JF yaisiadia CCM kujitambua

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Ndugu wanaJF wenzangu licha ya kejeli zinazoelekezwa kwa JF kutoka CCM hususan Makamu Mwenyekiti wake Ndg Pius Msekwa, JF kama chpmbo cha habari kimetimiza jukumu lake kilipoisadia CCM kurekebisha documentation zake zilizokuwa in shambles hususan orodha ya wajumbe wa Kamati Kuu kama ilivyokuwa ikionekana katika Tovuti zao.

Licha ya kuwa mwanaJF mwenzetu KABUNANGO kujitahidi kutetea uzembe huo lakini hatua za kurekebisha zimechukuliwa na hivi sasa tovuti ya CCM inaonyesha orodha mpya kama inavyosomeka hapo chini kuwa ndio wajumbe halali wa Kamati Kuu ya CCM. Kam kawaida ya CCM hawakosi usanii KABUNANGO anadai kuwa tovuti hizo zilikuwa hazijawa updated. Kama ni hivyo majina ya Wilsona Mukama, Nape Nnauye na January Makamba yaliingiaje na jina la Yusuph Makamaba na wenzie kuondokaje katika orodha iliyorekebishwa?

Je ni kwanini hasa nalivalia njuga suala hili? Ni kwa sababu ya kutaka kuonyesha jamii hususan vijana kuwa Nape na January Makamba hawako makini kama wanavyotaka tuamini. January Makamba katika wadhifa mpya wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa alitamba sana kuwa sasa CCM itaendeshwa kisasa na kwa kutumia teknolojia za kisasa. Alishindwa vipi kutambua kuwa muonekana wa CCM kimataifa ni kupitia tovuti yake ambayo ina majina ya Mafisadi waliotoswa na vikao vya chama?

Ikiwa January Makamaba ameshindwa kubaini athari za majina ya mafisadi waliotoswa na NEC kuendelea kuwemo katika orodha ya wajumbe wa Kamati Kuu mpya ya CCM kupitia tovuti ya CCM; atawezaje kuleta mitazamo mipya. Huu ni udhaifu mkubwa wa kwanza unaofanana kabisa na kitendo chake cha kuwatukana vijana wa vyuo vya elimu ya juu katika majukwaa kuwa eti wao kazi yao ni kusombwa kuzomea kuzomea tuu.

Natoa wito kwa Sekreterieti ya CCM pia kurekebisha maamuzi ya mkutano wa NEC kama inavyoonekana kwenye tovuti hiyo ili ile "ultimatum ya siku 90 kwa Mafisadi kujitoa ndani ya uongozi wa CCM" isomeka hivyo badala ya lugha ya kuchakachuliwa iliyopo katika ibara ya 5 ya Maamuzi ya mkutano wa NEC ya CCM wa tar 10 Aprili 2011 (in red hapo chini). Katika hili msione aibu kufanya marekebisho ni kwa faida yenu itawasaidia kuhalalisha matamshi yenu mnayoto hadaharani katika jitihada za kuipoka CHADEMA hoja ya UFISADI; hivyo onyesheni ujasiri katika sauala hilo badala ya kuwa na lugha ya kuoneana haya.

ORODHA YA WAJUMBE WA KAMATI KUU BAADA YA KUFANYIWA MAREKEBISHO KATIKA TOVUTI KWA SHNIKIZO LA JF.

1. Ndugu Jakaya Mrisho KIKWETE – Mwenyekiti
2. Ndugu Pius MSEKWA - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani KARUME - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Wilson MUKAMA - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) John Zefania CHILIGATI - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Vuai Ali VUAI - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed SHEIN – Mjumbe
8. Ndugu Mizengo Kayanza PINDA – Mjumbe
9. Alhaj Ali Hassan MWINYI – Mjumbe
10. Ndugu Benjamin William MKAPA - Mjumbe
11. Dr. Salmin AMOUR – Mjumbe
12. Ndugu John Samwel MALECELA – Mjumbe
13. Ndugu Nape NNAUYE - Mjumbe
14. Ndugu Mwigulu MCHEMBA - Mjumbe
15. Ndugu January MAKAMBA – Mjumbe
16. Ndugu Asha Abdallah JUMA – Mjumbe
17. Dr. Hussein Ali MWINYI
18. Dr. Maua Abeid DAFTARI
19. Ndugu Samia Suluhu HASSAN
20. Ndugu Omar Yussuf MZEE
21. Prof. Makame Mnyaa MBARAWA
22. Ndugu Mohammed Seif KHATIB
23. Ndugu Shamsi Vuai NAHODHA
24. Ndugu Abdulrahaman KINANA
25. Ndugu Zakiah Hamdani MEGHJI
26. Ndugu Abdallah Omar KIGODA
27. Ndugu Pindi Hazara CHANA
28. Ndugu Steven Masatu WASSIRA
29. Ndugu Constansia BUHIE
30. Ndugu William LUKUVI

5. KUHUSU TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU 2010

Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kujadili taarifa ya Tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, imeagiza mambo yafuatayo:-
(a) Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa Shukurani kwa wana CCM na wananchi kwa jumla kwa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi kwa kukipigia kura nyingi zilizokipa ushindi na hatimaye kuunda Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wananchi wanaombwa kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zingine zijazo.
(b) Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zimetakiwa zitekeleze ipasavyo Ilani ya CCM ya 2010-2015 kwa kadri Chama kilivyoahidi wakati wa kampeni; kama zilivyo tekeleze kwa ufanisi mkubwa Ilani iliyopita iliyopita ya Uchaguzi ya 2005-2010.
(c) Serikali zote mbili ziongeze kasi ya kushughulikia matatizo ya wananchi ili kuwaondolea kero zinazowakabili, hasa tatizo la kupanda kwa gharama za maisha.

(d) Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kiongeze kasi ya mapambano dhidi ya viongozi na wanachama wanaojihusisha na rushwa. Aidha viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa wajenge tabia ya kuwajibika wenyewe kwa maslahi ya Chama wasipofanya hivyo Chama kiwawajibishe kwa maslahi ya Chama na nchi

MY TAKE: kUBAKIZWA KWA MAJINA YA MAFISADI KATIKA TOVUTI YA CCM WAS A STRATEGIC MOVE YA KUWAPATIA MAFISADI HAO MUDA WA KUJIPANGA KURETALIATE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom