Jiji la Dar linanuka kupindukia

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Mara nyingi watu - wenyeji na wageni - wamekuwa wakilalamika kuhusu uchafu na kunuka kwa jiji letu la Dar es Salaam. Ukisafiri mitaa ya Dar es Salaam usiku harufu mbaya ya kinyesi inakera. Sijui ndio muda watu wanatiririsha kinyesi kwenye mifereji/mitaro ya maji! Kwa kweli hali hii inakera sana na sijui itaisha lini.

Nini kifanyike na hasa wahusika wawajibikeje pengine hawajui cha kufanya?
 
Dar ni jiji chafu nadhani kuliko miji yote TZ! Hakuna kujali maswala ya ustaarabu hata kidogo na wakati huohuo ndiyo makao makuu ya karibu kila kitu kinachoweza kusukuma mbele uwajibikaji na hata kufuata sheria.Uchafu wa Dar nionavyo mimi ni reflection ya hao wanaosimamia taratibu, sheria etc kwa maana ya mipango miji, miundo mbinu mbalimbali,sheria ndogondogo za jiji ( by- laws) etc.Iweje watu watiririshe maji machafu na hata kutupa vinyesi vilivyohifadhiwa kwenye mifuko ya plastik na serikali ifumbie macho? iweje watu watupe taka hovyo bila kujali, iweje watu watupe ovyo makaratasi, mifuko ya plastiki, wale mahindi, machungwa,miwa,n.k. na kutupa maganda na takataka nyingine ovyo barabarani?
Kama kuna mikoa au miji mingine kama Mwanza na Kilimanjaro wamefanikiwa, kuna maajabu gani waliyotumia ambayo viongozi wa Dar hawawezi kujifunza?
Aibu!
 
ukishakuwa fisadi unachoona ni kile kinacho kupa pesa tu wala huna shida na ustaarabu wa kusimamia sheria. Unadhani wakiamua kuna mtu atatupa kitu nje ya daladala? basi tu hawataki
 
Lakini na wakazi wa Dar inabidi wabadilike, lazima watambue kuwa hili ndio jiji kuu nchini. Unakuta mtu ananunua maji barabarani akiwa kwenye daladala, halafu akimaliza kunywa anatupa chupa/kopo la maji barabarani bila wasiwasi wowote !! Huwa nashangaa sana!! Au mtu ananunua miwa (hasa madereva) halafu anakula na kutupa makapi barabarani !!! Mtu kama huyu akiwa nyumbani hataona shida kufungulia maji machafu na kuyatiririsha miferejini.
 
Hilo nalikataa jiji la Dar Halinuki hapa nitaitetea serekali yangu kwa hilo ,tatizo ni vikwapa vya watu vikisha kuwa vingi ndio inachafuwa hali ya hewa na sio jiji kama unavyodai.
 
Hilo nalikataa jiji la Dar Halinuki hapa nitaitetea serekali yangu kwa hilo ,tatizo ni vikwapa vya watu vikisha kuwa vingi ndio inachafuwa hali ya hewa na sio jiji kama unavyodai.

...maji hakuna na umeme wa mgao unategemea nini? weka huduma nzuri ya maji vikwapa vitapungua!
 
Mara nyingi watu - wenyeji na wageni - wamekuwa wakilalamika kuhusu uchafu na kunuka kwa jiji letu la Dar es Salaam. Ukisafiri mitaa ya Dar es Salaam usiku harufu mbaya ya kinyesi inakera. Sijui ndio muda watu wanatiririsha kinyesi kwenye mifereji/mitaro ya maji! Kwa kweli hali hii inakera sana na sijui itaisha lini.

Nini kifanyike na hasa wahusika wawajibikeje pengine hawajui cha kufanya?

Eti magari ya kubeba taka yako wazi kabisa. Basi taka zote zilizobebwa na magari hayo hupeperusha na upepo badala ya kusafisha jiji wanazidi kulichafua na kuongeza uwezekano wa mlipuko wa magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama kipindupindu n.k.
 
...maji hakuna na umeme wa mgao unategemea nini? weka huduma nzuri ya maji vikwapa vitapungua!

Pia weka vikusanya taka vya kutosha mitaani, Magari ya kuzoa taka yauhakika yenye reliable and regular timetable, Himiza ustaarabu watabadilika tu.
 
Lakini na wakazi wa Dar inabidi wabadilike, lazima watambue kuwa hili ndio jiji kuu nchini. Unakuta mtu ananunua maji barabarani akiwa kwenye daladala, halafu akimaliza kunywa anatupa chupa/kopo la maji barabarani bila wasiwasi wowote !! Huwa nashangaa sana!! Au mtu ananunua miwa (hasa madereva) halafu anakula na kutupa makapi barabarani !!! Mtu kama huyu akiwa nyumbani hataona shida kufungulia maji machafu na kuyatiririsha miferejini.

Hilo ni kweli kabisa, lakini pia hakuna sehemu za kutupia taka barabarani unaweza ukatembea na hilo kopo lako la maji siku nzima ukakosa pa kulitupa!
 
Wavivu wa kufikiri, wanasubiri wabeba maboksi aka 'Educated TZ Immigrants in US in tough Situation' waje wawasaidie kusafisha uchafu wao.
Bongo tambarareeee...mji unanuka kinyesi LOL!!
 
Mara nyingi watu - wenyeji na wageni - wamekuwa wakilalamika kuhusu uchafu na kunuka kwa jiji letu la Dar es Salaam. Ukisafiri mitaa ya Dar es Salaam usiku harufu mbaya ya kinyesi inakera. Sijui ndio muda watu wanatiririsha kinyesi kwenye mifereji/mitaro ya maji! Kwa kweli hali hii inakera sana na sijui itaisha lini.

Nini kifanyike na hasa wahusika wawajibikeje pengine hawajui cha kufanya?

Mbona umeelezea tu tatizo. Je kama ni wewe mjiji utafanya nini ili jiji liwe safi? its time to give na advice sio tu kuelezea matatizo. sorry if ofended
 
Kweli mji wa dar ni mchafu, mimi nilikuwa siamini. kuna kipindi nilisafiri kwenda huko Ughaibuni, kufika huko nikakuta hewa nyepesi na nzuri. Ukafika muda wa kurejea home, e bwana si mchezo, natua tu na ndege pale air port ya Dar nikaona ghafla hewa nzito na kuna kiharufu fulani cha kunuka. Kweli mji wa dar kwa usafi bado kabisaaa!!!!!!
 
Matatizo ya Jiji ni complex kidogo.inabidi kyaainisha one by one
1. poor infrastructure- barabara ni za zamani, hazitoshi kulingana na mfumuko wa uingizaji magari. pollution kibao!!!
2. poor/ none housing planning- nyumba za Dar zinaota kama uyoga hakuna facilities zozote i.e maji, umeme, mifereji ya maji taka n.k hivyo mlundikano wa nyumba kunafanya uchafu usikusanywe sawsawa
3 Hakuna strategy madhubuti za ukusanyaji taka. kuanzia house hold mpaka katika industrial waste hapa ndio kasheshe maana watu majumbani je uchafu kuanzia wa vyooni, vyakuala n.k maji machafu vinatupwa wapi?
4. Culture ya kutojali- Wakaaji wengi wa jiji hawajali kabisa mazingira. wanadhani utunzaji wa mazingira ni kazi ya mtu fulani. na hii ndiyo mbaya zaidi. Maana mtu annamua kunya anywhere, kukojoa popote, kutupa taka kiholela, mifereji ya maji machafu ya vyoo na misalani just kuelekea bondeni!!

4. Usimamizi bomu- Jiji likiwa chini ya serikali za mitaa ni wazembe, wanachojua ni kukaba watu koo kulipa kodi tu! hakuna mikakati tekelezeki ya usafi wa jiji. Mikakati mingi ipo katika katika paper work. hadithi mlima. JE si mnamkumbika Keenja? alijitahidi mpaka akaukwa ubunge!!! Jiji linahitaji mtu makakamavu, hodari, shujaa kwelikweli, makini, mchapa kazi MKALI ili kuwaswaga maofsa wa jiji na wananchi kusafisha Jiji.
I.e Ni kwani ni kila nyumba isiwe na pipa la takataka? a) za kawaida b) recycling
2. Ni kwa nini kila mtaa usiwe madhubuti kuhakikisha kuwa mtaa wao ni safi ikiwa ni pamoja na kuripoti yeyote anayeshisiwa kuchafua mazingira?
3. Ni kwa nini kisitengwe maeneo ya recycling? maana takataka nyingi zinaweza kuwa recycled i.e mabaki ya vyakula kama mbolea. etc etc.
 
Title ya thread inatakiwa isomeke Wakazi wa Dar ni wachafu kupindukia. .and this is the bottomline. The rest of the story ni kutupiana mpira tu hakuna substance.
 
Kweli mji wa dar ni mchafu, mimi nilikuwa siamini. kuna kipindi nilisafiri kwenda huko Ughaibuni, kufika huko nikakuta hewa nyepesi na nzuri. Ukafika muda wa kurejea home, e bwana si mchezo, natua tu na ndege pale air port ya Dar nikaona ghafla hewa nzito na kuna kiharufu fulani cha kunuka. Kweli mji wa dar kwa usafi bado kabisaaa!!!!!!

Hiyo ni kweli tupu hewa ni nzito sana halafu kuna njemba zinawasha mioto ya kuchoma taka kila jioni basi hili nalo huchangia sana katika uzito wa hali ya hewa. Mrema alipokuwa mambo ya ndani aliwahamasisha wakazi wa Dar na jiji likaanza kuwa safi. Nafikiri kuna haja ya kuwa wakali na kuweka faini kubwa kwa yeyote yule anayechangia katika uchafuzi wa jiji kama kutupa takataka bila mpango n.k. ikiwa ni pamoja na makampuni na watu binafsi.
 
Hilo nalikataa jiji la Dar Halinuki hapa nitaitetea serekali yangu kwa hilo ,tatizo ni vikwapa vya watu vikisha kuwa vingi ndio inachafuwa hali ya hewa na sio jiji kama unavyodai.

Kusema jiji la Dar es Salaam halinuki siyo kuitetea serikali yako ni kuikana na kutotaka kuwepo mabadiliko katika nchi yetu. Watu kama wewe ndio wale wanaoficha maovu wakidhani kuyasema ni kukosa uzalendo kwa nchi yao. Kwani hao wanaonuka vikwa ni wa nchi gani au serikali yao ni ipi?
 
Back
Top Bottom