Jiji la Dar linanuka kupindukia

Wakazi wa Dar wamezoea kinyaa![/QUOTE]

Sikubaliani na hitimisho hili.Kama mkazi wa Dar sijazoea na hakuna kubwa sana ninaloweza kufanya zaidi ya kuhakikisha mazingira yangu nayaweka safi na kwamba situpi uchafu au kufanya chochote kile cha kuchafua mazingira kwa kadri ya uwezo wangu.
 
Mbona umeelezea tu tatizo. Je kama ni wewe mjiji utafanya nini ili jiji liwe safi? its time to give na advice sio tu kuelezea matatizo. sorry if ofended

Ningefanya haya: 1. Nikikataza watu wasitupe taka mahali basi nitakuwa nimewatayarishia mahali pengine pa kutupa hizo taka zao na siyo kuweka tu matangazo: 'Hakuna ruhusa kutupa taka hapa. Manispaa.' 2. Miundombinu ya maji taka ijengwe kwa ubora na siyo mradi imejengwa na kuharibika baada ya muda tu. 3. Kuwepo usimamizi mzuri kwa kukusanya na kutupa taka. 4. Ukaguzi ufanyike mara kwa mara ili wale wanaotiririsha maji taka (kinyesi) kwenye mifereji usiku wadhibitiwe na wanaokaidi watozwe faini kubwa sana kwani hiyo ni mojawapo ya 'public nuisance offences'. 5. Kuundwe chombo madhubuti cha usimamizi au kuwepo na kampuni na watu 'serious' waajiriwe katika kuleta mabadiliko ya usafi wa jiji. 6. Magari chakavu yadhibitiwe na pia madereva wote wa daladala walazimishwe kuwa nadhifu. 7. Kujengwe 'public toilets' za maana na za kutosha jijini na zisimamiwe vizuri na pia kuwepo na matangazo makubwa wapi huduma kama hizo zinapatikana. 8. Maji na umeme viwepo muda wote na siyo kwa musimu kama ilivyo sasa hivi. Mfano, tangu kuanza kujenga barabara ya Kilwa wakazi wa Mbagala hawana maji ya bomba na haijulikani wataanza kuyapata mwaka gani au pengine yanasubiri kampeni za uchaguzi.
 
...Mkuu Magobe T, nawasilisha picha kuambatana na maelekezo yako, yote ikiwa kupigia msitari ukubwa wa tatizo linalotukabili!

ningefanya haya: 1. Nikikataza watu wasitupe taka mahali basi nitakuwa nimewatayarishia mahali pengine pa kutupa hizo taka zao na siyo kuweka tu matangazo: 'hakuna ruhusa kutupa taka hapa. Manispaa.'

View attachment 4266

2. Miundombinu ya maji taka ijengwe kwa ubora na siyo mradi imejengwa na kuharibika baada ya muda tu.

View attachment 4260
View attachment 4264

3. Kuwepo usimamizi mzuri kwa kukusanya na kutupa taka.

View attachment 4261

4. Ukaguzi ufanyike mara kwa mara ili wale wanaotiririsha maji taka (kinyesi) kwenye mifereji usiku wadhibitiwe na wanaokaidi watozwe faini kubwa sana kwani hiyo ni mojawapo ya 'public nuisance offences'.

View attachment 4267
View attachment 4262

5. Kuundwe chombo madhubuti cha usimamizi au kuwepo na kampuni na watu 'serious' waajiriwe katika kuleta mabadiliko ya usafi wa jiji.

View attachment 4265
View attachment 4263

6. Magari chakavu yadhibitiwe na pia madereva wote wa daladala walazimishwe kuwa nadhifu.

7. Kujengwe 'public toilets' za maana na za kutosha jijini na zisimamiwe vizuri na pia kuwepo na matangazo makubwa wapi huduma kama hizo zinapatikana. ...
View attachment 4259

...No wonder Mzee Mwanakijiji akajisemea "watu wa Dar es Salaam wamezoea Kinyaa!"
 
Mkuu Mbu naona umeongezea topic mpya of discussion.

Hebu tuijadili hii mada ktk picha, picha ya tatu kutoka mwisho ya huyu afande mwenye redi vest nyekundu.
 
Kama kuna mikoa au miji mingine kama Mwanza na Kilimanjaro wamefanikiwa, kuna maajabu gani waliyotumia ambayo viongozi wa Dar hawawezi kujifunza?
Aibu!
hee yaani mnakata gogo barabarani na kwingineko mnataka adam kimbisa afanyaje?

....jamani hata suala la usafi mnawalaumu viongozi?....wewe kuchimba choo na kuzingatia kanuni za afya unataka kiongozi aje akushike mkono?

....kuna wakati R Mengi alikuwa anatoa misaada kwenye hosp moja dar..akionyeshwa na ITV karibia dakika 10 akiwa wodini alisema ugonjwa wa kipindu pindu unatokana na kula mavi! akawapa misaada wagonjwa kisha akawaambia wawe wasafi(wasile mavi tena)

.....Zingatieni kanuni za usafi,msisubiri jiji kuja kuwajengea vyoo.....changishaneni nyie wenyewe pesa msafishe mitaa yenu..mnatoa michango ya harusi mpaka laki 5 mkiambiwa mtoe buku tu ya kununulia VIM ya ch.ooni hamtaki

Hitimisho.....wakazi wa DAR ES SALAAM wamezoea kinyaa/uchafu ni moja ya maisha yao...
 
