Jibu maswali haya kabla hamjamhukumu Maige kwa twiga

Tena mabaya zaidi walichukuliwa kwa ndege ya jeshi je watu wakitengo cha anga walikuwa wapi ndege ya jeshi inaingia kwenye anga letu inashuka na inachukua twiga wao bila kuhoji??Hapa nikuwa kila kitu kilikuwa kimekuwa organized na document zote zilionyesha uhalali wakuchukua twiga!!Maige kaangukiwa na jumba bovu!
 
uhamiaji, usalama wa taifa, polisi na wengine wowote unsowafahamu wanatekeleza maagizo ya ikulu, fikiria sisi wahamiaji haramu tulivyoishika idara ya uhamiaji ndo utajua nini namaanisha.

salute wote
 
Naona wengi wenu mnakurupuka bila kusoma hii kesi inaendaje na pia hamkupitia ripoti ya CAG.

Kusafirisha Twiga sio kosa, kusafirisha Twiga bila kuwa na vibali maalum ndio kosa. Sasa walioruhusu Twiga kukamatwa, kusafirishwa nchi kavu, wapakiwe kwenye ndege na kusafirishwa bila vibali ndio wa kuchukuliwa hatua. Ni mlolongo wa kuanzia walipotegwa hawa Twiga waliowapakia kwenye malori bila vibali, waliowachoma Sindano zinazotakiwa kiafya, waliowaweka karantini, waliowasafirisha. ujinga huu umefanywa na watendaji wa kila kada, kuanzia mbugani, kijijini, barabarani, uwanja wa ndege.

Tuwe wakweli.
 
Siamini kama twiga wametoroshwa na kusafirishwa kwenda nje ya nchi bila serikali kujua.
Kinachonifanya nisiamini ni maswali haya:

1. Ni dhahiri kuwa maeneo ambako twiga wanaishi (mbugani) serikali imeweka watumishi mbalimbali wanaohusika na ulinzi na usalama.
2.ni dhahiri pia kuwa viwanja vya ndege vyote vinalindwa na maofisa na maafisa wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama yaani polisi, usalama wa taifa, takukuru, uhamiaji nk.
3. Ni dhahiri pia kabla ya mgeni yeyote kutoka nje kuingia nchini pasi yake ya kusafiria inakaguliwa na wenzetu wa uhamiaji.
4. Ni dhahiri kuwa mgeni husika lazima atakuwa ameeleza nini amekuja kufanya hapa nchini.

Sasa mimi sijui kutokana na maswali hayo hapo juu kwanini suala la kutoroshwa twiga wetu anahukumiwa maige peke yake.

Sijui pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi hadi wanyama warefu kuliko wote wanakimbizwa uarabuni bila mkuu wa nchi kupata taarifa na hata mzee nahodha, hussein mwinyi nao hawakumweleza mkuu wa kaya juu ya hilo?

Haya hao mbali, mkuu wa usalama wa taifa, igp, na mkurugenzi mkuu wa uhamiaji nao walikuwa wapi?

Mimi nahisi hao twiga walitoroshwa kwa maelekezo ya mkuu zaidi ya hao mawaziri na wakuu wa taasisi za ulinzi na usalama. Maana bado tunakumbuka wale mbuni walivyoisha pale mjengoni ikulu wakati fulani. Walipungua taratibu hadi kuisha. Au twiga wameondoka kwa mtindo huo huo lakini lawama zote kwa maige? Kidumu chama cha mapinduziiiiiiiiiiiiii.

sasa kamwambie basi awataje watu mbao wewe na yeye mnahisi walihusika kusudi tumsaidie. Kwa nini akae kimya!!!! alete hoja na sio kulialia tu
 
Jamani kwa hili mnamwonea maige, labda hamna kumbux2, alilikuta sheshe hilo wakati anaingia wizarani! Alipoingia tuu
 
Tena mabaya zaidi walichukuliwa kwa ndege ya jeshi je watu wakitengo cha anga walikuwa wapi ndege ya jeshi inaingia kwenye anga letu inashuka na inachukua twiga wao bila kuhoji??Hapa nikuwa kila kitu kilikuwa kimekuwa organized na document zote zilionyesha uhalali wakuchukua twiga!!Maige kaangukiwa na jumba bovu!

Kama ni hivyo, waziri wa ulinzi na Mkuu wa majeshi inabidi nao wajiuzuru au wawajibishwe kisheria
 
Yaani sheshe lilikuwa si lake, wakamsimamisha mkrugnzi mpya wa wanyamapori Mbangwa!Maige, mbangwa walikuwa wageni wzrn
 
Hapa hakuna jinsi ya kumtetea Maige badala yake naona mnazidi kumkaanga.
Kwa wanaoelewa mambo ya adminstration hata management kuna kitu kinaitwa "collective accountability"....yaani unawajibika kwa kushindwa kushughulikia matatizo ambayo yamefanywa na watendaji wako au wenzako!
Kama aliambiwa na mkuu angesema mie siwezi najiuzulu...hii ndio political accountability.....kama Maige akipelekwa mahakamani hapo ndio utaona mlolongo wa watuhumiwa....this is how accountability is at the law,lakini anawajibishwa kwanza yeye kwa kushindwa kuwawajibisha awali au kuwajibika mwenyewe.
Cha kupigia kelele hapa ni mtuhumiwa kupelekwa mahakamani katika uchunguzi wa kesi ukweli utadhihirika!
But he is responsible and answerable for actions and inactions....hii ndio collective accountability!
 
