Jifunze kufunga Tai na sheria zake baada ya kuvaa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,
Nimeona ni vema leo tukajuzana namna ya kufunga tai kwasababau nimekutana na wadau kibao wanakwambia hawavai tai eti kwasababu hawajui kufunga, pia hata akina dada nivema mkajua kufunga tai ili kuwasaidia wenzi wenu. Kwa mfano kwetu sisi Baba alitufundisha kufunga tai kuanzia Mama na watoto wote wakiume na wakike na tukawa fiti kabisa.

Jifunze kupitia video hii:






Lakini baada ya kuvaa zingatia sheria na kanuni zifuatazo
*Hairuhusiwi kuvaa kandambili
  1. Hairuhusiwi kuuliza muda kwa mwenzako

  2. Hairuhusiwi kusema nimeishiwa fedha

  3. Hairuhusiwi kukimbiza mwizi

  4. Hairuhusiwi kula gengeni au kwenye hitima

  5. Hairuhusiwi kupanda lori

  6. Hairuhusiwi kujisaidia uchochoroni

  7. Hairuhusiwi kupiga miayo kwa njaa

  8. Hairuhusiwi kupiga kelele ukishaibiwa

  9. Hairuhusiwi kuvaa nguo zisizonyooshwa

  10. Hairuhusiwi kuyumba kwa ulevi barabarani

  11. Hairuhusiwi kupanda baiskeli

  12. Hairuhusiwi kuacha nywele ovyo ovyo

  13. Hairuhusiwi kubeba mfuko wa rambo

  14. Hairuhusiwi soli ya viatu kwenda upande

  15. Hairuhusiwi kuvaa kaptura (pensi)

  16. Hairuhusiwi kutochomekea shati

  17. Hairuhusiwi kuomba kalamu
Nawatakia uvaaji mwema wa tai.

==============================
Mkuu Bitoz ameongezea hizi pia:
18/ Hairuhusiwi kunuka mdomo + kwapa
19/ Ni marufuku kuvaa tai na mavazi oversize
20/Hairuhusiwi kuvalia makubanzi
21/Hairuhusiwi kutafuna mahindi km ng'ombe barabarani
 
18/ Hairuhusiwi kunuka mdomo + kwapa
19/ Ni marufuku kuvaa tai na mavazi oversize
20/Hairuhusiwi kuvalia makubanzi
21/Hairuhusiwi kutafuna mahindi km ng'ombe barabarani
 
kama hizo ndio sheria basi haturuhusiwi kuvaa tai
 
Naona sheria 17 kaka soccer duh bas sawa ila u mesahau moja hutakiwi kujamba
 
18/ Hairuhusiwi kunuka mdomo + kwapa
19/ Ni marufuku kuvaa tai na mavazi oversize
20/Hairuhusiwi kuvalia makubanzi
21/Hairuhusiwi kutafuna mahindi km ng'ombe barabarani
Hapo kwenye kutafuna mahindi utawekwa ndani na DC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom