Jiji la Dar es Salaam na kero ya usafiri

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,376
3,823
Kwa kero hii ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam tunaweza kweli kuendelea?
Kila siku inanichukua masaa manne hadi matano kwenda na kurudi kazini. si mimi peke yangu bali walio wengi wanakerwa mno na usafiri wa Dar es Salaam.
Tunaweza kujiuliza maswali machache tu kama vile: je,watu wanaotumia usafiri huu wanazalisha kiasi gani na je, ikiwa kusingekuwa na kero hii hali ya uzalishaji na utendaji ingekuwa vipi? Je,mafuta yanyoongezeka kwa magari kukaa barabarani ni kiasi gani na yanaliingizia taifa kiasi gani cha hasara? Mtu akiweza kukokotoa mahesabu vizuri kabisa anaweza kugundua kuwa taifa linapata hasara kubwa kuliko fedha zinzopatikana kutokana na kuuza mashirika yetu. ingawa watanzania kwa ujumla wao wana kero nyingi lakini la usafiri katika hiki kitovu cha biashara na uchumi limezidi.TUNATAKA WALE WOTE WANAOTAKA UONGOZI WAELEZE PASIPO SHAKA NI JINSI GANI WATAVYOKABILIANA NA VIKWAZO VYA MAENDELEO KATIKA TAIFA LETU. KWA DAR, KUBWA NI USAFIRI!
 
TUNATAKA WALE WOTE WANAOTAKA UONGOZI WAELEZE PASIPO SHAKA NI JINSI GANI WATAVYOKABILIANA NA VIKWAZO VYA MAENDELEO KATIKA TAIFA LETU. KWA DAR, KUBWA NI USAFIRI!

Hii ni sera tayari umetoa Mzamifu, jamani tukitumieni kama kipimo cha kuwapa kura zetu.
 
Back
Top Bottom