Elections 2010 JF's Maxence LIVE on EATV "Uchaguzi Express Live"

Maxence umefanya jambo jema kuipeleka JF kwenye mijadala ya wazi. Sasa wasubiri watakapoifahamu vyema JF na what is inside watajuta kwa nini hawakuifahamu mapema.

Tuendelee kuelimisha umma wa watanzania waipende na kuipa nafasi ya kwanza nchi yao.

Pamoja tunapanda
Shukrani mkuu, tutaongea kupitia Radio, tulianza na Morning Star radio na leo itakuwa ni kupitia East Africa Radio.

Aidha, tutahitaji members kadhaa walio tayari kushiriki mijadala kwenye television na radio tuwasiliane nao ili tushiriki vipindi ambavyo wametuomba baadhi ya vyombo vya habari. Watakaokuwa tayari tuwasiliane ili tuweze kufahamishana ajenda kuu ni nini.
 
Sasa kutuweka sote ktk kapu la CHADEMA ni kuonesha huna upeo kuhusu JF na unayo tabia ya kutoa majumuisho marahisi bila ya kuwa na facts.
Hili itabidi niligusie kwenye radio, najua wataruhusu maswali; kuna uwezekano mkubwa likaulizwa. Shukrani kwa kutoa ufafanuzi mkuu
 
kwa umbumbumbu wake maxence ameshindwa kuwaambia watanzania kuwa hii jamii ni ya wachadema....! na kipindi kimeshaisha...!

Mimi sio Chadema ila nataka mabadiliko - Rais mpya. Chama kingine kuunda serikali!
 
Wakuu kumradhi, ilikuwa kipindi hicho wawepo Synovate, nilichotarajia tujadili sicho kilichojadilika hivyo ikabidi twende kadiri inavyowezekana na kuongea na vijana kupitia TV ya vijana EATV.

Hii leo saa 4 asubuhi nitakuwa East Africa Radio; hapa natambua naongea na watu wazima wengi na si wa Tanzania pekee bali na wale wa Kenya na Uganda wamo.

Kuna vitu nimeona kuwa itabidi tuvifanyie ufafanuzi:

  1. JF inatembelewa na watu si pungufu ya 12,000 kwa siku; watu hawa wanaoitembelea si watu wa kupenda siasa tu, si watanzania tu n.k. Aidha kila mmoja anakaa ndani ya JF kwa wastani wa dakika 15 akiiperuzi (huu si muda mdogo). Kwa mwezi (August stats) JF inapata hits milioni 60+
  2. Asilimia 67.2 ya watembeleaji wa JF ni kutoka Tanzania
  3. Watumiaji wa JF mpaka sasa walio wengi ni umri wa miaka 25 na kuendelea mpaka miaka 44, wengi ni wahitimu wa vyuo walau.
  4. JF ipo ranked kuwa ndani ya tovuti 35,000 (nafasi ya 34,544 hadi naandika) kutembelewa sana ulimwenguni (tembelea Alexa - Jamiiforums.com Site Info ) na ni ya kwanza Tanzania kuwa na wasomaji wengi (japo Alexa huwa hawaandiki hilo, unaweza kujaribu mwenyewe kulinganisha na tovuti nyingine)
  5. JF ni user generated content website. Kila anayejisajili anaweza kuanzisha hoja na ikajadiliwa (kama inajadilika) na registration ipo huru kwa kila mmoja
  6. JF si mali ya CHAMA wala MTU flani, hoja zilizoandikwa na watu zinamilikiwa na watu hao zikisimamiwa na waendeshaji wa JF. Kila mwana JF ni mmiliki wa alichokiandika, anapata uwezo wa kuki-edit au kukiondosha anapoamua. Ukiwa mwanachama na ukashiriki mjadala wowote unakuwa umejiweka katika familia ya wana JF.

Sidhani kama nilikosea kuwataja baadhi ya wanachama wenye kutumia majina yao halisi bila kujali wapo chama gani; nakumbuka nilimtaja Nape, nadhani nilimsahau Bashe pia, hawa tunao ni jambo la heri kuwa wapo tayari kwa debate.

Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake, kila mmoja anavyoona inastahili, tunayazingatia. Tunachofanya ni kuiangalia mijadala isiharibiwe kwa kuzingatia sheria tulizojiwekea.

Kwa wale wanaoi-access JF via mobiles endapo kutakuwa na matatizo (test period) tunaomba tufahamishwe ili turekebishe kabla hatujaja na kitu kipya Oktoba hii.

Shukrani wakuu
kiongozi ukitoka tu hapo east-africa nitakuwa nakusubiri maryland nikupe kesto laiti zako tano tu
 
kiongozi ukitoka tu hapo east-africa nitakuwa nakusubiri maryland nikupe kesto laiti zako tano tu

Hahahahaaaaaa.......Then akishazimaliza akaitwa Clouds ataongea nini??? au Jamaa sio kichwa maji kama sie wengine Castle Mbili tu HOI?????
 
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya members wa JF hawapo Tanzania,wako nje ya nchi na mengi yanayozungumzwa na kujadiliwa ndani ya JF huishia humu humu JF....JF ni darasa tosha sana kwa wa Tanzania,tatizo ni kwamba haijulikani....Nikiwa Tanzania nilijaribu kuwauliza baadhi ya watu tu kuhusu JF wengi wanasema hawaijui,sana sana wanachojua ni facebook,Michuzi,yahoo n.k................JF ijitangaze sasa............Inaweza kuwa na mchango mkubwa sana kwa Taifa letu mbeleni

Sio Zaidi ya watanzania 500,000 ndio wana access ya internet. Na wengi wao wanatumia internet za maofisini hivyo hawako huru kwenye suala la Muda.

Wale wenye nazo majumbani au kwenye simu gharama yake ni Kubwa sana hivyo wanatumia kwa vitu vya ulazima.

Pia watanzania wengi hawajui internet ni burudani, na wanapenda muda wao free kuutumia kwenye Mabaa.

Ila JF ni makini kama waandishi wa habari watajiunga, na viongozi mbalimbali, kwani watapata nafasi ya kujua masuala mengi na kero nyingi.
 
Wale wenye nazo majumbani au kwenye simu gharama yake ni Kubwa sana hivyo wanatumia kwa vitu vya ulazima.
Mkuu, huo utafiti wako umeufanyia wapi? Sasa hivi Bongo kupata Access ya Internet ni pesa yako tu, Kwa mtu wa kipato cha kati hatashindwa kulipia Tsh 40,000/= kwa mwezi? na anapata unlimited up/dwn.... mimi nina net home/office na kwenye simu niko JF kwa masaa 5/8 kwa siku kutegemeana na muda nitakaoupata.

Mtaani kwangu 30% wana huduma ya mtandao.
 
Wakuu kumradhi, ilikuwa kipindi hicho wawepo Synovate, nilichotarajia tujadili sicho kilichojadilika hivyo ikabidi twende kadiri inavyowezekana na kuongea na vijana kupitia TV ya vijana EATV.

Hii leo saa 4 asubuhi nitakuwa East Africa Radio; hapa natambua naongea na watu wazima wengi na si wa Tanzania pekee bali na wale wa Kenya na Uganda wamo.

Kuna vitu nimeona kuwa itabidi tuvifanyie ufafanuzi:

