Jihadhari unapokuwa maeneo haya Dar es Salaam

Ocean road hakufai, waliwahi nipora kasimu kangu ka tochi na vihela...
 
Asanteni kwa taarifa, sisi wengine wageni tutazidi kuchukua tahadhari, japo tulishatahadharishwa hata kabla hatujafika! Kiufupi huu mji wenu sio, hata mtu anaekufahamu anaweza akakuliza, aidha kwa kukuibia, ulaghai, utapeli ama ilimradi dhuluma tu. Si mbaya tutawaachia jiji lenu mmalizane wenyewe
 
Kijitonyama, Sinza na Mikocheni:
Mitaa ya Sayansi, Makumbusho na Maeneo ya Mikocheni Rose Garden ni hatari sana kwa kina dada na kina kaka ambao huninginiza mabegi ya laptop na mapochi makwapani mwao.
Kuna kundi la vijana linatumia magari kukwapua mabegi na mapochi hayo.
Wanachofanya ni kwamba dereva anapunguza mwendo na kukusogelea kisha abiria aliokuwa nao hukwapua mikoba hiyo na kukimbia.
Simu pia huibiwa kwa mtindo huo.

Mbagala:
Mitaa yote ya Mbagala Charambe, Hadi Kiburugwa hi hatari sana kwa kuwa kuna kundi la vibaka linaloitwa Mbwa Mwitu. Kundi hili hupora fedha, simu na kila ulichonacho hadi viatu. Ukikutana nao wanakushambulia kwa vipisi vya nondo na kukuibia huku wakikuacha huna fahamu.

Girrafe Hotel:
Kwenye maegesho ya hoteli hii ni hatari sana kwa wenye tabia ya kuacha mali za thamani ndani ya magari yao.
Kuna kundi la vijana likishirikiana na walinzi wa hoteli hiyo, huvunja vioo vidogo ya nyuma sehemu ya kiti cha abiria, hung'oa power windows na kuchukua kila wanachoweza.
Hoteli imekuwa ikijibu wanaoibiwa kuwa hapa kwetu Parking is at owners risk.

Posta:
Maeneo haya ni hatari kwa wanaotumia daladala na wale wanaogesha magari sehemu mbalimbali za katikati ya jiji hili.
Watumia daladala wa Posta huibiwa pesa na simu zao zilizomo kwenye mikoba na mifukoni wakati wakiwa wanagombania magari mida ambayo usafiri huwa mgumu.
Wenye magari huibiwa vitu kama power windows na laptop ikiwa utaacha ndani ya gari. Na wezi wakubwa ni vijana wanaozagaa maeneo ya maegesho.

Bonde la Jangwani, Selander Bridge na Bonde la Kigogo:
Maeneo haya ni hatari kwani hamna makazi, hivyo vibaka hutumia mwanya huo kufanya uhalifu mchana kweupe, na usiku maeneo haya ni hatari zaidi.
Ukipata pancha maeneo ya jangwani nakushauri utembelee ringi hadi eitha Faya au Magomeni Mapipa ambapo pana watu na pana usalama.
Vibaka hutokea kwa staili ya kukupa msaada na mwisho wa siku hukuacha ukiwa huna kitu na huku gari yako ikiwa skrepa.

Sea View, Ocean Road na Viwanja vya Golf Gymkhanna Club:
Maeneo haya kuna vibaka hatari sana ambao hushambulia kwa kikundi na kupora mali zote na kukuacha ukiwa majeruhi.
Maeneo haya yametulia sana na yanaonekana ni salama sana kwani yako jirani na ikulu, lakini hayana usalama wowote na ni hatari kabisa.
Usipite maeneo hayo kwa miguu mida ya kuanzia saa kumi na mbili na nusu giza likiwa linaingia, maana utakumbwa na dhahama.

Polisi wanayajua maeneo yote hatari kwa raia, lakini haiboreshi ulinzi maeneo hayo na wala haiwatahadharishi wananchi.
Cha kufanya ni sisi kutahadharishana. maeneo hatari hapa Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla yapo mengi sana, naomba na wenzangu muyaongeze maeneo ambayo sijayataja hapa.
Duh!
 
Hivi Magari na polisi walioongezwa wakati wa uchaguzi hawawezi kuwadhibiti hawa dogs?
 
Kuna siku nisikia kibaka akisema yeye haibagi mnazi mmoja yeye ni karume ndio maskani yake kwa hiyo tukio la wizi wa sim mnazi mmoja hausiki kabisa.
 
Back
Top Bottom