Jiadjustishe

Mtanzanika

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
2,389
1,131
Last weekend nilijiAdjust mitaa
Fulani na washkaji, tukajiAdjust
sehemu tukaAdjust na misosi na
drinks.
Kila mtu akawa busy anaAdjust
plate yake huku mdogomdogo
tunaAdjust story mbili tatu.
TukaAdust tukaAdjust….mara
simu yangu ikawa inaAdjust,
nikapokea. Sasa wakati naAdjust
na mtu aliyenipigia kuna dada
akawa amejiaAdjust kwenye meza
yetu, akaomba kujiaAdjust na sisi.
Washkaji wakamuaAdjust akawa
ameAdjust nayeye kinywaji chake.
Nilipomaliza kuAdjust na simu
yangu, nikamuAdjust vizuri Yule
dada lakini sura ilikua ngeni, me
nikaAdjust kwamba labda
washkaji wanamuAdjust ndo
mana amejiAdjust na sisi. Yule
dada AkaniaAdjust me nikaitikia
vizuri tu,si akaniAdjust simu yangu
“we kaka simu yako nzuri hebu
niAdjust kidogo”.
Me nikampa akawa anaiAdjust,
wakati me naendelea kuAdjust
Chips zangu Yule dada akawa
bado tu anaiAdjust simu yangu.
Mara akanirudishia simu yangu
me nikaiAdjust mfukoni. Ghafla
Yule dada akainuka baada ya
kuwa amemaliza kuAdjust kinywaji
chake akatuAdjust kwaherini.
Washkaji wakamuAdjust vipi
mbona ghafla! AkatuAdjust kuwa
kuna kitu amekiAdjust home
kwao kwahiyo anakiwahi haraka.
Me nikawaAdjust washkaji kwani
vipi nyi hamumuAdjust Yule dada!
Wakasema wao hawamuAjust
wameshangaa tu kajiAdjust kwa
meza yetu…
Sasa baadae katika matumizi ya
hapa na pale ya simu yangu si
nikawa na Adjust salio! Loh
nikagundua kama 4000/= zilikua
zimeAdjustiwa….ndo nilipogundua
kumbe Yule dada alipoAdjust
simu yangu aliAdjust na salio
langu pia…halafu mbaya zaidi
hata ile Sms ya kuAdjust salio
aliiAdjust….so ndo nikawa
nimeAdjustiwa kiivo yaani!!!!!
 
Back
Top Bottom