Maige alifanya nini baada ya kujua twiga na wanyama wengine wameporwa? alitakiwa kujiuzulu siku ya kwanza alipogundua kuwa wenzake wamemzunguka; angekuwa shujaa!

Mzee Mwanakijiji, Kwani Maige kaondolewa kwa sababu ya wanyama kutoroshwa au ni kwa sababu alishindwa kufunika dill lisijulikane? Kama ingekuwa ni kwa sababu ni wanyama kutoroshwa naamini waziri wa mambo ya ndani (anashughulikia uhamiaji na usalama wa raia), IGP na wakurugenzi wa uhamiaji na TISS nao wangeondolewa. Maige kawa victim kwa sababu hii habari hii ilivujia upande wake. Hawa wengine ni wasafi maana kwao hakujavuja.
 
Siamini kama twiga wametoroshwa na kusafirishwa kwenda nje ya nchi bila serikali kujua.
Kinachonifanya nisiamini ni maswali haya:

1. Ni dhahiri kuwa maeneo ambako twiga wanaishi (mbugani) serikali imeweka watumishi mbalimbali wanaohusika na ulinzi na usalama.
2.ni dhahiri pia kuwa viwanja vya ndege vyote vinalindwa na maofisa na maafisa wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama yaani polisi, usalama wa taifa, takukuru, uhamiaji nk.
3. Ni dhahiri pia kabla ya mgeni yeyote kutoka nje kuingia nchini pasi yake ya kusafiria inakaguliwa na wenzetu wa uhamiaji.
4. Ni dhahiri kuwa mgeni husika lazima atakuwa ameeleza nini amekuja kufanya hapa nchini.

Sasa mimi sijui kutokana na maswali hayo hapo juu kwanini suala la kutoroshwa twiga wetu anahukumiwa maige peke yake.

Sijui pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilikuwa wapi hadi wanyama warefu kuliko wote wanakimbizwa uarabuni bila mkuu wa nchi kupata taarifa na hata mzee nahodha, hussein mwinyi nao hawakumweleza mkuu wa kaya juu ya hilo?

Haya hao mbali, mkuu wa usalama wa taifa, igp, na mkurugenzi mkuu wa uhamiaji nao walikuwa wapi?

Mimi nahisi hao twiga walitoroshwa kwa maelekezo ya mkuu zaidi ya hao mawaziri na wakuu wa taasisi za ulinzi na usalama. Maana bado tunakumbuka wale mbuni walivyoisha pale mjengoni ikulu wakati fulani. Walipungua taratibu hadi kuisha. Au twiga wameondoka kwa mtindo huo huo lakini lawama zote kwa maige? Kidumu chama cha mapinduziiiiiiiiiiiiii.

Yule bwana komba alishateuliwa ni balozi wetu nchi fulani hivi wakati maige akiumizwa huku yeyew mhusika ameula
 
mi sion tatizo la watu wa chin waliopewa maagizo tu. mfan familia ina tv mbovu na baba akamtafuta fundi na kumuelekeza aifuate nyumban akiwa amekwisha wapigia housegal\boy watoe tv kwa fund na fundi akaishia kuiiba na kutokomea nayo.uje uwalaumu wao kwa kuitoa ndani,kufungua geti na kuitoa wakat wana maagizo kamil ni kuwaonea sawa na kuwaonea watumishi wa mbugan waliochoma sindano,watumishi wa ndege na nk
 
Unachosema kimesemwa na watu wengi sana hapa JF. Hakuna waziri mwenye nguvu ya kutorosha wanyama hai bila kupata go-ahead ya Ikulu. It's a known fact. Kitu watu wengi walichokuwa wanataka ni kumwona waziri mhusika anachukua responsibility hiyo ya kutoroshwa hao wanyama kwa sababu wamechukuliwa kwenye "watch" yake. Most people know who the main player is and now that the minister has been tossed, we hope he will become bitter enough to name the culprit(s). Actually kama wabunge wataendelea kupress kuwajibishwa kwa hawa wezi kisheria, nahisi hii serikali haitafika 2015. Naona hii soap opera yetu imeanza rasmi. Sit back, grab a drink and keep your eyes peeled!

Usiihusishe Ikulu na huu ujinga.

Humjui Kikwete, kaa kimya. Ikulu ya Kikwete si Ikulu ya Mkapa wala Mwinyi wala Nyerere. Huko kwa Kikwete, ukienda na huu ujinga wa vibali unaambiwa kuna sheria na kanuni fateni hizo. Nnakuhakikishia humjui Kikwete, unamsikia tu.
 
Maige hawezi kukwepa lawama kwa sababu alikuwa ni sehemu ya serikali kwa maana hiyo alikuwa anajua kinachoendelea kwenye suala hili na yeye alikuwa na masilahi nalo vinginevyo angejiuzuru mapema baada ya suala hili kuibuka ili kuonesha kuwa yeye hahusiki
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom