Jiji inusuruni manzese

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Kuna habari zilielezwa wakati ule Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson alipotembelea Dar es Salaam kwamba bila kuficha alisema mji unanuka, baadhi wakamponda kwamba ana nyodo.
Amini usiamini pita Manzese sasa hivi barabara yote toka stend ya mkoa mpaka Mwembechai kuna harufu kali sana hii inatokana na mfereji uliojengwa pembeni ya barabara kutumika kumwaga maji taka ya vyoo.
Noma ni pale siku kukitokea magonjwa ya mlipuko, ndugu zetu hawa wataumia na majirani wa karibu. Hivi Jiji hili mnaliona? Hivi cheo cha Bwana afya kilifutwa? wanajamvi hili linawagusa na ninyi?
 
Sasa hivi ni muda wa kampeni bana...serikali iko likizo ya muda!...lol!:smile-big:

Bahati mbaya sana kipindi kama hiki mambo mengi yanaachwa holele bila kufuatiliwa!...Arusha kwasasa kila mahali pametandikwa mitumba na mbogamboga, hakuna mtu anayeulizwa, mgambo wameambiwa wasimbugudhi yeyote..ndio madhara ya serikali ya second-hand!
 
Paka,..
ni kweli nguvu zimeelekezwa kwenye kampeni, ila kila baya linaloachiwa litokee sasa kwa kigezo cha kutobughuzi wananchi ili kuwarubuni wanapendwa, madhara na gharama yake ni kubwa sana awamu ijayo. ngoja turudi tena uone mgambo hao hao watakavyokuwa mbogo kuwaondoa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom