JF's impact on Tanzanian Politicts

Ukitaka kujua utamu wa jf utaona members wanatishia kujitoa na wengine wanalalamika lakini hawajitoi uanachama! JF inapendwa si mchezo, wanaodai imekosa mwelekeo hawaachi kila siku kuchungulia humu! Hongereni sana waanzilishi wa JF!

kuna swali la msingi halijajibiwa hapa. Ni nani mwanzilishi na mwenye copyright ya JF?
 
Kweleakwelea, tafadhali nifahamishe 'proportion' ya wadini Tanzania, kwa kutumia vielelezo hapa JF au mitaani. Majimbo mangapi yalikuwa yanajadiliwa JF kwenye kipindi cha uchaguzi? Yanazidi 80? Ilikupa picha halisi ya mambo Tanzania kwa ujumla?

SWALI ZURI. UDINI UMEONEKANA NI SILAHA YA WAPUMBAVU WANAPOTAKA KUPATA CHEAP POPULARITY. NI DHANA AMBAYO NI TOP DOWN, IKIPANDIKIZWA KWA NGUVU NA VIONGOZI WALIOPOTEZA UMAARUFU. HATA WALE WANAOAMINI KATIKA DHANA HIYO MFANO JK NA ZITO PIA WAMEISHIWA HOJA! NASHUKURU WATU WAMEKATAA KUBURUZWA NA WATU WA DISAINI HIYO. - katika jf pia watu wanaoargue kiudini are few and very weak in arguments! - wale wanaoacha akili zao getini.
 
Kwamba ziandikwe makala nyingi zaida kupitia magazeti. Shaka yangu ni wasomi wangapi watz wanaosoma makala. Hapa JF tu ukiandika nusu ukurasa watu wanalalama na wengine wanadiriki hata kuagiza wenzao wawasomee!

Sasa, binafsi naamini redio zinafikia watu wengi, hapa tz, kuliko chombo kingine chochote. Shida kubwa ni maeneo ya vijijini, tena. Wakati wa kampeni kuna mikoa walilalamika hawafikiwi na radio, za tz. Pendekezo kwa JF, kama wanaweza kuanzisha community radio kakika maeneo ya namna hii ili kuwafikishia habari zinazopatikana kupitia JF na magazeti ikiwa ni pamoja na kundesha mijadala live.

Kuhusu redio, hapo kuna mtihani mwingine kama ulivyojadili hapo juu.

Mi' binafsi nina "bifu" na vituo vingi vya redio -- hasa vile maarufu. Haya mambo ya taarifa za habari za dakika mbili mpaka tano ni matusi! Hakuna la maana linalowafungua macho watu na kuwaelimisha.

Kuna watu hapa JF walishiriki vizuri sana kwenye mjadala mmoja wa Bongo Radio (ukipata muda uusikilize: Mjadala wa Bongoradio: Kuelekea Uchaguzi Mkuu Tanzania 2010).. Yaani, unapata elimu tosha; na mambo kama haya yanaweza yakaleta mabadiliko tunayopigia kelele.

Sasa, mi' ushauri wangu ni kutumia vyombo kama hivi, halafu ikisharekodiwa iwe inapelekwa kwenye redio ambazo zitakuwa tayari kuirusha hewani. Najua, zile redio maarufu zitagoma, lakini zipo ambazo zitakubali. Fanyeni bure tu. Halafu mtaona kitakachotokea... Redio nyingi hazijawahi kuwa na mjadala kama huo. Na isiwe kipindi cha uchaguzi tu.

Kuhusu makala (na hata vitabu), ndio Watanzania hatuna tabia ya kusoma makala na vitabu. Sababu tunazijua. Hata hapa, sijui wangapi waliipitia ilani ya Chadema na wakaona sera zao kuhusu vijana; au ile ya kurudisha mashindano ya kitaaluma mashuleni?? Ndio kuna ile sera 'maarufu' ya elimu bure, lakini nayo si watu walituchambulia, wakaijadili, sisi tukaja tukameza tu?

Lakini lazima kuwe na mwanzo. Nimeshasema mara nyingi sana -- Tanzania ni nchi pekee ambayo mwandishi (wa vitabu na makala) anakufa maskini. That says a lot about us! (Sizungumzii waandishi wa habari uchwara wa magazeti haya ya kishabiki na kipuuzi.)
 
Kwa kuongezea tu, naelewa lengo la huu mjadala...

Na kama viongozi au waasisi wa JF wanafuatilia, basi inabidi waamue:

1. Je, wanataka JF iwe jukwaa la mijadala tu? Halafu, watu wakirudi nyumbani waache kila kitu hapa?

AU:

2. Kuna malengo makubwa zaidi ya kujadili mambo tu? Wanataka wapige hatua kubwa na kusaidia jamii ya Tanzania kwa ujumla kuleta maendeleo? (Aisee, kuna wachambuaji wengi sana wenye upeo wa hali ya juu)...

