Je, waliosimamishwa wameweza kuwasiliana nani ili tuweze kuwasaidia, au kama mnanipa ruksa nifanye jitihada za binafsi kuwapata na kuwaleta hapa?
Mwenye mawazo tafadhali anitumie PM.
Haya mapambano ya kifikra yanazidi kupata majeruhi...hii inanikumbusha ule waraka wa mafisadi; mwanzoni walianza kutafuta umetoka wapi badala ya kuangalia kilichomo. Nadhani wakati umefika waandishi wapige kambi kule Posta na kuwabana kwa maswali wahusika wote..
Aprili mwaka jana kwa ushirikiano na wanachama watatu, uongozi wa JF uliiandikia Bodi barua ya kutaka waliokuwa wamesimamishwa kazi kurejeshwa haraka:Jamani;
JF ina wananchama ambao ni wengi na hawajuani. Sasa mnaanza vipi kuwaandikia barua?
Mtu yeyote anaweza kupost chochote humu bila ridhaa ya uongozi wa JF.
Kwahiyo HONGERA ZIENDE KWA WANACHAMA na si uongozi wa JF!
Mkurugenzi Mkuu
Benki ya Posta Tanzania
Dar es Salaam.
YAH: TUHUMA ZA UBADHIRIFU KATIKA BENKI YA POSTA
Katika gazeti la Tanzania Daima la Jumatano ya tarehe 16 Aprili 2008, pamoja na habari nyingine, kulikuwa na taarifa ya kupewa likizo ya lazima wafanyakazi watano wa benki yako kwa kile kilichodaiwa kupisha uchunguzi unaofanywa katika kuwatambua watu waliosambaza taarifa kuhusu ubadhirifu katika Benki ya Posta katika mtandao wa internet wa Jambo Forums. Tunapenda kuamini kwamba taarifa hizi ni za kweli kwa kuwa hazijakanushwa na ofisi yako hadi tunapoandika barua hii.
Sisi wanachama wa Jambo Forums na Menejimenti nzima tumesikitishwa sana na uamuzi wako wa kuwapa kile kinachodaiwa kuwa ni likizo ya lazima wafanyakazi watano wa Benki ya Posta. Tukiamini kwamba Benki ya Posta inaendeshwa kwa misingi ya uwazi na kwa kuheshimu haki za wafanyakazi na binadamu kwa ujumla, tulitarajia kwamba uongozi wa benki yetu hii baada ya kupata taarifa za ubadhirifu ungeanzisha mchakato wa kujua ukweli kuhusu taarifa hizi ili kuchukua hatua stahiki. Hatuoni ni kwa namna gani uamuzi wako wa kuwapa likizo wafanyakazi hawa watano kutakomesha vitendo vya ubadhirifu ambavyo, kwa taarifa ambazo mtandao wetu wa Jambo Forums unazo, vimekithiri katika Benki ya Posta.
Pamoja na kwamba hatupendi kuingilia utendaji wako wa kazi, hatukubaliani na uamuzi wako wa kuwapa likizo wafanyakazi watano wa Benki ya Posta kwa kuwahusisha na taarifa zilizopatikana katika mtandao wetu wa Jambo Forums. Tunapenda kukuhakikishia kuwa habari za ubadhirifu katika Benki ya Posta zilizopatikana katika mtandao wa Internet wa Jambo Forums [hazikutolewa na mfanyakazi yeyote wa benki hiyo]. Zaidi ya yote, tunapinga kwa nguvu zetu zote vitendo vyovyote vya kudhoofisha mapambano dhidi ya ufisadi na udhaifu wa kiutendaji kwa viongozi wa mashirika ya umma, kama kilichoonyeshwa na Benki ya Posta, kwa kuwatia hofu watu wenye nia njema ya kufichua vitendo hivyo vya ufisadi hapa nchini.
Kwa barua hii tunakushauri uondoshe adhabu uliyowapa wafanyakazi wako kwa kuwa hawahusiki kwa namna yeyote ile na taarifa za ubadhirifu wa Benki ya Posta kama zilivyoandikwa katika mtandao wa Jambo Forums.
Tuhuma zilizoandikwa JamboForums ni kidogo kulinganisha na kile tulichopewa kuhusiana na Benki ya Posta na wanasiasa wa Tanzania. Tulichofanya ni kutoa kwa ufupi tu nini kinaendelea ndani ya Benki yetu ya Posta, kwa nia ya kuwazindua na kuepuka kuibua "EPA" nyingine inayoweza kuendelea kuchafua ‘hali ya hewa' ya kisiasa nchini.
Wako katika ujenzi wa Tanzania bila ubadhirifu,
Invisible,
k.n.y Jambo Forums.
CC.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (Tuma watu makini kuchunguza)
Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo (Safisha kumbukumbu zako TPB)
Gavana Benki Kuu ya Tanzania
Kamishna Financial Intelligence Unit (FIU)
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
Vyombo vya Habari