Hivi kuagiza camera mfano canon 5d na kisha utumie njia ya posta ya kawaida si risky kubwa sana?
Ni risk ndiyo kama mzigo wako utakuja kwaida kwa kutumia international mail postage.
Lakini unaweza kupunguza hiyo risk kwa kutumia tracking postage.

Mzigo wako utakuwa tracked katika kila kituo ambacho umepitia mpaka kukufikia wewe mtu wa mwisho. Na unaweza ukaongea na Seller wako akakutufutia best shipping method you can afford.
 
Katika bidhaa kuna bei imeandikwa pale, je kuna uwezekano wa ku-bargain ili kupunguziwa bei kwa namna moja au nyingine.

Kama jibu ni NDIO, je manunuzi yatakuaje baada ya seller kupunguza bei na kuwa tofauti na ile iliyoandikwa pale amazon/ebay/ alibaba n.k.
 
Nimejifunza jambo zuri sana hapa, ambalo kwa kweli nilikuwa ni kipofu katika hili. Je, MasterCard na Visa card ipi ni bora katika manunuzi ya mtandaoni?
 
Nimejifunza jambo zuri sana hapa, ambalo kwa kweli nilikuwa ni kipofu katika hili. Je, MasterCard na Visa card ipi ni bora katika manunuzi ya mtandaoni?

swali gumu kidogo ila kwa ufahamu wangu mastercard ni bora zaidi kuzidi visa kaka.. mastercard ina huduma nyingi kuliko visa ila kwa upande wa online shopping zinakuwa na same value kwa maana karibu masoko yote wanakubali visa na mastercard.. hivi karibuni naona visa inazidi pukoteza support ila still sio mbaya,, to be safe nakushauri go for mastercard...
 
Kwa seller ambaye hatumi mizigo tz nimetumia campany ya SHIPITO ni nzuri sana na bei zao ni cheap sana

Unazionaje huduma za SHIPITO mkuu.. nikikuomba rate yako ya huduma uliyo pata utairate ngapi out of ten
 
Unazionaje huduma za SHIPITO mkuu.. nikikuomba rate yako ya huduma uliyo pata utairate ngapi out of ten

Kwa SHIPITO naipa 8/10 kwasababu
1.gharama zao zipo chini sana.
2. Wanatumia Paypal kufanya malipo
3.wanakupa option nyingi za kutumiwa mzigo wako kuanzia dollar $3 mpaka dollar $65 ni wewe tu unauwaraka kiasi gani na unapenda njia gani.
4.wanakutumia mzigo wako hata kama hauna hela kwenye akaunti yao.
5. wako fasta sana mzigo ukifika kwenye warehouse yao wanakutumia email kuwa kuna mzigo wako haizidi dakika 15 baada ya mzigo kuwafikia
6.wanaonline chat ambayo muda wote wapo online na unasikilizwa 24 hrs.
 
swali gumu kidogo ila kwa ufahamu wangu mastercard ni bora zaidi kuzidi visa kaka.. mastercard ina huduma nyingi kuliko visa ila kwa upande wa online shopping zinakuwa na same value kwa maana karibu masoko yote wanakubali visa na mastercard.. hivi karibuni naona visa inazidi pukoteza support ila still sio mbaya,, to be safe nakushauri go for mastercard...

Asante kaka kwa ushirikiano wako. Nimekupata sasa.
 
Kwa SHIPITO naipa 8/10 kwasababu
1.gharama zao zipo chini sana.
2. Wanatumia Paypal kufanya malipo
3.wanakupa option nyingi za kutumiwa mzigo wako kuanzia dollar $3 mpaka dollar $65 ni wewe tu unauwaraka kiasi gani na unapenda njia gani.
4.wanakutumia mzigo wako hata kama hauna hela kwenye akaunti yao.
5. wako fasta sana mzigo ukifika kwenye warehouse yao wanakutumia email kuwa kuna mzigo wako haizidi dakika 15 baada ya mzigo kuwafikia
6.wanaonline chat ambayo muda wote wapo online na unasikilizwa 24 hrs.

Ungetoa ufafanuzi zaidi kuhusu hao SHIPITO
1.Gharama ziko chini ukilinganisha na zipi ?
2.Paypal nafikiri karibia kampuni zote wanatumia paypay

3.Wanatumia vigezo gani kucharge gharama zao,wanaangalia uzito wa mzigo,thamani ya mzigo,nchi uliyopo?

Kama ikiwezekana ungetupa simu au link ya website yao
 
Imekuwa ni shida sana kwa watanzania wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania. baadhi ya thread zilianzishwa na zimeelezea mengi sana kuhusiana na manunuzi haya ya mtandaoni, ila tulipata ufumbuzi mdogo. Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi. hii ni kwa kutumia FOWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni 1: Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri marekani au uingereza UK) au US Shipping Address 2:Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia (eidha amazon,ebay au lolote lile lisilo ship Tanzania) 3:Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL,FEDEX,UPS,USPS NK baada ya kujua kazi ya fowarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo (kwa wageni wasiofahamu/hawajapitia previous threads:

1:CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana almost bank zote hapa Tanzania (kasoro NMB sina uhakika), ni kadi yeyote ya visa au mastercard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni(online purchases) na mara nyingi huchukua maximum 24hours kuactivate.

2:KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa paypal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.

3:KUJIUNGA NA FOWARDING COMPANY

Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi fowarding company na kujiunga (sighnup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma... nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi

4:KUTAMBUA SOKO BORA LENYE HUDUMA NZURI(ONLINE MARKET)
Hapa tunazungumzia website za masoko kama ebay,amazon, bestbuy, apple.com, dell.com, toshiba.com nk.. masoko haya ndipo utakapo nunua bidhaa yako.

PROCESS NZIMA KUANZIA UNANUNUA MPAKA MZIGO UNAKUFIKIA IKOJE?
hii iko hivi.... 1:Ingia katika soko lako ulilolichagua au unalopendelea, hapa nasuggest kutumia sana amazon(ndilo ninaloliamini) amazon ukiingia utakuta bidhaa nyingi ila kuwa makini kuchukua zile bidhaa zilizo na alama ya prime chini...alama hiyo inamaanisha kuwa huo mzigo unauzwa, utapakiwa, na kutumwa na amazon wenyewe, so no utapeli hapo, yani u get what u wanted. 2:Nunua na kuagiza kitu kwenda kwenye address ya fowarding company ulioichagua, hivyo mzigo ulioununua utaenda moja kwa moja kwenye company yako, wao wakishaupata watakutumia e-mail uthibitishe au uchague courier wa kukutumia mzigo wako, hapo ndio utachagua either dhl,ups,fedex nk.wao watakutumia na kuchukua kiasi chao cha pesa ya huduma na kukutumia mzigo pamoja na kukupatia tracking number ya kujua mzigo wako ulipo na utaupokea vyema.

FOWARDING COMPANIES ZENYEWE:

1: MYUS.COM link- MyUS.com - #1 International Shipping, Mail and Package Forwarding Service - MyUS.comhii ni company niliyoitumia na nina expirience nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wana charge pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika upesi sana bila ya zengwe lolote.
Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga na huduma zao
Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,

2:COMGATEWAY
link-http://comgateway.com/ hawa pia ni fowarding company nzuri sana (thanks tu Mwl.RCT), nimepitia site yao na uona wana policy nzuri sana,cha kwanza ni sales tax-free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi marekani,hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courie DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi.pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus..

3:BORDERLINX
link- Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ... wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia..hawa pia hawana registration fee na wanakupa option tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.

4:SHIPITO
link-USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com | English hii pia ni kampuni kongwe ya fowarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao

5:STACKRY
link- Stackry - US shopping, global shipping hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mabo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao. waungwana ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mabo kabla ya kuchukua uamuzi. STACKRY na BORDERLINX walikuwa recommended sana na wanasifiwa mno angalia hii link -http://tech-vise.com/10-parcel-forwarding-services-for-international-shoppers/ pitia hizo websites na ujionee mwenyewe chagua moja na utazame kama wanakufaa.

HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI WAKUU please evaluate kindly.

nilikuwa nataka kuonyesha steps ila naona thread haitoshi . maana nimeagiza mzigo na nimechukua hatua zote ili mpate kuona ila ithink there r limits.. help Mwl.RCT

nashukuru mkuu kwa kuniongezea vitu vipya......!!!
 
Ungetoa ufafanuzi zaidi kuhusu hao SHIPITO
1.Gharama ziko chini ukilinganisha na zipi ?
2.Paypal nafikiri karibia kampuni zote wanatumia paypay

3.Wanatumia vigezo gani kucharge gharama zao,wanaangalia uzito wa mzigo,thamani ya mzigo,nchi uliyopo?

Kama ikiwezekana ungetupa simu au link ya website yao

link yao ni www.shipito.com nawapenda kwasababu hawana pesa ya kufungua acc na wanacharge mzigo kutokana na uzito kama kampuni nyingine wanavyofanya ila wana option nyingi sana kuanzia za bei rahisi sana mpaka za bei kubwa tofauti na kampuni nyingine utakuta kutuma mzigo kutoka marekani lazima utumie FEDEX au DHL.
 
Safi sana hii

huu uzi ni mzuri sana mimi mwenyewe nilijifunzia hapa hapa nikajaribu na nimefanikiwa na nilichogundua wenzetu wazungu waaminifu sana siyo kama sisi waafrika kwaiyo msiogope kujaribu. japo unatakiwa uwe makini pia.
 
Hii kitu imetulia, nilishajaza fomu husika kupata huduma hii, Leo hii naiwakilisha banki inayohifadhi madafu yangu.
 
Mwenye uzoefu na gari za mazda demio anipatie. Intems of spare je kwa nchini zinapatikana? Je zipo kama IST au swift kwa ukubwa.
 
Nahitaji kujua juu ya Matumizi ya PayPal Account!!! Hasa katika Kuweka au tuseme Ku-Add hela Kwenye akaunti yangu ya PayPal.
 
Mwenye uzoefu na gari za mazda demio anipatie. Nataka kujua spare zake zinapatikana hapa Tanzania kwa urahisi au gharama ni kubwa sana?
 
Back
Top Bottom