(a) Wateue watu ambao wawe wanafuatilia mijadala muhimu, kisha waandike makala na kuzichapisha sehemu. Najua kuna visingizio vingi tu, lakini njia zipo. Kwa mfano, wanaweza wakawa na jarida lao la kila mwezi ambalo linasambazwa bure nchi nzima. Mkibaniwa na wachapishaji wa Dar, tumieni contacts za watu waliopo India! Nasikia huko kuchapisha vitabu ni chee tu, halafu hakuna kodi kuingiza vitabu Tanzania (nisahihishe kama nimekosea).

(2) Wale majamaa wa Bongo Radio inabidi waanze kutafuta contacts kwenye vituo vya redio. Sidhani kama ni ngumu kutengeneza vipindi vya redio. Wale wameshaonesha kuwa wanaweza kuandaa mijadala ya maana. Sidhani kama wanashindwa kuandaa kipindi kimoja kila wiki. Topics ziko nyingi sana, kuanzia elimu, katiba, mwelekeo wa siasa, na matukio mbalimbali nchini. Hata hivyo, wachangiaji ndio gurudumu la vipindi kama hivi...

Nawasilisha. Ijumaa njema!
 
kuna wanachadema humu! huwa wanakurupuka na sasa wanabagua watu kidini na kimaeneo! usipime kabisa, to aneno baya kuhusu chadema ndio utaona hiyo impact yake unayoisema,

JF ipo siku zote, impact yake imekuwa positive, ila kuna wachache wanaiharibu na kumwaga upupu humu ndani ambao ni aibu kabisa, though wanakuwa wamefikia maximum level ya kufikiri kwao,
Mimi mtu wa kijijini kanda ya ziwa huwa tuna usemi kuwa ukitaka kujua mchawi kwa hakika gombana naye. Yeye ndiye wa kwanza kukurushia dongo kuwa 'mchawi mkubwa wewe!' Hivyo mimi naamini kuwa ukiona mtu anazungumzia ubaguzi kwa kuuelekezea kwa wenzie huyo ndiye mbaguzi wa kwanza. Hii inathibitisha ya kuwa wasoipenda CHADEMA ni wabaguzi ndio maana wanakuwa wa kwanza kujihami kuwa CHADEMA ni wabaguzi wakati wao wakiwabagua watu kwa imani zao! Uteuzi wa rais wa wabunge watatu wote dini moja si ubaguzi kwa vile haukufanywa na rais wa CHADEMA! Uteuzi wa mawaziri katika wizara nyeti zote (Elimu, ulinzi, mambo ya ndani, fedha na Afya) si ubaguzi kwa vile aliyeteua hatoki CHADEMA. Ubaguzi wenu ndiyo laana itakayowamaliza huku mkipiga kelele CHADEMA ni wabaguziiiiiii!
 
SN,

Nakushukuru bwana, nacheka mwenyewe! Sijui kwa nini watu wengi wanachungulia tu kwenye hii thread lakini hawatoi mawazo yao. Kuna maswali mengi sana huko ukurasa wa kwanza na wa pili wa hii thread hayajajibiwa. Nashukuru GAGL kakumbusha mojawapo, labda hili lijibiwe na Mods.
 
Unaonekana hujazoea haya mambo, Gurudumu. Tunajua "kujadili" sana, lakini ni wachache ambao wanajua cha kufanya; na wachache mno, sana, ambao wanaweza kuamka na kufanya wanachopaswa kufanya (na hao ni wachache sana hapa.. wapo hapa lakini na ninawafahamu).

Anyways, naona watu wamegomea mjadala. Mi' siku ya leo nimeamua kuwapa heko wananchi waliojitokeza kulinda kura: Uchaguzi 2010: Wamelinda kura. Naamini hawa ndio waliotupa matumaini ya mabadiliko Tanzania.

Kwaherini.
 
Impact ipo ingawa si kubwa kwani wenyeaccess kwenye JF ni wachache wenye uwezo wa kulipia internet etcetc kila siku, lakini naweza kusema kwa kupitia JF (wanakubali mawazo ya kila mtu), maujumbe mbali mbali ya kisiasa yamekuwa yakiwafikia viongozi/wanasiasa wachache wasiowavivu kupata public opinions. Hawa wanaelewa kiasi gani katika kundi dogo tu la watanzania sasa wana mawazo gani na wanataka nini kwa maendeleo yao na vizazi vijavyo. Kwa mfano mdogo Zitto amejielewa kiasi gani siye wanamapinduzi hatumwamini tena huyo ni mfano tu lakini wako wengi tu. Kwa hiyo impact ipo kwa kiasi fulani na itazidi kuwepo kwani the youthful population of Tanzania is very keen to see changes in their country
 
NewVision,

Kama unakiri impact ni ndogo wakati JF imefanikiwa kuleta pamoja all these great minds, nini ushauri wako ili kuongeza impact kuelekea 2015? Na kama skendo nyingi zinawekwa wazi hapa lakini imebadili tabia za wanasiasa wachaChe, nini kifanyike ili skendo likitua Hapa JF na ikathibitishwa basi wanasiasa wawajibike. Umetoa mfano wa zitto kwamba amebadili tabia kutokana na kushambuliwa hapa JF, unaweza kutupatia mifano namna alivyobadili tabia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom