Jicho la tatu; Utekwaji nyara Dr Ulimboka, hata makampuni binafsi ya ulinzi yanaweza tumiwa.

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Wakati tunaendelea kutanua tafakari zetu kwa ukatili aliofanyiwa ndugu yetu. Macho yetu mawili tuyaelekeze kwa serikali huku tukiangalia mbele lakini kuna haja ya kuweka jicho la ziada kisogoni mwetu hata kama la bandia kwa ajili ya kutizama pande nyingine ambazo tunazisahau sana. Kwa mfano, siku hizi kuna makampuni ya ulinzi binafsi ambayo nayo hutumia silaha kama watumiavyo polisi. Tena huzibeba bila ya uficho, hawa nao wanaweza kukodiwa na kutumiwa kufanya tukio kama lililotokea. Ni vyema kwa nia njema ikiwa kweli tunamsaka adui huyu, ni budi tuweke eneo pana katika kutafuta njia ya kutufikisha walipo wauaji pasi na shaka.
 
Kinyaaaa!!!!!!!!!!!

Naona CCM mko bize kufanya Shopping for a POSSIBLE CRIMINAL ON-SALE to come and stand in for you guys presumably at a pay lakini katika hili la Dr Ulimboka ...!!!!
 
Wakati tunaendelea kutanua tafakari zetu kwa ukatili aliofanyiwa ndugu yetu. Macho yetu mawili tuyaelekeze kwa serikali huku tukiangalia mbele lakini kuna haja ya kuweka jicho la ziada kisogoni mwetu hata kama la bandia kwa ajili ya kutizama pande nyingine ambazo tunazisahau sana. Kwa mfano, siku hizi kuna makampuni ya ulinzi binafsi ambayo nayo hutumia silaha kama watumiavyo polisi. Tena huzibeba bila ya uficho, hawa nao wanaweza kukodiwa na kutumiwa kufanya tukio kama lililotokea. Ni vyema kwa nia njema ikiwa kweli tunamsaka adui huyu, ni budi tuweke eneo pana katika kutafuta njia ya kutufikisha walipo wauaji pasi na shaka.
Mbona mnatumia nguvu kubwa sana kuondoa dhana ya kwamba serikali imehusika?..Jamani sisi wote hapa sio wageni wa System inavyofanya kazi hata kesho wakitaka kumwondoa JK wanaweza na asiwe na habari yeye. Wameondoka wangapi ndani ya chama, serikali na nje wamekolumbiwa..Tena inasemekana hadi Mwalimu aliondolewa hatuma tu ushahidi..

Sii rahisi mtu wa kampuni za Ulinzi ajitutumue kumwita mtu ktk mahojiano akijitambulisha yeye ni usalama wa Taifa. Dr.Ulimboka leo mgonjwa lakini hata yale machache alotueleza yanatosha kabisa kuiweka serikali hatiani maana sii rahisi kabisa kwa mtu wa kawaida kupanga mazungumzo na Dr. Ulimboka nakama nakumbuka vizuri kuna habari niilisoma hapa alitakiwa kwanza kwenda Ikulu hakwenda, yakafanyika maandalizi mengine ya kukutana wala sii mara moja.

Watu wanaomtafuta Dr. Ulimboka nje ya systema wangetafuta anaishi wapi wakamwingilia nyumbani kwake au hata kazini lakini haya ya kuzungumza naye kwa muda halafu kikubwa zaidi kinachomaliza yote ni pale aliposema alikuwa akiulizwa "Ni nani anahusika na maandalizi ya Mgomo huu.." Hapakuwepo na swali jingine lolote zaidi ya kuhusiana naMgomo sasa wewe nambie nani kati wa vyombo vyote nvchini wangekuwa na haja ya kujua hilo..

Wanasema Chadema kama ni Chadema na wao ndio wanasemekana wamepanga mgomo huu basi lazima wanamfahamu aliyendaa mgomo wasingeuliza swali hilo. Kama ni walinzi wa makampuni ambao wanafundishwa kwata geuka kushoto kulia na marktime sidhani kama wana ujuzi wa interrofation maana mchanganuo ule unaonyesha wazi ni mtu anayeijua kazi yake.. Acheni kuficha madhambi wametutoka wengi tu wala huyu sii huyu wa kwanza..
 
Kinara wa unyama huo ni Rais Kikwete!!! Uzuri Dr. Ulimboka hajafa!! Siri zote ziko wazi!!
 
Walinzi wa makampuni binafsi wanatembea na kolea kung'olea watu meno na kucha? Na yule kachero aliyekuwa anaongelea chooni kuhusu hali ya Dr Ulimboka naye anafanya kazi kwenye kampuni binafsi ya ulinzi? Vipi kuhusu mzee wa wallet na simu, anafanya wapi kazi?
 
huu muda mnaotumia humu mgetumia kupatia majawabu hoja za madaktari,acheni tabia ya liwalo na liwe
 
Ulimboka hajafa habari zote anazo akipona ataanika kila kitu tutajua,ila wasiwasi wangu ni hatari ya maisha yake kwani wabaya wake bado wanamuwinda kweli,mara hii usishangae ikawa ni ajali.
 
Kinara wa unyama huo ni Rais Kikwete!!! Uzuri Dr. Ulimboka hajafa!! Siri zote ziko wazi!!

Na ukweli ukijulikana na hizi tuhuma unazotoa utajificha wapi? Acha kukurupuka. Kikwete ni Dhaifu, ndiyo, lakini acha tuhuma usizokuwa na ushahidi, hizi zinaitwa chuki na udaku!
 
Wakati tunaendelea kutanua tafakari zetu kwa ukatili aliofanyiwa ndugu yetu. Macho yetu mawili tuyaelekeze kwa serikali huku tukiangalia mbele lakini kuna haja ya kuweka jicho la ziada kisogoni mwetu hata kama la bandia kwa ajili ya kutizama pande nyingine ambazo tunazisahau sana. Kwa mfano, siku hizi kuna makampuni ya ulinzi binafsi ambayo nayo hutumia silaha kama watumiavyo polisi. Tena huzibeba bila ya uficho, hawa nao wanaweza kukodiwa na kutumiwa kufanya tukio kama lililotokea. Ni vyema kwa nia njema ikiwa kweli tunamsaka adui huyu, ni budi tuweke eneo pana katika kutafuta njia ya kutufikisha walipo wauaji pasi na shaka.

Mnahangaika sana, yaani kwa akili yenu mnafikiri watanzania ni wale wa "ndiyo mzee"pole sana
 
huu muda mnaotumia humu mgetumia kupatia majawabu hoja za madaktari,acheni tabia ya liwalo na liwe

Ha haaa, hata mm nawashangaa. Mtu kakaaa, katunga ka sread kake anakaleta eti aonekane great thinker au kuwahadaisha watu na mambo yatakavyokuwa. Wanatakiwa walete hoja za maana. Kama tu hana hoja bora akae kimya.
 
Hata kama ni jicho la sita,serikali ndo iliyohusika na huu unyama,ila Mungu amewaumbua!
 
Moja ya udhaifu mkubwa wa serikali hii mpaka sasa wanahangaika kuficha ukweli wa wazi. Sielewi kwanini hawajawatoa muhanga wahusika ili kulinda heshima ya vyombo vyetu vya usalama,serikali na nchi.
 
Mnahangaika sana, yaani kwa akili yenu mnafikiri watanzania ni wale wa "ndiyo mzee"pole sana

Huu ushabiki wa siasa unatepeleka pabaya kiasi cha kupooza akili zetu. Mjinga yeyote lazima afikirishe akili yake kwa upeo mfupi kama wewe. Bando hakuna mantiki na msingi wa serikali kuhusika moja kwa moja, wengi mnatawaliwa na hisia za kisiasa zaidi kuliko kutafuta ukweli.
 
Moja ya udhaifu mkubwa wa serikali hii mpaka sasa wanahangaika kuficha ukweli wa wazi. Sielewi kwanini hawajawatoa muhanga wahusika ili kulinda heshima ya vyombo vyetu vya usalama,serikali na nchi.

Wahusika unaowajua wewe ni kina nani? Mbona mnapiga kelele tu lakini hamsemi wala hamuwataji hao mnaowajua?
 
Hata kama ni jicho la sita,serikali ndo iliyohusika na huu unyama,ila Mungu amewaumbua!

Hisia za kisiasa ushabiki wa kivyama, na chuki dhidi ya serikali ikizidi namna hii ni udhaifu mkubwa, pengine maadui wa Dr Ulimboka waliofanya tendo hilo wakisikia kauli zenu za kuangalia upande mmoja wanafurahi na kujiona washindi.
 
huu muda mnaotumia humu mgetumia kupatia majawabu hoja za madaktari,acheni tabia ya liwalo na liwe

Amakweli mtesaji wa Dr Ulimboka amefanikiwa kuwachonganisha pro CDM na serikali. Kiasi akili zenu zimedumaa na kutulia.
 
Walinzi wa makampuni binafsi wanatembea na kolea kung'olea watu meno na kucha? Na yule kachero aliyekuwa anaongelea chooni kuhusu hali ya Dr Ulimboka naye anafanya kazi kwenye kampuni binafsi ya ulinzi? Vipi kuhusu mzee wa wallet na simu, anafanya wapi kazi?

Mzee weka Uchadema pembeni katika nafsi yako na ufikirishe akili yako kwa undani. Koleo la kutolea meno hata mtoto wa chekechea anaweza kuwa nalo, hoja ya pochi na simu nadhani ulisoma maneno ya profesa Mseru aliyekuwepo wakati Msangi anamuhoji Dr Ulimboka. Kasema wazi kuwa huo ni uzushi wenu tu, kwani yeye alikuwepo mwanzo mpaka mwisho. Kulazimisha kwenu upuuzi badala ya kutafuta ukweli hatuwezi kufika popote. Tutaishia kwenye siasa za ushabiki wa chama tu.
 
Back
Top Bottom