  1. JF inatembelewa na watu si pungufu ya 12,000 kwa siku; watu hawa wanaoitembelea si watu wa kupenda siasa tu, si watanzania tu n.k. Aidha kila mmoja anakaa ndani ya JF kwa wastani wa dakika 15 akiiperuzi (huu si muda mdogo). Kwa mwezi (August stats) JF inapata hits milioni 60+
  2. Asilimia 67.2 ya watembeleaji wa JF ni kutoka Tanzania
  3. Watumiaji wa JF mpaka sasa walio wengi ni umri wa miaka 25 na kuendelea mpaka miaka 44, wengi ni wahitimu wa vyuo walau.
  4. JF ipo ranked kuwa ndani ya tovuti 35,000 (nafasi ya 34,544 hadi naandika) kutembelewa sana ulimwenguni (tembelea Alexa - Jamiiforums.com Site Info ) na ni ya kwanza Tanzania kuwa na wasomaji wengi (japo Alexa huwa hawaandiki hilo, unaweza kujaribu mwenyewe kulinganisha na tovuti nyingine)
  5. JF ni user generated content website. Kila anayejisajili anaweza kuanzisha hoja na ikajadiliwa (kama inajadilika) na registration ipo huru kwa kila mmoja
  6. JF si mali ya CHAMA wala MTU flani, hoja zilizoandikwa na watu zinamilikiwa na watu hao zikisimamiwa na waendeshaji wa JF. Kila mwana JF ni mmiliki wa alichokiandika, anapata uwezo wa kuki-edit au kukiondosha anapoamua. Ukiwa mwanachama na ukashiriki mjadala wowote unakuwa umejiweka katika familia ya wana JF.
Sidhani kama nilikosea kuwataja baadhi ya wanachama wenye kutumia majina yao halisi bila kujali wapo chama gani; nakumbuka nilimtaja Nape, nadhani nilimsahau Bashe pia, hawa tunao ni jambo la heri kuwa wapo tayari kwa debate.

Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake, kila mmoja anavyoona inastahili, tunayazingatia. Tunachofanya ni kuiangalia mijadala isiharibiwe kwa kuzingatia sheria tulizojiwekea.

Kwa wale wanaoi-access JF via mobiles endapo kutakuwa na matatizo (test period) tunaomba tufahamishwe ili turekebishe kabla hatujaja na kitu kipya Oktoba hii.

Shukrani wakuu

Hongera sana Mkuu. NImeona clip ya mjadala mliokuwa nao EATV (shukran Mwanakijiji). Ni mwanzo mzuri.

Kutokana na mialiko kama hii, ni dhahiri kuwa JF inajulikana kwa walio wengi, hasa vijana. Nina ombi moja kuu. Nalo ni kutumia vizuri nafasi hizi vizuri kwa kuitangaza zaidi JF. Kwa mfano, katika kila usemacho, zungumzia JF (Kule JF tuna...., Kuna maoni yaliwahi kutolewa JF kuhusu ... n.k).

JF inatakiwa ikue kiasi ambacho itaweza kuwafikia watu wengi zaidi. Habari nyingi za nchi yetu zinapatikana mara moja JF. I call it a Web University.

Pamoja na kila kinachosemwa, JF ina bahati ya kutovumilia unafiki wa kisiasa au kimaadili. Kuna wengi hapa wa vyama mbalimbali ambao wanatoa maoni yao kwa heshima, bila kuvunja kanuni za JF na pia kwa kuheshimu maoni ya wengine.

Mkuu, nakutakia kila la kheri katika mijadala unaofuata katika media mbalimbali.
 
Max, ndio anajitambulisha kwenye radio, anasema anatoka JF.Mussa anasema kwa wale wanaopenda kuperuzi FB,TwT lazima watakuwa wanaujua huu mtandao wa JF. wamekwenda mapumziko kabla ya kuanza mjadala. Mjomba yuko hewani na kibao chake cha Adella
 
Ameanza kuhojiwa James, Niko Nairobi nawapata vizuri sana EA Radio!
 
Guys kwa wale ambao mna access na radio hivi sasa u may tune to East Africa Radio, JamiiForums ikiwakilishwa na Maxence Melo wapo live.

Ni review ya yale ambayo waliongelea jana kuhusiana na suala zima la uchaguzi, so kwa wale ambao hamkupata nafasi ya kuona live jana basi mna nafasi ya kusikia leo.

-wamegusia suala la usawa katika vyombo vya habari kuwahabarisha wananchi.
 
ni jamaa wa JF aliyeongea mwishoni ndo katoa point za ukweli wengine hasa huyo dada wa YTVA ni longo longo za face book., bravoo max.
 
Kwa Max anavishukuru vyombo vya habari na mitandao mingine. Anaviponda vyombo vya habari vinavyopendelea vyama fulani!
 
Back
Top Bottom