chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,961
Annie Nyaga amefanya kitu ambacho kimebadiisha fikra za watu wengi hasa vijana wa kiafrika,na hii ilikuja baada ya jina lake kuchomoza katika orodha ya vijana mamilionea nchini Kenya wakati huo akiwa hajulikani na mtu yeyote kabisa.Akiwa na digrii yake ya kwanza ya Biomedical Science and Technology kutoka chuo kikuu cha Egerton aljikuta amekataa scholarship aliyopewa ya kwenda kusoma Marekani ili aiishi ndoto yake ya kuwa mkulima.Annie wakati ameibuka kuwa milionea alikuwa ni binti kijana wa miaka 29 lakini maisha yake yamebadilika sana kwa kuamua kuishi kitu ambacho moyo wake ulikuwa unakitamani kila siku.
Annie kwa sasa haishi mjini,anaishi kijijini kwake kwa asili Mbeere,Embu Kaunti ambako analima matikiti maji,nyanya pamoja na mazao mengine.Kwa sasa shamba lake limekuwa la kisasa likiwa na mashine mbalimbali na wafanyakazi kadhaa walio chini yake,yeye akiwa ni mkurugenzi wa kampuni yake aliyoianzisha ya Farm2Home.Kabla ya kuamua kuwa mkulima Annie alikuwa ni afisa ugavi na baadaye alikuwa anatembeza bidhaa kuuza kwenye maduka mbalimbali jijini Nairobi kama ambavyo vijana wengi wanafanya katika miji mikubwa.
Habari ya Anne inafanana na maisha ya watu wengi sana na kuna mambo kadhaa ya kujifunza kutoka katika maisha yake.
Moja ni kuwa,pamoja na usomi wake Annie aliamua kuiishi ndoto yake;yaani lile jambo ambalo alikuwa analiota kulifanya tangu akiwa na umri mdogo.Hakuruhusu masomo aliyosoma chuo kikuu yawe ni kikwazo kwa yeye kuifuata ndoto yake.Elimu kazi yake ni kutupa maarifa ya ziada ili tufanye kwa ubora mambo tuliyoamua kuyaishi.Kuna watu wengi leo ndani ya moyo wao kuna kitu wanatamani kufanya lakini wameendelea kung’ang’ania kukabwa na taaluma zao eti kwa sababu tu walisomea.Ni lazima ujue kuwa watu wanaofanikiwa haraka ni wale ambao wanafanya kitu ambacho kinagusa moyo wao,wanaishi katika “Passion yao”.Usione haya kufanya kazi inayoonekana sio ya kisomi lakini ina utajiri ndani yake.
Annie anatufundisha kuwa tusifuate mkumbo wa maisha.Ni kawaida kwa vijana wengi kung’ang’ania mijini mara baada ya kumaliza masomo yao vya vyuo.Unakuta miezi kwa miezi,wengine hadi miaka,wengine wanathubutu kukataa nafasi za kazi eti kwa sababu ziko mikoa mingine toafuti na Dar es Salaam ama sio kwenye miji mikubwa.Kuna fursa nyingi kila mahali,usiwe mtumwa wa fikra kuwa ili ufanikiwe lazima urundikane kwenye miji na wenzako.Angalia ndoto yako,usijali wengine watasema nini,chukua hatua mara moja na anza kuiishi.Annie aliacha kazi toka kwenye kampuni ya mauzo na kwenda kuanza kuishi ndoto yake kijijini.Na leo amefanikiwa kuliko wengi aliowaacha mijini.Suala sio unaishi wapi,suala la muhimu ni kama uanfanya jambo ambalo ndio ndoto ya maisha yako.
Inashangaza kuona kuna watu wanang’ang’ania kukaa mijini eti kwa ufahari tu kwamba wanaishi kwenye majiji lakini ukichunguza kazi na kipato wanachopata ukweli ni kuwa wanasurvive(wanasukuma siku) wakati kama wangeamua kuchukua fursa zilizoko nje ya miji wangefanikiwa.Usiwe mmoja wao.Kwa sasa Annie ni milionea anayeishi kijijini.Hivi jambo zuri ni lipi?Kuishi kitajiri kijijini na ukawa na uwezo wa kuja mjini wakati wowote unaotaka tena kwa ndege ama kuishi mjini huku ukiugulia maumivu ya maisha na hata mzazi akiomba hela ya vocha hauna?Uchaguzi ni wako.
Jambo lingine analotufundisha Annie ni ukweli kuwa tunahitaji kuwa wavumilivu ili kutimiza ndoto zetu.Katika mahojiano Annie alieleza kuwa amekutana na changamoto mbalimbali ikiwezo ya kubadilika kwa bei ya mazao yake na pia ukosefu wa mvua za wakati.Kiufupi ni kuwa hakuna ndoto ambayo haitakabiliwa na changamoto utakapoanza kuitekeleza.Ni lazima ufanye uamuzi tangia mwanzo unapoanza kuchukua hatua kuwa hautakata tamaa.
Ni lazima ujue kuwa kuna watu watakucheka,wengine watakudhihaki,wengine watakushangaa lakini kama ni ndoto umeiamini ni lazima uamue kukabiliana na vitu vyote hivyo katika maisha yako.Jiulize?je unaishi ndoto yako leo?ama unaishi maisha ya kuwafurahisha wengine huku ndani yako unaumia?FANYA MAAMUZI.
Mafanikio ya kweli yanaanza pale unapokuwa na ujasiri wa kuchukua hatua za kuanza kuiishi ndoto yako.
Endelea kutemebelea www.JoelNanauka.Com ili kujiifunza Zaidi na unaweza kulike ukurasa wangu wa facebook ili kupta mafunzo na pia unaweza kujiunga kwenye watasapp group ili kupata amafunzo bure.Tuma Majina yako kamili na neno “ndoto yangu” kwenda 0655 720 197.
Kumbuka kuwa ndoto yako inawezekana,