Jiji chafu na linanuka.....lol

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
dsc01203.jpg


Makutano ya Mtaa wa Amani na Congo,Kariakoo.
 
hii ndio BONGO kila kitu ni kero tu. halafu juzijuzi nilisikia halmashari ya wilaya ya ilala wamepata magari mapya ya kuzoa takataka, au ndio yanapeleka michanga na kokoto kwenye site zao waheshimiwa wetu?
 
dsc01153.jpg

Hili ni eneo la Posta mpya,usoni kabisa mwa jengo la Haidery Plaza ambapo kuna mashimo makubwa sana yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara za chini kwa chini ili kuwezesha kupungua kwa msongamano wa magari katikati ya jiji.
 
dsc01157.jpg

Dereva wa gari hilo akimpigia mkandarasi wa ujenzi huo kumwambia kuwa mambo bado hayajakaa sawa katika eneo hilo.
 
dsc01158.jpg

Baadae Msaada tutani ulibidi uchukue nafasi yake ili kufanya mambo mengine yaende kama yanavyotakiwa.

HII NDIO BONGO DASLAMAA NA HUU NDIO MPANGOOOO.

 
hivi miaka hamsini ya uhru twasherehekea nini?///////////////////////POVERTY and things poverty can buy....................................
 
Nguvu Muda na rasilimali wanazotumia kufukuza kukamata kuwashitaki na kuwafunga wamachinga zingetumika kwenye usafi huu mji ungekuwa afadhali. Ukienda mahakama ya jiji utakuta kosa la wapiga debe jela mwezi mmoja. Government hospitality at no cost at all, wakati kama wakamataji na waendesha mashitaka wangekuwa na akili wangewapa community services.

Mkuu, eyesores ziko kibao, just to mention a few, Pitia Railway Station aka Relwe jirani na geti ambalo mabasi ya relwe yalikuwa yanaingilia nia aibu, mwenge nako karibu na kituo cha mabasi, kawe opposite Tanganyika packers Hizi zote ni official dumpsites.

Halafu mameya wanatembea na mercedes metalic, kwenye barabara zenye kinyesi na mashimo sawa na mahandaki, huku wakifunga vioo vya magari ili wasisikie harufu ya takataka zilizojaa kila mahali mjini. Ambazo zimesababishwa na uzembe wao.
 
Hawa viongozi wetu nadhani wakifunga vioo na kwasha AC zao katika magari yao (yenye kuvutia na bei kubwa toka katika kodi zetu),MACHO YANAJIFUNGA AUTOMATICALLY kuona uchafu na ushenzi wote ulio katika TUZIITAZO barabara zetu....

Kwa wakati tofauti nimeona uzinduzi wa magari mapya ya kubeba uchafu (tokea mwaka jana robo ya kwanza)...Mchango wa magari hayo kiukweli sijauona kama ilivyo kwa magari mapya (wakati yalipotambulishwa kwetu wananchi kupitia vyombo va habari) ya ZIMAMOTO YA HALMASHAURI YA JIJI NA MANISPAA ZAKE
 
Kwa kweli nashukuru sana kwa hizi pics,jamani kama hata taka kuzitoa ni kazi je ni nini tunachoweza,eti miaka 50 ya uhuru,kweli tunahitaji kujifunza kufikiri zaidi,kwa wachaga ukishndwa hata kufagia mbenge yako ni aibu,
 
Back
Top Bottom