pamoja na kujaliwa watu wachapa kazi kwa upande mmoja, jambo ambalo wanaamini Mbeya haipo katika hatua stahili kimaendeleo, na hivyo kuona haja ya kufanya mabadiliko katika nyanja mbalimbali ikiwepo ya kisiasa.

Dhana ya mabadiliko kisiasa inathibitishwa na historia ya mapokeo ya mageuzi katika miaka ya tisini ambapo wananchi waliweza kukipatia chama cha NCCR- Mageuzi zamana ya ubunge na hatimae tena CCM mwaka 2000-2010 na kwa mara nyingine tena Chadema. Naamini watanzania wenzangu kwa mwenendo huwo ni wazi wanambeya wanayo malengo yao wanayohitaji kuyafikia, na kwa lugha rahisi malengo hayo kutofikiwa kwa sehemu kubwa ndicho kimechukuliwa kama kipimo cha viongozi wetu wa kisiasa kuendelea au kuondolewa katika nafasi husika.

Malengo yanayotakiwa kufikiwa na sehemu kubwa ya wanambeya si ya ajabu zaidi ya kuona rasilimali zilizopo zinasimamiwa kwa maslahi ya taifa, kwani mara kadhaa imekuwa ikiwafadhaisha sana wanapopata habari ya matumizi mabovu ya pesa zao katika halmashauri ya jiji kiasi cha kupata hati chafu (Qualified report), Miradi mingi isiyoisha kwa wakati, usimamizi mbovu wa shughuli na raslimali za jiji, kama magari ya taka kusomba mchanga, mawe, na samadi wakati hali ya usafi wa jiji ukiwa tete, na wakati mwingine kupelekea hata uongozi wa mkoa kuingilia utekelezaji wa majukumu hayo. Wanambeya wamesikika mara kadhaa wakilaumu ufanisi na michango kiduchu utolewao na jiji katika kuchangia shughuli za maendeleo na badala yake kuwaachia mzigo mkubwa wananchi, na hata pale wanapojaliwa kutoa basi uwazi wa michango hiyo umekuwa wenye mlolongo mrefu na bila sababu. Miradi kadhaa imesemwa kuhusishwa na tatizo hilo ikiwemo miradi ya TASAF, DAD’s, ujenzi wa shule za sekondari, msingi, na hata utoaji wa ruzuku za kimaendeleo ndani ya kata, umekuwa ni tatizo kubwa hasa ukizingatia kuwa haufuati kanuni (formular) inayotaka ruzuku hiyo kutolewa kwa kufuata uwiano wa pato la ndani lililopatikana kwa kipindi cha gawio hilo.

Changamoto ni nyingi ikiwemo kukiukwa kwa makusudi kwa ushauri na maelekezo mbalimbali ya wataalamu wa ndani ya halmashauri yenyewe na hata nje ya halmashauri, mfano ni kubadili matumizi ya fedha za miradi unaoenda sambamba na kujengewa hoja zenye nguvu ya maslahi binafsi mfano badala ya kujenga (NEW BUILDING) wamekuwa wakiishia kukarabati hususani katika miradi ya AFYA, MAJI.

Maamuzi mengi kandamizi yasiyolenga madhara kwa upande wa pili na ambayo mara kadhaa yamekuwa yakitolewa kwa visingizio vya maelekezo ya juu, au chama ni alama kubwa ya uwezo mdogo wa uendeshaji wa halmashauri, migogoro iliyopelekea matabaka yasiyoisha kati ya watendaji wenyewe kwa wenyewe, na hata madiwani wenyewe kwa wenyewe kimekuwa ni kigezo kikubwa kwa wananchi waliowengi kuona Mbeya haiendi na badala yake raslimali zao zinatumika zaidi kutatua migogoro hiyo na si vinginevyo.