Mkuu Mbu naona umeongezea topic mpya of discussion.

Hebu tuijadili hii mada ktk picha, picha ya tatu kutoka mwisho ya huyu afande mwenye redi vest nyekundu.

...naaaaaaam,

wanachoniudhi hawa kina "Rambo", huvamia kina mama ntilie, wauza machungwa, nk ...By the time lorry lao linafika kituo cha jiji, hakuna kidhibiti kilichobakia, ...weshaula ubwabwa na maharage, na kujipongeza kwa machungwa.

Kesho yake wanavamia mitaa mingine kujipatia mlo wa mchana!
 
hee yaani mnakata gogo barabarani na kwingineko mnataka adam kimbisa afanyaje?

...
....kuna wakati R Mengi alikuwa anatoa misaada kwenye hosp moja dar..akionyeshwa na ITV karibia dakika 10 akiwa wodini alisema ugonjwa wa kipindu pindu unatokana na kula mavi! akawapa misaada wagonjwa kisha akawaambia wawe wasafi(wasile mavi tena)

.....Zingatieni kanuni za usafi,msisubiri jiji kuja kuwajengea vyoo.....changishaneni nyie wenyewe pesa msafishe mitaa yenu..mnatoa michango ya harusi mpaka laki 5 mkiambiwa mtoe buku tu ya kununulia VIM ya ch.ooni hamtaki

Hitimisho.....wakazi wa DAR ES SALAAM wamezoea kinyaa/uchafu ni moja ya maisha yao...
View attachment 4272

...mama n'tilie huyu akichota maji ya kwenda kupikia ubwabwa! :(
 
Mbu hebu nifafanulie hapo ktk picha ya nne toka mwisho ambapo rambo wamemkomalia mlalahoi (sijui wanampeleka chumba cha sindano).
je huyo mjeda wa kike anajua mahala aliposhika ni jirani na mahala fulani anapootea ndoto kupamiliki?? ni mean ubebaji huu ni udhalilishaji, sasa akishika mhogo wa jang'ombe atalalama?
 
hee yaani mnakata gogo barabarani na kwingineko mnataka adam kimbisa afanyaje?

....jamani hata suala la usafi mnawalaumu viongozi?....wewe kuchimba choo na kuzingatia kanuni za afya unataka kiongozi aje akushike mkono?

....kuna wakati R Mengi alikuwa anatoa misaada kwenye hosp moja dar..akionyeshwa na ITV karibia dakika 10 akiwa wodini alisema ugonjwa wa kipindu pindu unatokana na kula mavi! akawapa misaada wagonjwa kisha akawaambia wawe wasafi(wasile mavi tena)

.....Zingatieni kanuni za usafi,msisubiri jiji kuja kuwajengea vyoo.....changishaneni nyie wenyewe pesa msafishe mitaa yenu..mnatoa michango ya harusi mpaka laki 5 mkiambiwa mtoe buku tu ya kununulia VIM ya ch.ooni hamtaki

Hitimisho.....wakazi wa DAR ES SALAAM wamezoea kinyaa/uchafu ni moja ya maisha yao...

..alisema ugonjwa wa kipindu pindu unatokana na kula KINYESI KISICHOCHEMSHWA! naomba kuweka kumbukumbu sawa hapo
 
..alisema ugonjwa wa kipindu pindu unatokana na kula KINYESI KISICHOCHEMSHWA! naomba kuweka kumbukumbu sawa hapo
Nakumbuka mkuu..alisema ugonjwa wa kipindu pindu unatokana na kula mavi....alisisitiza sana.....kisha akawakabidhi misaada wagonjwa..
 
Nakumbuka mkuu..alisema ugonjwa wa kipindu pindu unatokana na kula mavi....alisisitiza sana.....kisha akawakabidhi misaada wagonjwa..

kinyesi na mavi yote sawa ila kuna neno hapo mnalikwepa kuwa kinyesi kisichochemshwa. maajabu ya musa haya. kwa hiyo tukila kinyesi kilichochemshwa (na kuwekwa madikodiko) hatupati kipindua-pindu
 
...ukitua hapa,
hasa pale Arrivals ukisubiria kuonana na afisa uhamiaji/kusubiria sanduku lako toka kwenye conveyor belt, kuna 'kaharufu' fulani kanakeraaa! (...jua umefika nyumbani!)

View attachment 4279

...mbona ukitua hapa, unapambana na marashi ya karafuu na al Oud fulani hivi?...

View attachment 4278
 
Tatizo la uchafu DSM ni sisi wenyewe. Tuwawalazimishe watawala wasimamie sheria zinazohimiza usafi wa miji. Tuwawajibishe kama wakishindwa!
 
Back
Top Bottom