JF Wing Arusha yawakilisha msiba wa marehemu mama mzazi Smile

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Habari zenu wakuu.

Wengi wetu natumaini tulikuwa tuna habari juu ya msiba mzito uliompata Smile wa kufiwa na mama yake. Kupitia thread ile alijulisha mazishi yalikuwa leo (Jumatano).

Baada ya uzi huo kupandisha JF Wing Arusha tulijipanga kuona jinsi tutavyoweza kuwakilisha kwenye msiba huo. Tuliitisha kikao cha dharura na kufikia maazio ya kila mmoja kuchanga kwa jinsi atavyoweza.

Kwa moyo wa ajabu watu walijitoa na shukrani za pekee kwa wageni wetu tuliokuwa nao siku hiyo Kaizer na Dark City kwa kutupa support kubwa bila kusahau changamoto mbali mbali.

Hivyo leo ndiyo tuliopata nafasi ya kuwakilisha, kiukweli Smile ameshukuru sana ushirikiano wa wanaJF wote mliomsupport kuanzia kwenye thread mpaka wale waliompigia simu. Japokuwa alikuwa yupo katika wakati mgumu lakini aliendelea kufarijika kila dakika kutokana na jinsi ambavyo mlivyokuwa mkimfariji.

Kwa mantiko hiyo napenda kuwajuza hicho ndicho kilichoendelea leo hii katika sherehe ya kumuuaga mama yetu, mama Smile.

PakaJimmy, Preta, marejesho, LiverpoolFC, Lily Flower, Blaki Womani, sweetlady, Mamzalendo, Filipo, Mtumishi Wetu, Erickb52, Crashwise, Arushaone, Mungi, Jackbauer, Saharavoice,

IMG_0325.JPG
 
Last edited by a moderator:
Aksante Mzee wa Rula kwa uzi. This is how friendS should be!

Smile si mwana Arusha-Wing, lakini ni mwana-JF.
Kwa mantiki hiyo tulikuwa na kila sababu ya kumpa heshma anayopasa kwa kuwa tu MwanaJf!

Pia mazishi yalifanyika katika ukanda wetu-Moshi, kwahivo hapakuwa na namna ya kuukwepa msiba huu wa mama wa mdau mwenzetu.

Kwa mara nyingine nitoe shukran kwa wana-Wing walioguswa na msiba huu na kuwezesha gari mbili kujazwa full-tank na kuwahi eneo la tukio kuzika na kumfariji mwenzi wetu Smile.

Pumzika salama mama Smile-Amen.
 
Maneno haya yanastahili like 1000, kwa kuwa ndiyo ukweli. Nashukuru kwa kujazia nyama.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli nimeguswa sana na upendo wa kipekee wa arusha wing,nawashukuru kwa kusimama kidogo kunisalimu,nimefurahi sana kuwaona nimepata marafiki wazuri leo,nawapenda wote arusha wing,nimejua leo kuwa friends mean the world,najua mmempa smile faraja kubwa hakika ni baraka tele na hatasahau kamwe,
 
Back
Top Bottom