Mkuu umeongea mengi sana lakini kwa jiji la Mbeya na vitongoji vyake unaweza kuona yafuatayo:
  • Barabara nyingi hazina lami umiacha zile barabara kuu.Sehemu za Mwanjelwa,kwa Mama Joni, Sai,Mwakibete.Sehemu hizi Jiji limepiga "marufuku" barabara hizi kuwekewa lami.
  • Majumba mengi ya jiji la Mbeya ni ya UDONGO! katika karne hii ya 21!!!! Lazima uwepo mkakati maalum wa kuondoa nyumba hizi na kuweka sheria ndogo ya kuweka viwango vya nyumba zitakiwazo katikati ya Jiji.
  • Kiwanja cha Sokoine katikati ya Jiji la Mbeya ni aibu ya mwaka.Uwanja huu ni gofu lisilotazamika
  • Hakuna mkakati wowote wa kuendeleza CBD(Centra Business District) kwa kubomoa nyumba za udongo sehemu zinazozunguka soko la Matola.Sehemu ambazo ziko katikati ya Jiji
  • Kutokamilika kwa kiwanja cha ndege cha kimataifa, Songwe inapunguza sana hadhi ya Mbeya kuwa Jiji.
Mbeya ni Mkoa /Jiji tajiri sana hasa kutokana na position yake kijiografia.Jiji la Mbeya ni njia kuu kuelekea Congo,Zambia na Malawi.
Ni miji michache nchini yenye oppurtunity kama hii.
Viongozi wa Jiji la Mbeya lazima wawe na vision ya kuona mbali
 
pia bara bara ya south to Egypt imepita pale
 
unanikumbusha kauli ya rafiki yangu mmoja aliyesema MBEYA siyo jiji walimaanisha kijiji kikubwa
 
Kuna Hospitali maarufu sana ya akina mama pale Uyole inaitwa Uyole Hospital au Hospitali ya Sijabaje. Wakti wa mvua wagonjwa ili wafike huvushwa kwa baiskeli au kwa migongo ya watu. Jiji wamshindwa kuweka Karvati kwa muda mrefu: hii hospitali ni tegemeo la wote Nyanda za juu Kusini na hata wengine wanatoka nje ya hiyo Kanda.
 
Hivi ilikuwaje Mbeya ikawa Jiji.......shame! shame!

Mkuu Lole...kaelezea vizuri sana kuhusu huu mkoa.....natamani viongozi wa mkoa ule wangepata ujumbe wa Lole.........au wewe mwenyewe Lole wafikishie huo ujumbe wako..........
 
Kuna Hospitali maarufu sana ya akina mama pale Uyole inaitwa Uyole Hospital au Hospitali ya Sijabaje. Wakti wa mvua wagonjwa ili wafike huvushwa kwa baiskeli au kwa migongo ya watu. Jiji wamshindwa kuweka Karvati kwa muda mrefu: hii hospitali ni tegemeo la wote Nyanda za juu Kusini na hata wengine wanatoka nje ya hiyo Kanda.

kwa ujumla swala la barabara siyo kipaombele cha jiji letu, na kwa mwaka huu wa fedha sidhani kama watamudu, kwani ktk budget wana deficit ya karibu 7.5 tillion kwa makisio hewa kwa vyanzo ambavyo havijaweza kuzaa matunda kama, walitegemea kupata zaidi ya shs 3 tillion kwa misingi ya kuanza kukusanya kutoka soko jipya la kisasa, na walikisia kupata zaidi ya tillion 5tillion mauzo ya viwanja ambavyo havijapatikana. utaona mradi wa hostel ulioanzishwa na mkurugenzi wilson kabwe umekwama mara tu baada ya loans board kutoa mkopo wa nyongeza wa zaidi ya shs 400 million.
 
pia bara bara ya south to Egypt imepita pale

Kumbuka ndugu yangu shida ni viongozi tulionao na wakati mwingine lawama ziende kwa wapiga kura wetu kwani wataalamu wanasema garbage in garbage out. ukuchagua bomu lazima litazaa bomu.
 
mh. Sugu atalimudu vyema!

Nashawishika kuungana na wewe haswa ukizingatia historia inatwambia Mbeya haijawahi kupata waziri kwa huyu mh. Sugu amewini kwani kapata uwaziri kivuli (kavinja mwiko)
 
Back
Top Bottom