Jihadhari na hizi barrier za polisi from arusha to dar

Nduka Original

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,012
816
Du wakubwa kuna hizi barrier zinakera sana unapo drive toka Arusha kwenda Dar or other way round.

1. Daraja la Nduruma yani hawa jamaa wanakera sana ila uzuri wao kama kuna malori yakutosha hawasumbui
2. KIA - Hawa jamaa nao wanakera sana tena kuna traffic mmoja white huyo anasimamisha magari mpaka mengine anasahau
3.Mombo - Hawa wafaiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. ni wale wanaokaa pale kwenye bump
4. Korogwe - Wale wanakaa pembeni ya travelers Inn kama unakwenda stand kuu
5. Msata - Hawa nao ni nuksi
6
7
8
9
 
Wa kabuku ndio komesha wanakula ruswa ya madawa ya kulevya toka tanga kwa kwenda mbele
 
umenichekesha sana! eti anasimamisha mpaka mengine anarahau kama kasimamisha... huyo soo
 
kuna sehemu moja inaitwa kitumbi, wanapapenda sana wale wenye tochi, wala rushwa sana, washakula buku 5 zangu kama 10 ivi, maana watalazimisha mpaka wakukute na kosa, hata kama sio la kuzidisha spidi 50 kwenye kamji kale
 
hawa jamaa nasikia wanacheza kibati/upatu kila siku kwa mtu utoe laki hawataacha kula rushwa sijui mwema kama analifahamu hilo
 
Kuna Ruvu Darajani, pale kuna Polisi mmoja mchaga kwa rafidhi yake ana Moustach, na kifimbo, ni Copral au V mbili, huyo akikagua gari hata huna kosa anaomba basi umwachie hata ya soda, nikamwuliza kama shida yako ni soda kwa nini unisumbue na kunipotezea muda wote huu? Mara lete fire extinguisher, license, card ya gari, triangle n.k.?
 
Tunashukuru kwa taarifa hizo maana nitapita wiki ijayo naenda ARUSHA tutapambana nao tu.
 
Ha ha ha,nilikuwa na familia yangu tukitoka arusha kurudi dar, hiyo timu ya korogwe ikatusimamisha. Tulikuwa na mwanangu wa miezi 5 amebebwa na mama yake, ile kioo kinafunguliwa tu Mwanangu huyo aliachia kilio kikali sana hata sikujua ni nini. Polisi walishangaa na kutuambia hebu nendeni na malaika wenu msije mkatuharibia siku bure.

Nilisheka sana. Ila hii njia inakera sana, wanaka highway nzuri halafu wanakutaka utembee speed 30 kitu ambacho sio uhalisia kabisaaa. wamejiwekea mazingira ya kujipatia pesa (rushwa)
 
Hawa jamaa wa ajabu sana juz wametumsmamisha walvyoona hatuna kosa mmoja akainama chini ya gari akasema"mbona hii drai shafti inakata kiuno"
 
hawa jamaa ni balaa jana nimekutana nao toka arusha mpaka Dar sina hamu mtu ana kusimamisha anaangalia kila kitu uko safi mwishowe kitunguu nyanya chumvi inahu
 
Jamaa walishanisimamisha Korogwe na baada ya kukagua gari na kukuta haina kosa (maana ilikuwa Land Cruiser brand new)mmoja wao akaniuliza mbona driving licence yako imepauka...............
 
Back
Top Bottom